Samaki wa Magufuli

Samaki wa Magufuli

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
01Jul 2021
WAANDISHI WETU
Dar es Salaam
Habari
Nipashe
Mtihani samaki wa Magufuli
WAKATI upande wa utetezi ukisubiri kutekelezwa kwa hukumu ya serikali kulipa fidia ya mabilioni ya shilingi kutokana na kukamata meli ya Tawariq 1 iliyokuwa na samaki mwaka 2009, maarufu Samaki wa Magufuli, serikali imesema inafikiria kuiuza meli hiyo kama chuma chakavu.

mee.jpg
Meli ya Tawaliq 1 iliyokamatwa mwezi Machi, 2009 ikiwa na tani za samaki aina ya Jodari, iliyowavua katika Bahari ya Hindi ndani ya Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), wakati ilipoanza kuzama mahala ilipoegeshwa upande wa Kigamboni, mkoani Dar es Salaam. Picha nyingine; meli hiyo ikionekana kidogo jana, baada ya sehemu kubwa kuzama kabisa. PICHA: MIRAJI MSALA/MAKTABA
Meli hiyo iliyodaiwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na samaki wenye thamani ya Sh. bilioni 2.074, ilikamatwa Machi 8, 2009 na boti ya askari wa doria wa Tanzania, Afrika Kusini na Botswana. Ilidaiwa leseni waliyokuwa nayo ilikuwa imemaliza muda wake Desemba Mosi, 2008.

Wiki iliyopita, Nipashe ilimtafuta Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, kuzungumzia suala hilo na alisisitiza utekelezaji wa hukumu iliyotolewa na mahakama unafanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Akizungumza na Nipashe kuhusu suala hilo jana, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, alisema:
"Ile meli bado iko pale ilipowekwa na 'actually' imeziba nafasi. Sisi tulianza kufikiria tuiuze kama chuma chakavu kwa sababu imeziba nafasi ambayo meli zingine zinaweza kuwekwa pale.

"Kwa ufafanuzi zaidi wa suala lenyewe, ninaomba nipate muda zaidi nione hatima ya serikali kupata fedha kwa maana tupige bei kama chuma chakavu ile meli iachie nafasi. Kwa hiyo, lile suala ni kama limeisha lakini bado halijaisha."

Machi 2017 kampuni ya uwakili iliyokuwa inawatetea 'Wachina wa Samaki wa Magufuli', ilitarajiwa kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Bahari kujua hatima ya madai yao ya meli ya Tawariq 1 yenye thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na zaidi ya Sh. bilioni mbili za samaki endapo hukumu haitatekelezeka.

Kampuni hiyo ilikusudia kuchukua uamuzi huo endapo hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti, mwaka 2014 haitatekelezeka.

Hatua huyo imefikiwa kutokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kwamba suala hilo lirudi Mahakama ya Kisutu ambako amri ya kurejeshewa vitu hivyo ilitolewa.

MAHAKAMA KUU
Uamuzi wa kuwataka wadai kudai utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya Kisutu ulitolewa na Jaji Munisi kutokana na hoja za Jamhuri.
Aliyekuwa Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis katika hoja za pingamizi alidai Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam haiwezi kusikiliza maombi ya ‘Wachina wa Samaki wa Magufuli‘ ya kutaka kurejeshewa meli yao iliyozama na samaki kwa sababu amri ya kurejeshewa ilitolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Upande huo wa Jamhuri ulidai mwombaji katika maombi hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tawariq, Said Mohammed, hana sifa ya kukabidhiwa mali hiyo, hivyo waliomba mahakama itupilie mbali maombi ya kutaka kurejeshwa meli ya Tawariq 1 na zaidi ya Sh. bilioni mbili za tani 296.3 za samaki.

Pics%20pg%201.JPG
Maombi hayo yalitokana na kesi iliyokuwa inawakabili Nahodha wa Meli, Hsu Chin Tai na Wakala wa Meli ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing.
Wachina hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari ya Tanzania.

Vitalis alidai haiwezekani maombi hayo yapelekwe Mahakama Kuu kwa sababu Mahakama ya Kisutu ilishaamuru mali akabidhiwe mshtakiwa wa kwanza aliyekuwa kapteni wa meli hiyo.

Alidai Mahakama ya Rufani ilishafuta mwenendo wa kesi ya msingi wa Mahakama Kuu, hivyo maombi hayo ni batili na hayawezi kusikilizwa na kutolewa amri mbili katika mahakama mbili zinazohusu kitu kimoja.

