- Tunachokijua
- Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa jambo hilo halina uhalisia wowote. Na licha ya kuwa hakuna taarifa sahihi ni wapi dhana hii ilipotokea lakini inatajwa kuwa, wafugaji waliitumia hii kama mbinu ya kuwaweka viumbe hao kwenye maeo yasiyo na nafasi ya kutosha wakiamini kwamba hawatojali sana kwani wanasahau baada ya muda mchache.
Makala iliyochapishwa na live science inamnukuu mtaalamu Culum Brown anaeleza kuwa jambo la kushangaza ni kwamba dhana hii imekuwepo karibu kila mahali duniani ikitofautiana kidogo kati ya eneo na eneo lakini wengi wanamtaja kuwa na uwezo wa kumbukumbu kati ya sekunde 2 hadi 10.
Tafiti zilizofanywa zinabainisha kuwa samaki "goldfish" ana uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu ambayo inaweza kufikia hadi zaidi ya wiki, miezi na hata miaka.
Tafiti za kisayansi zimeonyesha kuwa samaki wa dhahabu (goldfish) wanaweza kujifunza kazi mbalimbali, kutambua mifumo, na hata kutarajia ratiba za kawaida. Katika jaribio moja, goldfish walifundishwa kusukuma kifaa maalum kwa wakati fulani kila siku ili kupata chakula. Jambo la kushangaza ni kwamba walikumbuka jinsi ya kufanya hivyo hata baada ya kupita wiki kadhaa.