Samahanini wadau naomba kujuzwa nn tiba ya malaria sugu?

Samahanini wadau naomba kujuzwa nn tiba ya malaria sugu?

cleokippo

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2014
Posts
2,118
Reaction score
1,797
Wadau mm ni kijana mwenye afya njema tu, sema nimekuwa nikisumbuliwa na malaria mara kwa mara hali inayopelekea niwe nameza vidonge mara kwa mara kitu ambacho kiafya sio kitu kizur! nimepima vipimo vyote niko poa ila tatizo kubwa ndio ilo malaria za mara kwa mara, hivyo kwa yeyote anayefaham tiba nzur ya malaria naomba anijulishe ili nijaribu kutumia! aksanten sana!! Natanguliza shukran zangu
 
chukua maji ya dafu kamulia ndimu na limao kama saba hivi unywe glass moja kutwa mara tatu
 
Cleopkipoo.kwanza utambue kuanzia leo in medical hakuna malaria sugu.malaria ia treatable and curable disease.ni chanzo ni bite with infected female mosquito.anophelens gambience.or anophelense fenestus.la muhmu nenda hospital ya karibu mwone daktar atakusaidia zaid.
 
Kipi apo nikamulie, ndim.au limao? au vyote ndim na limao?
 
tiba ni kutumia chandarua,hata ukimeza quinine, marafine,artemether lumefantrine,,so, kama hutumii chandarua ni bure
 
Chandarua natumia xn, huwa siwez kulala bila chandarua
 
Yule anaejitangaza.itv amazo nahisi
 
Nashkuru kwa ushaur wako bhana chisagapipi
 
Pole braza
Huwa unapima kabla ya kunywa dawa ?
Na unapimia kituo gani ?
Maana huku mtaani maabara zimekuwa kama uyoga !
Hakuna qualified labaratory technician .
 
Hiyo siyo malaria. Tafuta maabara yenye ubora upime malaria na magonjwa mengine yanayofanana nayo. Pia wakumbushe wapime brucellosis. Ukikwama vipimo tutafutane
 
tiba ni kutumia chandarua,hata ukimeza quinine, marafine,artemether lumefantrine,,so, kama hutumii chandarua ni bure

Chandarua zetu nyavu za kudakia mbu tu kumbuka mbu mmoja tu aweza kukuletea malaria mseto ndio antibiotic ya nguvu huwezi kukwepa malaria kwa kulala kwenye nyavu zetu hizi
 
mashana jr Au mzizi mkavu naitaji kuongea na nyinyiw nitafute kwa namba izi 0763435277
 
Nimewahi kukutwa na tatizo kama lako pindi nilipokuwa najitambua as binadamu hadi form five! Niliugua mpaka nikafikiri nimeukwaaa...bahati mbaya nimekulia kwenye familia yenye kuamini haya madawa ya kizungu, basi nimeishatumia madawa hadi nikawa addicted sijui hizo fansida(sina hakika hata kama nimeweza kuzitamka) amodiaquine, meta...., quinine, chloroquine na mengine mengi (ya kichina) hata kutamka siwezi acha sindano na drip but bado malaria ilikuwa ni sugu! Nakumbuka nilikuja kumaliza hili tatizo kwa kufanya maamuzi magumu...nilikuwa nzega mwaka 2008 na nilikuwa najiandaa na mtihani wa kumaliza kidato cha tano, basi. Nikahisi hali sio njema...nikawaza kuwa endapo nitaenda hospital na kupewa dawa kuna kama siku nne za kulala bila kusoma nikaamua kuchukua aloe vera majani matatu yaliyokomaa vema nikayasafisha nikayakatakata na kutia kwenye brenda nikapata juice safi,(mchanganyo wa lita moja na nusu) nikapata glass moja muda ule ule jioni kama saa kumi na mbili! Nikajipumzisha mida ya saa nne usiku nikapata nyingine, na saa tisa usiku nyingine, asubuhi niliamka nikiwa safi sana nikamailizia dawa yangu vema! Nilikaa kama miezi mitatu bila malaria jambo ambalo sikuzoea hata kwa mwezi mmoja nikahisi dalili nikaludia tena, nikakaa kama miezi miwili nikaludia dozi bila kuwa na dalili yoyote ya kuugua nilijiskia tu kufanya hivyo! But kuanzia hapo mpaka leo malaria kwangu ni history, hata family yangu sasa ni mimea kwa kwenda mbele!
 
Na typhod pia jamani

Kwa typhoid kama huna vidonda vya tumbo chukua limao sita, vitunguu swaumu vinne au vitano viwe vikubwa hakika, then menya zile punje zake za kitunguu swaumu ( vyote vinne) tia kwenye brenda na maji kidogo sana ili visagike au tumia kinu ili kutoweka maji kabisa, (ila hakikisha vimegeuka kuwa uji) baada ya hapo kamua maji ya limao zote halafu changanya mchanganyiko huu kwenye chombo cha plastic, kioo au udongo. Baada ya hapo tia kwenye chupa ndogo ya plastic. Na uache ilale siku moja mbili au tatu ili iwe strong baada ya hapo asubuhi baada ya chai kijiko kimoja na mchana baada ya mlo fanya hivyo na usiku, ikiisha ludia mala mbili kwa mwenye typhoid sugu. ******* ANGALIZO*****Usijalibu kuitumia ukiwa mtupu tumboni utalia maana ni kali sana! niliwahi kuitumia asubuhi bila kitu tumboni mmmmm!!!!!! nilichokiona najua mwenyewe!
 
Poa emback nashukuru kwa ushaur wako
 
Back
Top Bottom