Jamhuri ilidai kama wadai wana hoja waziwasilishe katika mahakama iliyotoa amri hiyo ambayo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mdai katika maombi alikuwa ni mwajiri wa Wachina hao, Said Mohammed, akiwakilishwa na Mawakili Kapteni Ibrahim Bendera na John Mapinduzi.

Mawakili hao walifungua kesi hiyo kwa hati ya dharura dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wakidai Meli ya Tawariq 1 yenye thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na Sh. 2,074,249,000 ambazo ni gharama za samaki zilizofanyiwa uthamini Oktoba Mosi 2009.
Meli hiyo ilifanyiwa uthamini mwaka 2008 na kuonyesha kwamba thamani yake ni Dola 2,300,000. Ripoti hiyo ilitolewa na Kampuni ya Cambodia Shipping Services Ltd.

Akijibu hoja za Jamhuri, Kapten Bendera alidai kuwa waliwasilisha maombi hayo mahakamani hapo kwa sababu Mahakama ya Kisutu ilikataa kurejesha mali hizo kwa mshtakiwa wa kwanza.

Kapteni Bendera alidai waliwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu kwa sababu vielelezo vilitolewa katika mahakama hiyo wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi.

MAHAKAMA YA KISUTU
Agosti mwaka 2014, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru washtakiwa katika kesi ya 'Samaki wa Magufuli’ na kuamuru Jamhuri iwarejeshee vitu vyao, ikiwamo meli ya Tawariq 1.

Washtakiwa hao waliachiwa kwa mara ya pili -- mara ya kwanza waliachiwa na Mahakama ya Rufani Machi 28, 2014, lakini walikamatwa tena na kushtakiwa upya kwa mashtaka hayo hayo yaliyofutwa.

Septemba Mosi, 2014, wadai waliwasilisha barua mbele ya Msajili wa Mahakama hiyo wakiomba mahakama iwarejeshee vielelezo vilivyotolewa mahakamani wakati kesi namba 38 ya mwaka 2009 mbele ya Jaji Radhia Sheikh iliposikilizwa.

Barua hiyo ilivitaja vielelezo hivyo kuwa ni meli ya uvuvi Tawariq 1 pamoja na Sh. 2,074,249,000 za tani 296.3 za samaki walizokutwa nazo washtakiwa ambavyo vilitolewa Oktoba Mosi, 2009 mbele ya Jaji Sheikh.

UFAFANUZI KISHERIA
Jana, Wakili Reuben Simwanza aliiambia Nipashe kuwa endapo upande wa Jamhuri unashindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kurejesha vielelezo kwa mshtakiwa ama washtakiwa walioshinda kesi, hatua ya kwanza ya kuchukua ni kuandika barua kwa 'incharge' wa mahakama husika.

Kama barua imeandikwa kukumbushia na hakuna utekelezaji wowote, wahusika ama wadai wa vielelezo hivyo wanapaswa kuchukua hatua ya pili ambayo ni kuishtaki Jamhuri ama Ofisi ya DPP kwa kukaidi amri ya mahakama.
 
Naona Mawakili wetu Wasomi wameshanusa harufu ya mnuso wa fidia! Siyo kwa kupambana huko dhidi ya nchi yao, huku msababishi wa hayo madudu yote akiwa ameshaimaliza tayari safari yake hapa duniani.
 
Ile ilikua ni serikali ya kushika tu
Yaani inashika watu pamoja na vitu
Huu ni uzembe wa hawa wakurupukaji
Walipe fidia tu kwani hamna namna!
Usiongee kama umekatwa kichwa.
Hiyo meli ilikamatwa kwenye EEZ ya Tanzania ikivua bila kuwa na leseni kwa mujibu wa Sheria ya masuala ya Uvuvi.

Hiyo ilikuwa ni 2009 kama una chuki na hayati Magufuli jitahidi kumuomba Mungu akupunguzie chuki, pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu bado Magufuli alikuwa mpambanaji na mpenda nchi yake.
 
Usiongee kama umekatwa kichwa.
Hiyo meli ilikamatwa kwenye EEZ ya Tanzania ikivua bila kuwa na leseni kwa mujibu wa Sheria ya masuala ya Uvuvi.

Hiyo ilikuwa ni 2009 kama una chuki na hayati Magufuli jitahidi kumuomba Mungu akupunguzie chuki, pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu bado Magufuli alikuwa mpambanaji na mpenda nchi yake.
Ndio umeongea ugoro gani huu?
Kwa hio ndio mlikua mmedanganyana kua chochote chenye leseni iliopitwa na muda ni mali yenu?
Sasa kwa maamuzi haya ya mahakama bado unajisifu kua una akili?
Mliendesha mambo bila kutumia akili kwakweli inabidi mtuombe radhi wanyonge
 
Usiongee kama umekatwa kichwa.
Hiyo meli ilikamatwa kwenye EEZ ya Tanzania ikivua bila kuwa na leseni kwa mujibu wa Sheria ya masuala ya Uvuvi.

Hiyo ilikuwa ni 2009 kama una chuki na hayati Magufuli jitahidi kumuomba Mungu akupunguzie chuki, pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu bado Magufuli alikuwa mpambanaji na mpenda nchi yake.
hovyo sana meko
 
Hii nchi ina maruki wengi mliokalia kuipinga nchi yenu hata mtu afanye kitu kizur kwa ajili ya nchi!!

Mko upande wa wakoloni siku zote!! Ndyo kilichotokea enzi za nyuma nchi ikaingiliwa na wakoloni
 
Hii nchi ina maruki wengi mliokalia kuipinga nchi yenu hata mtu afanye kitu kizur kwa ajili ya nchi!!

Mko upande wa wakoloni siku zote!! Ndyo kilichotokea enzi za nyuma nchi ikaingiliwa na wakoloni
Sisi ni wajukuu wa wale machifu waliowauza ndugu zao kwa wazungu halafu wakapewa malipo ya shanga.

Ni DNA zile zile zisizojielewa vichwani.
 
Ndio umeongea ugoro gani huu?
Kwa hio ndio mlikua mmedanganyana kua chochote chenye leseni iliopitwa na muda ni mali yenu?
Sasa kwa maamuzi haya ya mahakama bado unajisifu kua una akili?
Mliendesha mambo bila kutumia akili kwakweli inabidi mtuombe radhi wanyonge
We acha chuki zako
Hiyo meli ilikamatwa kwa mujibu wa sheria na kushikiliwa kwake ni kwa kufuata utaratibu, na ulipoona Serikali imeshinda ni kwa mahakama hizo hizo, na kama hukumu imetenguliwa ni kwa kupitia mahakama hizo hizo.
Unapo attack watu personally inakuwa kama chuki dhidi ya watu hao.
 
Ndio umeongea ugoro gani huu?
Kwa hio ndio mlikua mmedanganyana kua chochote chenye leseni iliopitwa na muda ni mali yenu?
Sasa kwa maamuzi haya ya mahakama bado unajisifu kua una akili?
Mliendesha mambo bila kutumia akili kwakweli inabidi mtuombe radhi wanyonge
Uombwe radhi kama nani? Haha

Unaonekana una msongo wa mawazo. Tafuta pesa boss, acha kulialia. Kumchukia Magufuli ambaye ameifanyia mambo makubwa nchi hii haikusaidii chochote.

Unayemchukia amekufa akiwa anashika cheo kikubwa kuliko vyote Tanzania. Tafuta pesa upunguze msongo wa mawazo.
 
"Kwa hiyo, lile suala ni kama limeisha lakini bado halijaisha." Hahah.
 
We acha chuki zako
Hiyo meli ilikamatwa kwa mujibu wa sheria na kushikiliwa kwake ni kwa kufuata utaratibu, na ulipoona Serikali imeshinda ni kwa mahakama hizo hizo, na kama hukumu imetenguliwa ni kwa kupitia mahakama hizo hizo.
Unapo attack watu personally inakuwa kama chuki dhidi ya watu hao.
Ana msongo wa mawazo. Atafute pesa itamsaidia kupunguza chuki na visasi visivyokuwa na mbele wala nyuma.
 
Na bado Kuna makesi mengi tu kwny mahakama za kimataifa sababu ya maamuzi ya bwana yule.
 
Magufuli aliipenda nchi yake na alikuwa mzalendo kwelikweli.

Vizazi na vizazi vitamuenzi kwa kuipenda Tanzania kwa dhati na kuitakia mafanikio ya kweli - kupata uhuru wa kweli kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, na katika nyanja nyingine za maisha.

Apumzike kwa amani mbinguni.
 
Back
Top Bottom