Samata kutua Dar kujiunga na Taifa stars

Samata kutua Dar kujiunga na Taifa stars

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
SAMATTA 2.jpg
Nyota wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta anayekipiga kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubeligji anatarajiwa kutua nchini alfajiri ya kesho tayari kwa kujiunga na kambi ya Taifa Stars.

Afisa Habari wa shirikisho la soka nchini Alfred Lucas amethibitisha hilo ambapo ameeleza kuwa nyota huyo atatua nchini kesho na ataungana na wachezaji wengine ambao tayari wameshaanza kuingia kambini kuanzia Oktoba Mosi.

“Kambi imeanza tangu jana, na wachezaji wa kimataifa wameshaanza kuingia, mchana huu tumempokea Simon Msuva kutoka Difaa El Jadidah ya Morocco na tunatarajia Mbwana Samatta ataingia saa 9:45 alfajiri”, amesema Alfred Lucas.

Aidha Alfred Lucas amesema mchezaji Morel Orgenes kutoka FC Famalicao ya Ureno anamalizia taratibu za idara ya Uhamiaji nchini Ureno kisha atasafiri kuja nchini mapema iwezekanavyo.

Taifa Stars itashuka kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es salaam Oktoba 7 kuvaana na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA.

EATV
 
Back
Top Bottom