GE2025 Samandito: Rushwa yaiumiza CUF, wapo waliojitoa baada ya kurubuniwa fedha

GE2025 Samandito: Rushwa yaiumiza CUF, wapo waliojitoa baada ya kurubuniwa fedha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito, amesema kuwa tatizo la rushwa limekikumba chama chake baada ya baadhi ya wagombea na mawakala kujitoa dakika za mwisho, hali inayotishia uhalali wa ushindani wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

1761221254315.png
Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya Oktoba 22 mjini Morogoro, Samandito amesema baadhi ya watu waliojipenyeza kwenye mchakato wa kugombea walifanya hivyo kwa nia ya kupata fedha kutoka kwa wagombea wa CCM, na baada ya kulipwa, wameamua kujiondoa.

“Wapo waliokuja kwa kisingizio cha kutaka mabadiliko, kumbe walikuwa wakisubiri wapewe fedha kidogo na wagombea wa CCM waondoke. Hawa ndio wanaochangia kudhoofisha imani ya wananchi kwenye siasa,” amesema Samandito.

Ameongeza kuwa tabia kama hiyo inawaumiza wananchi wanaotamani mabadiliko ya kweli, kwani inaleta kukata tamaa na kudhoofisha nguvu za upinzani katika chaguzi.

“Wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu utawala wa CCM, lakini mabadiliko hayawezi kuja kwa maneno — lazima wananchi wenyewe waamue kwa vitendo,” amesema.

Akizungumzia changamoto ya kuweka mawakala katika kila kituo, Samandito amesema ni vigumu kwa vyama vya siasa kama CUF kufanya hivyo kutokana na ukosefu wa rasilimali, na hivyo imani yao hubaki kwa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) — ingawa alidai tume hiyo haina uhuru wa kutosha kwa kuwa imeundwa na Rais.

“Imani yetu ingetegemea INEC, lakini kwa sasa nayo ni uteuzi wa Rais, kwa hiyo hatuna namna nyingine,” amesema.

Aidha, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani Oktoba 29 bila kuogopa vitisho, vurugu au propaganda za hofu.

“Wasiogope. Wajitokeze kumpigia kura rais wao ambaye ni mimi, pamoja na wabunge na madiwani wanaoamini wana dhamira ya kweli ya kuwatumikia na kuleta mabadiliko,” amesema.

Kuhusu taasisi za uwajibikaji kama TAKUKURU na INEC, Samandito amesema vyombo hivyo vimepoteza nguvu kwa sababu vinateuliwa na Rais, hivyo haviwezi kuchukua hatua stahiki dhidi ya rushwa ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom