Samaki wasio na mapezi na magamba hawaruhusiwi kuliwa

Maandiko katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:9-12, yanasema:
9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.
10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu,
11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.
12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.

Mapezi ya samaki ni nini
Hivi ni vile vitu kama mbawa ngumu zenye mfano wa miiba zinazokaa kwa juu, au pembeni, au nyuma mwa mwili wa samaki. Ukitazama samaki kama perege, sato au sangara, utaona mapezi yao.
Faida za mapezi hayo ni kuwa yanasaidia kuogelea, kuelea vema kwenye maji, kukunja kona, kuongeza kasi, kusimama au kugeuka kwa haraka.

Magamba ya samaki ni nini
Halikadhalika, samaki waliokuwa na magamba ndio tu walioruhusiwa kuliwa. Magamba yaliwasaidia kujilinda na maadui au wadudu wavamiaji kwenye mwili. Ngozi ya samaki ni laini, hivyo isipofunikwa na magamba magumu kama yale, meno makali ya maadui katika njia wanapopita, ni rahisi kujeruhiwa. Yanakaa kama vile dirii (kinga/shield) kifuani mwa askari.

Lakini si samaki wote walikuwa na haya mapezi na magamba. Wengine hawakuwa nayo, mfano wa hao ni kama kambale, kamongo, papa, pomboo, pweza.

Kwa nini samaki hao wakatazwe kuliwa na ufunuo wake ni upi rohoni?
Kama tunavyofahamu, agano la kale ni kivuli cha agano jipya. Siyo kwamba viumbe hivyo vikiliwa vitamkosesha mtu kwenda mbingu, au vitamnajisi roho, hapana. Kuwa najisi siyo kutokwenda mbinguni, bali kunahitaji nguvu ya ziada ili kumpendeza Mungu, kama vile utakaso, nk.

Vilifanywa vile kwa makusudi ili kutupitishia sisi ujumbe wa rohoni katika agano jipya. Kwamba na sisi kama tutafanana na mojawapo wa viumbe hivyo rohoni, basi tunakuwa najisi mbele za Mungu.

Samaki mwenye magamba ni mwenye ulinzi wa kutosha dhidi ya mashambulizi ya maadui. Na sisi tunapokosa ulinzi wa rohoni, mfano wa yule askari anayezungumziwa katika Waefeso 6:13-16, mwenye dirii ya haki kifuani, ngao ya imani mkononi na chepeo ya wokovu kichwani, tunakuwa ni dhaifu, kiasi cha kutoweza kusimama mbele ya adui yetu shetani.

Hivyo, ni kuhakikisha kuwa umesimama imara katika wokovu wako, lakini pia utambue haki uliyopewa katika msalaba wa Yesu Kristo na imani yako timilifu ndani ya wokovu wako.

Hapo utakuwa umejidhatiti vya kutosha, mfano wa samaki mwenye gamba gumu, au mamba aliyefunikiwa na ngozi yenye gamba.
Ayubu 41:13 anasema: “Ni nani awezaye kumbambua magamba yake? Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?
14 Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake. 15 Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri. 16 Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati. 17 Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa”.

Vile vile, samaki aliyekuwa na mapezi alikuwa ni mwepesi kukatiza katika maji. Ni sawa na mabawa kwa ndege, au miguu kwa binadamu.

Hivyo, na sisi katika ulimwengu huu wa dhambi, ili tusionekane kuwa najisi, tuvae mapezi yetu ambayo maandiko yanasema. Ndio ule utayari wa kuihubiri injili:
Waefeso 6:15 "na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya amani".

Tusienende kama watu wasio na kusudi maalum la kufanya duniani. Tuvae utayari, ndiyo mapezi yetu. Tutembee ulimwenguni kote kiuhubiri/kushuhudia habari njema.

Kwa sababu tukikosa haya, siku ile ya mwisho, tutatengwa, samaki wema na waovu. Kisha wale waovu watatupwa nje. Zingatia Mathayo 13:
47 "Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;
48 hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.
49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki".

Tunaweza kulinganisha na nadharia ya baadhi ya vyakula, ambavyo vinasemwa sana na madaktari hata kwenye vyombo vya habari, kwamba watu wasipendelee sana kula chipsi, au unga wa nafaka ambazo zimekobolewa. Siyo kwamba binadamu akivila hataishi, la hasha. Ila ni kwamba uimara na ufanisi wa vyakula hivyo mwilini ni mdogo, hivyo mwili unakuwa dhaifu katika baadhi ya nyanja.

Kadhalika katika samaki wasiokuwa na mapezi, au wasiokuwa na magamba. Uimara na uthabiti wa ulinzi wa samaki hao unaakisi na ni kivuli cha moja kwa moja, katika uimara wa kiroho katika kupambana na adui shetani, maadui wa kiroho.

Ndiyo maana samaki wa aina hiyo hawaruhusiwi kuliwa, kulingana na imani ya kikristo.

Hivyo, tusiwe samaki najisi, wale wasiokuwa na mapezi, au wasiokuwa na magamba.

Hiyo itatuwezesha kupambana na adui shetani, NA KUSHINDA.
Sijui kwa nini huwa mnahangaika sana na hivyo vitu!

Chakula huliwa ama kutokuliwa sehemu kutokana na mila na tamaduni za watu wa eneo husika.

Kujikunja kuandika chakula cha utamaduni wa watu wa midle east ni kukubali kukaririshwa mambo kama kasuku.

Enhe embu tuelezeee madhara ya kisayansi yatokanayo na kula viumbe ama samaki wasio na magamba.
 
Maandiko yenu ya Imani za dini haya appy Kwa Kila Race ama Taifa , huko china wana kula Kila wakionacho kuwa kinafaa the same to new Papua guenea the same to India the same to Haiti and the likes

Na maisha Yao Yana songa tu , Mambo ya Imani ni mchongo
 
Umeambiwa hayo ni Mambo ya Walawi:
Someni Biblia kwa hekima na sio kukariri mistari:
Ukoo wa Walawi ulikuwa umetengwa kwa ajiri ya vyeo vya Ukuhani yaani viongozi wa Ibada za enzi za Musa:
Hivyo kwa wakati huo Mungu akawachagulia vitu kama Mavazi, Vyakula na mahitaji mengine maalum kwa ajiri Yao tu:
Najisi ni kile kimtokacho mtu:
Ukila chakula ambacho kila ukila unakitapika jua Mwili wako haupendi hicho chakula hivyo ni najisi kwako:
Mamba na Nyoka wakubwa kama Chatu ni chakula kitamu sana na kina virutubisho vingi vya kiafya:
 
Watu wameambiwa wasile kitimoto wao wanamla mpaka zakari😀
Imagine mtu anakula mpaka matusi ya kuku🤪.
Nadhani kuna kipindi hata Sir God mwenyewe anajilaumu kuumba hiki kiumbe kiitwacho binadamu🤣
Acha kumsingizia Mungu.
 
China wanakula nyoka, vyura, konokono na matakataka mengine yenye kinyaa kwa sisi tunaoangaika na dini. Unajua sababu ya wao kula haya matakataka? Sababu ni moja tu. Sio waamini katika imani zetu za uislam na ukristu.
Hizi dini ndio zimejaribu kutuwekea limitation ya aina ya vyakula vya kula.
Katika uumbaji, Mungu alimwambia Adam na majani ya kondeni ale. Sasa hayo majani hayakutajwa majina kama mchicha, spinachi, matembele au labda ilikuwa ni bangi.
Tukachagua michicha na mboga nyingine. Bangi tukaikataa. Mlikatazwa wapi kutumia bangi kama mboga? Maana nayo ni jani la kondeni.
Mbona sisi wanyalu majani ya bangi ni mboga? Tena tunaunga na mbegu za maboga. Ni tamu balaa!!!
 
Samaki wasio na mapezi na magamba hawaruhusiwi kuliwa

Maandiko katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:9-12, yanasema:
9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.

10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu,
11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.
12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.

Mapezi ya samaki ni nini
Hivi ni vile vitu kama mbawa ngumu zenye mfano wa miiba zinazokaa kwa juu, au pembeni, au nyuma mwa mwili wa samaki. Ukitazama samaki kama perege, sato au sangara, utaona mapezi yao.
Faida za mapezi hayo ni kuwa yanasaidia kuogelea, kuelea vema kwenye maji, kukunja kona, kuongeza kasi, kusimama au kugeuka kwa haraka.

Magamba ya samaki ni nini
Halikadhalika, samaki waliokuwa na magamba ndio tu walioruhusiwa kuliwa. Magamba yaliwasaidia kujilinda na maadui au wadudu wavamiaji kwenye mwili. Ngozi ya samaki ni laini, hivyo isipofunikwa na magamba magumu kama yale, meno makali ya maadui katika njia wanapopita, ni rahisi kujeruhiwa. Yanakaa kama vile dirii (kinga/shield) kifuani mwa askari.

Lakini si samaki wote walikuwa na haya mapezi na magamba. Wengine hawakuwa nayo, mfano wa hao ni kama kambale, kamongo, papa, pomboo, pweza.

Kwa nini samaki hao wakatazwe kuliwa na ufunuo wake ni upi rohoni?
Kama tunavyofahamu, agano la kale ni kivuli cha agano jipya. Siyo kwamba viumbe hivyo vikiliwa vitamkosesha mtu kwenda mbingu, au vitamnajisi roho, hapana. Kuwa najisi siyo kutokwenda mbinguni, bali kunahitaji nguvu ya ziada ili kumpendeza Mungu, kama vile utakaso, nk.

Vilifanywa vile kwa makusudi ili kutupitishia sisi ujumbe wa rohoni katika agano jipya. Kwamba na sisi kama tutafanana na mojawapo wa viumbe hivyo rohoni, basi tunakuwa najisi mbele za Mungu.

Samaki mwenye magamba ni mwenye ulinzi wa kutosha dhidi ya mashambulizi ya maadui. Na sisi tunapokosa ulinzi wa rohoni, mfano wa yule askari anayezungumziwa katika Waefeso 6:13-16, mwenye dirii ya haki kifuani, ngao ya imani mkononi na chepeo ya wokovu kichwani, tunakuwa ni dhaifu, kiasi cha kutoweza kusimama mbele ya adui yetu shetani.

Hivyo, ni kuhakikisha kuwa umesimama imara katika wokovu wako, lakini pia utambue haki uliyopewa katika msalaba wa Yesu Kristo na imani yako timilifu ndani ya wokovu wako.

Hapo utakuwa umejidhatiti vya kutosha, mfano wa samaki mwenye gamba gumu, au mamba aliyefunikiwa na ngozi yenye gamba.
Ayubu 41:13 anasema: “Ni nani awezaye kumbambua magamba yake? Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?
14 Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake. 15 Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri. 16 Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati. 17 Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa”.

Vile vile, samaki aliyekuwa na mapezi alikuwa ni mwepesi kukatiza katika maji. Ni sawa na mabawa kwa ndege, au miguu kwa binadamu.

Hivyo, na sisi katika ulimwengu huu wa dhambi, ili tusionekane kuwa najisi, tuvae mapezi yetu ambayo maandiko yanasema. Ndio ule utayari wa kuihubiri injili:
Waefeso 6:15 "na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya amani".

Tusienende kama watu wasio na kusudi maalum la kufanya duniani. Tuvae utayari, ndiyo mapezi yetu. Tutembee ulimwenguni kote kiuhubiri/kushuhudia habari njema.

Kwa sababu tukikosa haya, siku ile ya mwisho, tutatengwa, samaki wema na waovu. Kisha wale waovu watatupwa nje. Zingatia Mathayo 13:
47 "Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;
48 hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.
49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki".

Tunaweza kulinganisha na nadharia ya baadhi ya vyakula, ambavyo vinasemwa sana na madaktari hata kwenye vyombo vya habari, kwamba watu wasipendelee sana kula chipsi, au unga wa nafaka ambazo zimekobolewa. Siyo kwamba binadamu akivila hataishi, la hasha. Ila ni kwamba uimara na ufanisi wa vyakula hivyo mwilini ni mdogo, hivyo mwili unakuwa dhaifu katika baadhi ya nyanja.

