Afisa Habari wa shirikisho la soka nchini Alfred Lucas amethibitisha hilo ambapo ameeleza kuwa nyota huyo atatua nchini kesho na ataungana na wachezaji wengine ambao tayari wameshaanza kuingia kambini kuanzia Oktoba Mosi.
“Kambi imeanza tangu jana, na wachezaji wa kimataifa wameshaanza kuingia, mchana huu tumempokea Simon Msuva kutoka Difaa El Jadidah ya Morocco na tunatarajia Mbwana Samatta ataingia saa 9:45 alfajiri”, amesema Alfred Lucas.
Aidha Alfred Lucas amesema mchezaji Morel Orgenes kutoka FC Famalicao ya Ureno anamalizia taratibu za idara ya Uhamiaji nchini Ureno kisha atasafiri kuja nchini mapema iwezekanavyo.
Taifa Stars itashuka kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es salaam Oktoba 7 kuvaana na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA.
EATV