Samaki wa Magufuli wafufua mgogoro wa muungano?

Pathetic. Pamoja na kuwahifadhia bure, gharama za kuendesha kesi hawatachangia, na kama tukishindwa kwenye kulipa damages wataturuka kimanga! Halafu wakitubeza kuwa tunajipendekeza tunakasirikia nini?

Amandla.........

Aliyezoea vya kunyonga, vya kuchinja ataviweza ? Ngekewa ananikumbusha hadithi ya Maimuna wa bara !

Maimuna nenda kachange kuni
(Akiwa kajilaza)Haka mama naumwa mkono
Maimuna hebu kateke maji
(Akiendelea kulala)Hapana mama naumwa mguu
Maimuna kawashe jiko
Kweli mama naumwa mwili mzima
Maimuna kasonge ugali
Hakika mama simwezi hata kunyanyuka
Maimuna karibu mezani ule
(Akitoka mbio)Haya mama nakuja


Ngekewa kwa kupenda ngekewa naona hayuko peke yake ! Eti wanalilia samaki - labda kitakachofuata ni maandamano !
 
Sishangai hao jamaa kudai samaki,watu wa visiwani akili zao kama vile zina tatizo hivi!!!huu muungano wajameni siku ukifa kwanza watalia na kusaga meno kabla ya kumalizana hadi vichanga vyao kwa mapanga, halafu watakosa hadi hayo mafuta hewa yao ya kuwawezesha kukimbilia tena bara, kazi yao kulalamika tu kama mademu wapenda chips, wanakera hao! Wakishapewa samaki watataka na pweza wa bara haoo!!1
 

Mafuta gani hayo tunayogombea? mafuta gani ya Mtwara tunayowanyima? Hizi ndiyo ndoto za alinacha. Kitu hata khakijapatikana mnaanza kutumia!

Hivi mpka kati ya Tanzania na Zanzibar uko wapi? Hilo eneo la maili 200 ya bahari ya Zanzibar si litafika mpaka Morogoro?

Amandla..........
 

Pumba tupu!Muungano upo kwa muda wa miaka 45 tuu, jee visiwa vya Zanzibar na taifa la Zanzibar lipo duniani tokea lini?Kama umemaliza angalau elimu ya msingi, utaweza kugundua Zanzibar itasaga mawe au itaendelea zaidi.

@Joka Kuu
Shukurani mzee kwa maelezo hayo, ni mara ya pili nakutana nayo.Huo ni ushahidi wa kuwa Zanzibar na Tanganyika ni partners, na sio kama wengi watanganyika wanavyofikiria kuwa Zanzibar ni mzigo kwenye muungano huu.

Huu muungano kwa vyovyote vile, kama itathibitika kuwa unahitajika sio tatizo kubwa.Zipo nchi zimeungana na zinafanya vizuri ikiwemo UK, US, EU n.k.Tatizo liliopo ni mfumo wake una lots of loop holes, na mwishowe ni kuwa haki hazitendeki na upande mmoja kuona kuwa unabanwa.

Cha msingi ni kuchukua wataalamu ndani ya nchi na nje ya nchi, kuunda mfumo mbadala wa muungano.Hata mie sitopendelea kuenda Arusha nikahitajika kulipia visa,nimeshaenjoy sana muungano wa EU kwa kucross boarders.Ni raha sana sasa ivi ambapo nchi zimeunganishwa kushinda ilivyokuwa awali, kutembea Ujerumani kuingia Holland ni lazima upitie Immigration.Sasa hivi unapita na gari lako huku umefunga vioo hakuna anaekusumbua njiani, sijuwi kama mutanifahamu hapo.

Lakini hizi nchi ziko huru, kila nchi ina mamlaka yake kamili na kujiamulia inavyopenda.Sasa leo Zanzibar ikitaka kujiunga na OIC, haiwezekani!
Zanzibar ikitaka kujiunga na FIFA, haiwezekani!Zanzibar ikitaka kufanya chochote haiwezekani, sasa unatarajia kutoka kwangu kama mzanzibari?Vunja ili iwezekane!...period!
 


Mzee wa Maimuna naona unashindwa kujibu hoja. Hivyo alipwe nani hizo pesa? Na jee mbali ya huyo Magufuli ni waziri gani aliingilia hilo? Hivyo kwa akili yako kinato kila mmoja ashiriki katika kesi jee hiyo mahakama itakua inajua mdai ni nani na wakusikilizwa nani? Mbona mmejaa upumbavu kuweni na hoj na kueleza kuwa hao Zanzibar wamlipe nani? Na hao wanaolipwa ni nani ? Jaribu kujibu masuwala hayo mawili halafu kama bado una ubavu tuendelee.
 