Kadhalika katika samaki wasiokuwa na mapezi, au wasiokuwa na magamba. Uimara na uthabiti wa ulinzi wa samaki hao unaakisi na ni kivuli cha moja kwa moja, katika uimara wa kiroho katika kupambana na adui shetani, maadui wa kiroho.

Ndiyo maana samaki wa aina hiyo hawaruhusiwi kuliwa, kulingana na imani ya kikristo.

Hivyo, tusiwe samaki najisi, wale wasiokuwa na mapezi, au wasiokuwa na magamba.

Hiyo itatuwezesha kupambana na adui shetani, NA KUSHINDA.
Wamekatazwa na nani? Toa sababu za kiafya usilete mila za kigeni
 
Agano la kale kwa asilimia kubwa limezungumzia wayahudi(ambao na wenyewe hawaamini ukubwa wa nguvu za yesu)

Kuna maagizo ya chakula katika hatua zifuatazo
1. Maagzo ya chakula enzi za adam na hawa
2. Maagzo ya chakula enzi za nuhu
3. Maagzo ya chakula wakati wa safari ya wana wa israeli(hapa kuna makatazo mengi sana hadi na matambiko yapo)
4. Maagzo ya chakula wakati wa YESU KRISTO
5. maagzo ya chakula baada ya kupaa kwa YESU KRISTO

maagzo ya 1-2 yalikuwa ni maagzo makuu na walipewa kula, kutawala na kumiliki(ikiwemo matumizi), hapa hapakuwepo na miiko

maagzo namba 3, yalikuwa na makatatzo kutokana na wayahudi kutokuwa makini, pamoja na geographia ya mazingra waliokuwepo kipindi hcho (kumb. wakiwa misri hawakukatazwa maana mazingra yaliruhusu ulaji huo)
-hapa wayahudi wa ubungo tunatoana ngeo

maagzo ya 4-5, yanatutaka kula chochotd tena bila kuuliza kimetoka wapi
-katika maagzo haya tunakumbushwa kuwa hatupo chini ya sheria bali tupo kwa neema ya YESU KRISTO
-sis si wayahud bali ni wakristo
 
Mf, china wanakula hadi vyura na nyoka, hawadhuriki maana mazingiri na asili ya miili yao inawaruhusu, huku wayahudi wa vunjo mtatoana ngeo
-mm ni mkurya, nakula nyama kavu ya mnyamapori (kimolo) lakn mdengereko hawezi, wkt huo huo ukienda maeneo fulani ya morogro kuna watu wanakula nyani na wanajilamba.

1. Afrika dini zetu zmekufa, tumejikuta katika utumwa wa kimagharibi na mashariki ya kati
-pamoja na mapokeo hayo bado hatujui tumepokea nini.

2. Ukienda nchi kama thailand, japan, korea kaskazini huu ujinga upo kidogo sana.

LA MSINGI, ISHI MAISHA MEMA NA MUAMINI MUNGU KWA IMANI YAKO NA UZIDI KUTENDA MEMA KWA IMANI KUU ILI MWISHOWE UISHIE PAZURI.

-chakula, maulid, chrismass, jumamosi, jumapili, ijumaa na sikukuu za miandamo ya miezi havitakupeleka katika mwisho mzuri bali matendo mema na imani yako.
 
Waafrika bwanaa ndio maana hatuendelei tumeendekeza sana dini, wakati wenye dini waliotuletea wala hawana muda nazo. Wachina na wa South Asia wanakula kila kitu wakipendacho na ndio wana akili sana kuliko hawa waafrika wafata dini. Dini ndio ilirudisha nyuma mawazo na maendeleo ya waafrika, imewapumbaza mpaka tumekua mazezeta. Kila kitu dini , tumerogwa.
Don't get me wrong; Mungu yupo, lakini hizi dini naaaa!
 
Wachina hawalijui hilo wanakula kila kitu...
Za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom