Sishangai hao jamaa kudai samaki,watu wa visiwani akili zao kama vile zina tatizo hivi!!!huu muungano wajameni siku ukifa kwanza watalia na kusaga meno kabla ya kumalizana hadi vichanga vyao kwa mapanga, halafu watakosa hadi hayo mafuta hewa yao ya kuwawezesha kukimbilia tena bara, kazi yao kulalamika tu kama mademu wapenda chips, wanakera hao! Wakishapewa samaki watataka na pweza wa bara haoo!!1
Pumba tupu!Muungano upo kwa muda wa miaka 45 tuu, jee visiwa vya Zanzibar na taifa la Zanzibar lipo duniani tokea lini?Kama umemaliza angalau elimu ya msingi, utaweza kugundua Zanzibar itasaga mawe au itaendelea zaidi.
@Joka Kuu
Shukurani mzee kwa maelezo hayo, ni mara ya pili nakutana nayo.Huo ni ushahidi wa kuwa Zanzibar na Tanganyika ni partners, na sio kama wengi watanganyika wanavyofikiria kuwa Zanzibar ni mzigo kwenye muungano huu.
Huu muungano kwa vyovyote vile, kama itathibitika kuwa unahitajika sio tatizo kubwa.Zipo nchi zimeungana na zinafanya vizuri ikiwemo UK, US, EU n.k.Tatizo liliopo ni mfumo wake una lots of loop holes, na mwishowe ni kuwa haki hazitendeki na upande mmoja kuona kuwa unabanwa.
Cha msingi ni kuchukua wataalamu ndani ya nchi na nje ya nchi, kuunda mfumo mbadala wa muungano.Hata mie sitopendelea kuenda Arusha nikahitajika kulipia visa,nimeshaenjoy sana muungano wa EU kwa kucross boarders.Ni raha sana sasa ivi ambapo nchi zimeunganishwa kushinda ilivyokuwa awali, kutembea Ujerumani kuingia Holland ni lazima upitie Immigration.Sasa hivi unapita na gari lako huku umefunga vioo hakuna anaekusumbua njiani, sijuwi kama mutanifahamu hapo.
Lakini hizi nchi ziko huru, kila nchi ina mamlaka yake kamili na kujiamulia inavyopenda.Sasa leo Zanzibar ikitaka kujiunga na OIC, haiwezekani!
Zanzibar ikitaka kujiunga na FIFA, haiwezekani!Zanzibar ikitaka kufanya chochote haiwezekani, sasa unatarajia kutoka kwangu kama mzanzibari?Vunja ili iwezekane!...period!