Nimewahi kukutwa na tatizo kama lako pindi nilipokuwa najitambua as binadamu hadi form five! Niliugua mpaka nikafikiri nimeukwaaa...bahati mbaya nimekulia kwenye familia yenye kuamini haya madawa ya kizungu, basi nimeishatumia madawa hadi nikawa addicted sijui hizo fansida(sina hakika hata kama nimeweza kuzitamka) amodiaquine, meta...., quinine, chloroquine na mengine mengi (ya kichina) hata kutamka siwezi acha sindano na drip but bado malaria ilikuwa ni sugu! Nakumbuka nilikuja kumaliza hili tatizo kwa kufanya maamuzi magumu...nilikuwa nzega mwaka 2008 na nilikuwa najiandaa na mtihani wa kumaliza kidato cha tano, basi. Nikahisi hali sio njema...nikawaza kuwa endapo nitaenda hospital na kupewa dawa kuna kama siku nne za kulala bila kusoma nikaamua kuchukua aloe vera majani matatu yaliyokomaa vema nikayasafisha nikayakatakata na kutia kwenye brenda nikapata juice safi,(mchanganyo wa lita moja na nusu) nikapata glass moja muda ule ule jioni kama saa kumi na mbili! Nikajipumzisha mida ya saa nne usiku nikapata nyingine, na saa tisa usiku nyingine, asubuhi niliamka nikiwa safi sana nikamailizia dawa yangu vema! Nilikaa kama miezi mitatu bila malaria jambo ambalo sikuzoea hata kwa mwezi mmoja nikahisi dalili nikaludia tena, nikakaa kama miezi miwili nikaludia dozi bila kuwa na dalili yoyote ya kuugua nilijiskia tu kufanya hivyo! But kuanzia hapo mpaka leo malaria kwangu ni history, hata family yangu sasa ni mimea kwa kwenda mbele!