Samatta ahakikishiwa namba kuwaliza Leicester City

Samatta ahakikishiwa namba kuwaliza Leicester City

Benchi la ufundi la Aston Villa limemhakikishia nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta nafasi ya kucheza katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Leicester City kutokana na kiwango bora anachoonyesha mazoezini.

Kocha wa timu hiyo, Dean Smith alikaririwa na mtandao wa Sky Sports jana akisema kuwa licha ya Samatta kuonekana anapata wakati mgumu kuhimili mazoezi mazito ambayo amekutana nayo katika timu hiyo, haoni sababu ya kutompa nafasi kwenye mchezo dhidi ya Leicester City akiamini atakuwa chachu kwao kufanya vyema.
“Amefanya mazoezi na sisi Alhamisi na ameonyesha kiwango kizuri.

Anahitajika kuendana na kasi na anafahamu kwamba kiwango cha mazoezi ni tofauti na ilivyokuwa Genk,” alisema.

“Kwa hiyo mazoezi yetu ni magumu na anatakiwa azoee kwa haraka. Ameshapata utulivu na ni mchezaji mwenye haiba nzuri na itakuwa jambo jema kumjumuisha kwa namna fulani. Ni miongoni mwa walio tayari kujumuishwa Jumanne dhidi ya Leicester City.”


Source:
Mwananchi.
Mechi dhidi ya leicester ni saa ngapi?
 
Kuna beki kisiki Caglar Soyuncu, sijui kama atafunga huyo mchezaj wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzuri wa mpira ni mchezo wa wazi, sio kama karata!! Kwani hatukawii kusema ana hujumiwa, kwani ndio MOTTO, wetu siku hizi mtu anaposhindwa kitu, utasikia sio bure kuna hujuma!!! Samatta anatakiwa afanye kazi kweli kweli, yasiye yakatokea ya thabiti,
 
Sijaelewa hapo mtu katoka ubeligiji mnasema mazoezi ya uingereza magumu je angetokea tz mojakwamoja si angededi uwanjani
Na siyo katoka Ubeligiji tu bali kwenye timu ambayo ni bingwa mtetezi kwenye ligi hiyo ila unaambiwa mazoezi ni magumu AstonVilla ambayo inachechemea EPL.
 
I wish awa-impress Aston Villa kwenye first appearance ya leo kwa kuisadia timu kupata matokeo hata kwa assist pekee.
 
Once hater always hater. Yaani ukiwa hater unaamini Soyancu ni beki bora kuliko VVD.
 
Back
Top Bottom