Samatta ahakikishiwa namba kuwaliza Leicester City

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Benchi la ufundi la Aston Villa limemhakikishia nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta nafasi ya kucheza katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Leicester City kutokana na kiwango bora anachoonyesha mazoezini.

Kocha wa timu hiyo, Dean Smith alikaririwa na mtandao wa Sky Sports jana akisema kuwa licha ya Samatta kuonekana anapata wakati mgumu kuhimili mazoezi mazito ambayo amekutana nayo katika timu hiyo, haoni sababu ya kutompa nafasi kwenye mchezo dhidi ya Leicester City akiamini atakuwa chachu kwao kufanya vyema. Amefanya mazoezi na sisi Alhamisi na ameonyesha kiwango kizuri.

Anahitajika kuendana na kasi na anafahamu kwamba kiwango cha mazoezi ni tofauti na ilivyokuwa Genk,” alisema.

“Kwa hiyo mazoezi yetu ni magumu na anatakiwa azoee kwa haraka. Ameshapata utulivu na ni mchezaji mwenye haiba nzuri na itakuwa jambo jema kumjumuisha kwa namna fulani. Ni miongoni mwa walio tayari kujumuishwa Jumanne dhidi ya Leicester City.”


Source:
Mwananchi.
 
Sijaelewa hapo mtu katoka ubeligiji mnasema mazoezi ya uingereza magumu je angetokea tz mojakwamoja si angededi uwanjani
Kumbe wanavosemaga intensity ya ligi ya Uingereza ni balaa huwa ni kweli maana hata hayo mazoezi tu anashindwa
Kwahiyo kiwango cha mazoezi cha Aston Villa kinazidi mile cha wababe Genk
Ni kawaida hy , jamaa anaweza kuwashangaza siku hy akatupia

MTC | 101| [emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…