Samaki wapungua kwa sababu ya kushamiri uvuvi haramu, wawekezaji walalamika

Samaki wapungua kwa sababu ya kushamiri uvuvi haramu, wawekezaji walalamika

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,521
Reaction score
4,381
Wawekezaji wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki mkoani Mwanza wamelalamikia uhaba wa malighafi unaochangia kupungua kwa uzalishaji unaodaiwa kusababishwa na shughuli za uvuvi haramu.

wazalishaji hao wamesema uzalishaji umepungua kwa kasi kutoka tani 200 kwa siku mpaka tani 14 kwa sasa na hali hii imesababisha kuyumba kwa biashara hata mapato ya serikali kupungua.
 
Huu ndio ujinga!! Wao waliokuwa wanavua tani 200 ndio waliosababisha kufikia tani 14 sasa!!

Samaki ni kama miti ya mazao. Samaki wana msimu na lazima wapatiwe muda wazaane!! Fishing quotas lazima ziwepo tena kwa mwaka ili samaki wapata nafasi ya kuzaliana!! Hatuna usimamizi katika maki zetu, zitapotea tu na tusifaidike. Ulaya hata baharini kuna quota ya uvuvi kwa mwaka na hii inasaidia kutoa nafasi ya kuzaliana huku bei za bidhaa za samaki zikipata bei ya juu.

Na wanaolalamika hivi huenda hawana na wala hawashiriki katika kufanya sustainable fishing. Kama tunavosema “panda mti kata mti” ndivo inavopaswa kuwa kwa samaki na hata mifugo mingine!!
 
Fishing quotas lazima ziwepo tena kwa mwaka ili samaki wapata nafasi ya kuzaliana!! Hatuna usimamizi katika maki zetu, zitapotea tu na tusifaidike
Ndiyo maana nimemchagua waziri kichaa kama mimi
 
Mleta Mada nimemzoea akileta habari za Mbowe,

sasa Jukwaa la siasa mnapokea mambo ya samaki wakati Waziri Mpina alikuwa akichoma nyavu mnamnanga mpaka Mwendazake akamtoa, leo atakumbukwa
 
Mleta Mada nimemzoea akileta habari za Mbowe,
sasa Jukwaa la siasa mnapokea mambo ya samaki wakati Waziri Mpina alikuwa akichoma nyavu mnamnanga mpaka Mwendazake akamtoa, leo atakumbukwa
 
#HABARI: Wawekezaji wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki mkoani Mwanza wamelalamikia uhaba wa malighafi unaochangia kupungua kwa uzalishaji unaodaiwa kusababishwa na shughuli za uvuvi haramu.
wazalishaji hao wamesema uzalishaji umepungua kwa kasi kutoka tani 200 kwa siku mpaka tani 14 kwa sasa na hali hii imesababisha kuyumba kwa biashara hata mapato ya serikali kupungua
Juzi tu hapa nlijaribu kukaa na baadhi ya wamiliki wa mitumbwi na wavuvi ili nijue changamoto wanazopitia katika shughuli zao!

Wao wanasema Samaki na Dagaa wamekuwa adhimu kuwapata toka kipindi kile walipokuwa wakichomewa nyavu zao, na kutaifishwa kwa machine na mitumbwi yao, kwa hyo wao kwa akili ya kawaida wanadhani ni kwa sababu ya moshi uliokua ukitanda ziwani tokana na uchomwaji wa nyavu zao!
 
Huu ndio ujinga!! Wao waliokuwa wanavua tani 200 ndio waliosababisha kufikia tani 14 sasa!...
Sidhani kuwa mleta mada anauelewa wa uliyoandika hapa mkuu; yeye anachojua ni kushabikia, siyo siasa, kwa sababu hata yenyewe haijui, bali anashabikia mtu anayemdhania anatimiza maslahi yake.
 
#HABARI: Wawekezaji wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki mkoani Mwanza wamelalamikia uhaba wa malighafi unaochangia kupungua kwa uzalishaji unaodaiwa kusababishwa na shughuli za uvuvi haramu...
Chanzo cha habari tafadhali, TAGANIST at his finest
 
#HABARI: Wawekezaji wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki mkoani Mwanza wamelalamikia uhaba wa malighafi unaochangia kupungua kwa uzalishaji unaodaiwa kusababishwa na shughuli za uvuvi haramu.
wazalishaji hao wamesema uzalishaji umepungua kwa kasi kutoka tani 200 kwa siku mpaka tani 14 kwa sasa na hali hii imesababisha kuyumba kwa biashara hata mapato ya serikali kupungua
hawana faida, waache samaki wetu kama kuvua tutavua na kuwala hapahapa, wanavua samaki na kupeleka ulaya na sisi tunapata faida kidogo sana, imagine umefuga samaki ziwani, alafu mtu toka ulaya huko anakuja anaweka kiwanda na kuanza kuvua na kupeleka kwao kuuza anapata hela yake, wewe anakuachia kakamisheni kadogo tu, zikipungua anaanza kulalamika. wakwende zao.
 
Teknolojia ya uvuvi wa ziwa victoria imepitwa na wakat na haiendani na rasilimali iliopo na uhitaji wa soko ni mkubwa kuliko kinachopatikana.

Wadau wa uvuvi wajielekeze katika uvuvi kwenye bahari kuu kwa kuweka mazingira rafiki kwa wazawa kupata zana za uvuvi kwa gharama nafuu na kupewa mafunzo ya uendelezaji uvuvi na mikopo yenye riba nafuu ikiwezekana.

Ufugaji wa samaki katika mabwawa na vizimba unaweza kuwa suluhisho la uvuvi haramu.

Sasa je sera zimekaaje hapo?

Unakuta vifaa vya kusimika miundombinu hiyo vinagharama kubwa kupatikana.
 
Back
Top Bottom