Joka Kuu nakupa heshima kwa kujadili kwa hoja na hii inaonyesha unayotamka unatamka kwa nia njema .
Kuhusu hili la Law of Sea pengine umepitikiwa kuwa panapozungumziwa high seas panazungumziwa upeo ambao hakuna muingiliano wa mipaka kati ya nchi mbili na hivyo kuifanya nchi kudai sehemu kubwa inayoitangulia.
Kwa mfano kati ya Zanzibar na Tanganyika hakuna suwala la High sea kati yao bali kinachotambulika ni mipaka iliyowekwa hapo mwanzo wa kuasisiwa ujirani wa nchi mbili hizi. Ukichukua maili mia 200 kutoka pwani ya Tanganyika utaivuka hata hiyo Zanzibar yenyewe na ukichukua maili 200 kutoka Zanzibar utafika Kibaha. Hii yote ni kuonyesha kuwa suwala la maili 200 lia apply sehemu zenye ujirani kama huo kama vile pwani ya Tanganyika pengine na Comoro.
Mfano mwengie ni nchi za Ghuba ambako mipaka yao ya Bahari haifiki maili200 lakini hakua sehemu wanayogawana maliasili kwa vile mipaka ya asili ndiyo inayoamuwa.
 

Sasa kwani Tanganyika na Zanzibar zimepakana upande gani?Kwa upande wa kulia ya Zanzibar, Tanganyika hamna chenu!

Sijuwi hata mutaingia vipi na meli hapo bandarini kwenu Dar teh teh teh...
 


Mzee ndio umeamka? Naona unakurupuka tu si uje taratibu ili ubonyezwe kihuku?

Unaonaje hizo maili200 zikianzia kizingo Zanzibar? Labda Kibaha nayo itakuwa sehemu ya Zanzibar.
 
No reason to pretend we both knew it will end this way one day .

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=otuwNwsqHmQ"]http://www.youtube.com/watch?v=otuwNwsqH[/ame]
 
Mzee ndio umeamka? Naona unakurupuka tu si uje taratibu ili ubonyezwe kihuku?

Unaonaje hizo maili200 zikianzia kizingo Zanzibar? Labda Kibaha nayo itakuwa sehemu ya Zanzibar.

Jibu swali, Mkuu. Kebehi hazisaidii kitu.

Nautical mile moja ni sawa na 1.852 km. nautical mile 200 ni zaidi ya kilometre 360. Kwa mtaji huo utakuwa umebakiza kilometa 86 kuingia Dodoma! Wewe unazungumzia Kibaha!

Amandla.......
 
Jibu swali, Mkuu. Kebehi hazisaidii kitu.

Nautical mile moja ni sawa na 1.852 km. nautical mile 200 ni zaidi ya kilometre 360. Kwa mtaji huo utakuwa umebakiza kilometa 86 kuingia Dodoma! Wewe unazungumzia Kibaha!

Amandla.......

Baba yangu hapa hapakuwa na kejeli bali ni kuulizwa tu kuwa kwanini unauliza maswali ambapo hapana maswali?
1, Mafuta tunayogombea hivyo wewe hujui nini kinaendelea kuhusu hicho?
2. Niliposema mafuta yakipatikana Mtwara nakusudia kuwa hiyo ni sehemu ya Tanganyika ambayo Wazanzibari hawwezi kudai.
3. Aliezungumza maili 200 kuwa ndio mipaka ya bahari alihitajiwa kuulizwa yeye suwala hilo kwani kama unavyosema maili200 itakuwa kuingiliana.
Samahami kama ilkuwa kejeli!.
 

Nilikuwa natafuta mfano wa nchi ambazo zimepakana, na mwishowe nimepata.India na Srilanka, zimepaka almost the same baina ya Zanzibar na Tanganyika na zinaishi bila conflict yoyote ya boarders.

P:S
**Feel free to correct me, I havent made exact distance calculations on this
 
Zanzibar very soon will be another mkoa in the EAC !
 
Sasa nyie wazenji kama mlitaka samaki kwanini hamkuomba? maana hao waliopewa waliomba. Nia ya kugawa samaki ilitangazwa miezi kadhaa kabla, na wao waliona, kwanini hawakuongea na Mheshimiwa magufuli ili wapate hiyo share? Sasa ka mlisubiri kupewa bila kuomba au kuonesha nia, endeleeni kusubiri. Na Muungano hatuvunji kwa sababu hatukuungana kwa ajili ya samaki !
 
Kwanini Zanzibar haikupeleka ombi kwa Magufuli kuomba samaki?

Sasa kwani mulisikia Zanzibar ni mtoto yatima anaepita na kuomba omba samaki?Hatuna dhiki ya samaki, hao samaki waliokaa zaidi ya mwaka nani anawataka huko Zanzibar?Tutaendelea kutumia kila fursa itakayopatikana katika muungano kupiga bakora, kwa hiyo kaeni mkao wa fisi!


Na Muungano hatuvunji kwa sababu hatukuungana kwa ajili ya samaki !
Kwani aliesema uvunjwe nani?Au unajishtukia?Umeambia uzingatie katiba na kupeleka samaki huko visiwani, hujaambiwa kama uvunje muungano.Mie nimesoma hapo Dar tuition, na nimekusomeni vizuri wadanganyika tabia zenu ni mdomo mkubwa na mikwala mingi.Lakini ni laini sana kwa undani, sie wala hatusemi muungano uvunjwe tutacheza na hiyo katiba mbovu iliopo...hadi mutachoka na kusema uvunjike.
 
Code:
Code:

We ngekewa acha kuropoka kama mwendawazimu. Sasa kama pesa za kuhifadhiqa hao samaki zimetokana kwenye Muungano, waliopewa hao samaki pia si wana Muungano huo huo? Ulipaswa upongeze kuwa Watanzania wote wa bara na wazanzibari wamepewa samaki tena bure.

Muungano hauvunjwi, hakuna kidume cha kuvunja muungano na kama unadhani Zanzibar mnaonewa basi mtaonewa hadi vitukuu wa vitukuu vyako!

Usituandikie upupu wako humu. Nyambaf!
 

Haki inaombwa? Haki inaombwa? Sasa na nyie hamjuwi kuwa kuna makubaliano na kuna Muungano?
Hii tabia yenu ya kuifanya Zanzibar ni sawa na Taasisi yenu ya Tanganyika(magereza, mashule, jeshi) inakwenda kinyume na suala la Umoja. Una maana Zanzibar unaiona sawa na magereza?
 

WEWE ni mzito wa kufahamu na Kabwela wa akili.
Hebu rejea thread na uone ulivyo kabwela wa akili. Kama lazima useme basi chagua wa saizi yako.
 
wewe acha kidomodomo ,wakati zenji ilipoendelea ,tanganyika lilikuwa ni pori tu. zenji ilianza kurudi nyuma kimaendeleo baada ya hili muungano hasa hasa pale nyerere alipojifanya mjanja wa kuunganisha vyama.

tupeni nchi yetu, kama tutauwana au tutakufa njaa, kumbuka tu ,dua lenu ni la kuku. tumechoka!
 
Mimi hufurahi sana tunapojadili Zanzibar, maana nyinyi wenzetu wa bara muna akili kweli kweli. Akili za ubabaishaji na udanganyifu. Hivo miaka 45 imepita ya muungano feki na bado tu munafikiria mutaendelea kuwa kandamiza wazanzibari na hawatashituka?.
Zanzibar wana matatizo ya umeme, Kuna viongozi wa CCM wanasema maadamu Amani ana Makubaliano na CUF basi wazanzibari watakaa kizani tu.
Sasa nyinyi wabara munataka kitu gani?. Sisi tumekwisha waambia kuwa hatutaki muungano, kinacho wafanya mulalamike tunapodai posho yetu ni nini?. Muungano ulikuwa ni wa nchi mbili sio mkoa na nchi. Lazima tufahamiane. Muungano ulikuwa baina ya Tanganyika na Zanzibar. Hii propaganda munayoitia ukumbini kuwa sisi wazanzibari ni kidogo, tunadai 40% sijui kinyokonyoko gani kinyoko nyoko gani, haya ni mambo limbukeni. Njooni tuzungumze namna gani tutagawa kilicho bakia. Nyinyi muwe na kwenu na sisi tukae kwetu visiwani. Mukitaka biashara na sisi sawa na kama hamutaki kufanya bishara pia ni sawa. Zanzibar hatutegemei bara kwa chochote bali munatuibia mapato yetu kwa kisingizio cha muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…