Samaki wa foil

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,151
PISHI LA SAMAKI WA FOIL

MAHITAJI:

-Foil,
-Samaki,
-Limao,
-Soya Sauce,
-Chumvi,
-Karot,
-Hoho,
-Nyanya,
-Garlic,
-Vitunguu na Kabichi

Unampaka kwanza samaki wako chumvi inakolea mpaka ndani, unamuwekea limao na garlic Kisha unaweka Foil unatandika mboga mboga kwa chini halafu unamuweka samaki juu yake

Hakikisha pia mboga zingine zinakaa ndani ya tumbo la samaki
Kama inavyoonekana kwenye picha

Malizia mboga zingine kwa juu ya samaki

Kisha unamwagia soya sauce vijiko 2 kuongezea ladha

Halafu mfunge kwenye foil, na uweke kwenye oven kwa dakika 30 - 45
Kwa wanaotumia kuchoma na jiko la mkaa
Inabidi iwe dk 15 upande mmoja na dk 15 unamgeuza upande wa pili ili aive kote kote
Ila kwa oven ukiweka moto unafika pote bila kugeuza

Baada ya hapo mambo yanakuwa hivi
Sio lazima uweke mboga zote hizo
Unaweza kupunguza vitu ambavyo huvipendelei
Ila ki afya vyote vilivyowekwa ndio vinakamilisha mlo.
ENJOY IT!
 
Nicee...shukraan dear

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Hapa najiona Nipo Bukoba Gymkhana Club!
 
Reactions: amu
nimate imenijaa halafu atm haisomi salio
 
nimate imenijaa halafu atm haisomi salio

pole mwaya ila ya kuandaa mwenyewe si ghali kama ya hotelini.huku arusha samaki wa foil ni bei moja na kuku wa kienyeji 15,000-12,000 lakini ukiandaa mwenyewe haifiki hata elf 15
 
Nasikia sio nzuri kiafya, huo mvuke unaokosa pa kutokea huku ukichanganyika na Protein inatengeneza vimelea vya kansa, ni ripoti za kitaa tu. Wataalamu mpo, napenda sana hii kitu
 
Nasikia sio nzuri kiafya, huo mvuke unaokosa pa kutokea huku ukichanganyika na Protein inatengeneza vimelea vya kansa, ni ripoti za kitaa tu. Wataalamu mpo, napenda sana hii kitu

dont tell me?! na nnavofakamiaga mikuku, mimbuz na misamaki ya foil bas ni balaa aisee hebu wataalam watusaidie kuthibitisha hili jamani ili niwe nachomea kwenye moshii
 
Nasikia sio nzuri kiafya, huo mvuke unaokosa pa kutokea huku ukichanganyika na Protein inatengeneza vimelea vya kansa, ni ripoti za kitaa tu. Wataalamu mpo, napenda sana hii kitu

Wai, kipi kizuri kwao?? yani kila kitu watakwambia sio kizuri kiafya..
ndio maana tunaomba kabla ya kula tunamwachia Mungu mustakabali wa afya zetu.

kama kitamu kula tu.
 
Wai, kipi kizuri kwao?? yani kila kitu watakwambia sio kizuri kiafya..
ndio maana tunaomba kabla ya kula tunamwachia Mungu mustakabali wa afya zetu.

kama kitamu kula tu.

thats true..Mungu ndiye mlinzi wetu
 
Nicee...shukraan dear

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

shogah mambo! Hivi naweza pika mandazi bila kuweka hamira?yatatokaje?yataiva? Kwa asieyetumia yeast.
 
i will cook this weekend! na napenda samaki! Thank you so much for sharing ameline
 
Last edited by a moderator:
Kesho naandaa hivyo, nadhani somo nimelielewa.
 
Hii ndiyo JF, kila siku kujifunza.Ahsante sana mleta mada.
 
Nasikia sio nzuri kiafya, huo mvuke unaokosa pa kutokea huku ukichanganyika na Protein inatengeneza vimelea vya kansa, ni ripoti za kitaa tu. Wataalamu mpo, napenda sana hii kitu

Wewe nawe umeleta jambo jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…