Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

Mwanaume unanunuaje gari nyekundu.. angenunua nyeusi au nyeupe kama hiyo.. sio mbaya lakini
weka na wewe picha yako ukiwa na gari kama hiyo Nyeusi au Nyeupe...lazima tuwe tunaongea kwa mifano
 
spacial kwa chick hiyo likiwa kwenye parking sehemu yoyote ndio la kwanza kuonekana...pia special kwa kuikumbuka timu yake iliyomfikisha hapo


'kuikumbuka timu yake iliyomfikisha hapo',ndicho kinachomuuma huyo boya anayetatizwa na rangi nyekundu mkuu
 
Mwanaume unanunuaje gari nyekundu.. angenunua nyeusi au nyeupe kama hiyo.. sio mbaya lakini
Mmmmh, wabongo tuna nongwa bhana......mtu hela yake ameipenda gari nyekundu ww unampangia angenunua nyeusi au nyeupe kwa kujiamini kabisa...............TUPUNGUZE GUBU
 
Ni uamuzi wake, ni pesa zake.
Lakini mimi binafsi sijavutiwa na uamuzi huo, kwa sababu sio vizuri sana kwa kijana mdogo aliyepata mafanikio makubwa ya kipesa kwa muda mfupi kisha kukimbilia kutumia pesa zake kwenye Vitu vya gharama kubwa sana kama kununua gari ya kutembelea ya kifahali. Gari ya milioni 136 la nini kwa kijana ambaye ndio kwanza anamiliki gari katika maisha yake huko Ulaya?

Wenye Hekima watanielewa vizuri.

Mkuu, hayo magari huwa hayanunuliwi kwa fedha taslimu, kunakuwa na utaratibu maalum wa wauzaji wa magari kuwauzia wachezaji magari wanayotaka.

Hivyo anaweza kulipa ndani ya miaka 3 na katikati anaweza kupewa gari ingine na biashara inakwenda.

Hivyo utakuta analipa kama Euro 250 tu kwa mwezi ambazo sasa hivi ni kama vijisenti tu kwa Mbwana.
 
130M unanunua gari wkt ukiipasua robo unapata gari latest nzuri, hivi kajenga kwao? Hapo usikute anaishi ktk studio apartment, akili za vijana wa leo.

Kwaiyo hiyo aliyoinunua ni mbaya ?
Pesa si ni zake na gari kaipenda mwenyewe na kainunua, tatizo lako nini ?
Umeambiwa kwao wanaishi kwenye hema ?

NB:- Haishi kwenye apartment studio, anaishi UWANJANI.

[HASHTAG]#Akili[/HASHTAG] za vijana wa jana/kesho bwana!
 
Kwaiyo hiyo aliyoinunua ni mbaya ?
Pesa si ni zake na gari kaipenda mwenyewe na kainunua, tatizo lako nini ?
Umeambiwa kwao wanaishi kwenye hema ?

NB:- Haishi kwenye apartment studio, anaishi UWANJANI.

[HASHTAG]#Akili[/HASHTAG] za vijana wa jana/kesho bwana!


Kwa hiyo na wewe unajiona mwanaume kamili kujibu hiyo pumba hapo juu? Doh!

Wewe na huyo samatta wote wa..pu..mba..vu tu,
Mtu katoka bongo kapauka kama anapaka mawese usoni, anapata hela and the first thing ni gari ya mil130??? Cha! Hela yake lakini ni mjinga! Kama wewe
 
Kwa hiyo na wewe unajiona mwanaume kamili kujibu hiyo pumba hapo juu? Doh!

Wewe na huyo samatta wote wa..pu..mba..vu tu,
Mtu katoka bongo kapauka kama anapaka mawese usoni, anapata hela and the first thing ni gari ya mil130??? Cha! Hela yake lakini ni mjinga! Kama wewe


Kwanza asante kwa:-
1. Kutilia mashaka UANAUME Wangu. (Japokua nimeshindwa kuelewa unawezaje kujua jinsia za members wa humu ndani)
2. Kutuita wapumbavu na huyo "mp.umbavu mwenzangu" (nadhani ulimlenga nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania).

Pili;-
Unaweza ukawa unamaanisha nini labda unavyosema mtu kapata hela na THE FIRST THING Kununua ni gari ya 130M ? Unataka kutuambia hata saa ya mkononi, kijiko, glasi, sturi, kiwanja, nyumba n.k hana ?

Hata ikiwa hivyo vyote hana, U nani wewe hata umpangie nini aanze kununua nini afuate ?

Unajua hata angenunulia bia hela zake zote yuko sahihi maana hela ni mali yake na anapata kwa njia halali!

Sijui huko mtaani kwenu unaishije na majirani kwa hili gubu, mtu asinunue bodaboda, smartphone, kitenge, suruali mpya, mafuta ya kupakaa etc halafu ukajua utaongea wiki nzima na hizo critics zako.

Nitoe RAI tu kwa MBWANA ALLI SAMATTA POPPAT, kaka saizi nunua BOMBARDIER kabisa umnyooshe huyu.

LoveYou
 
Mwanaume unanunuaje gari nyekundu.. angenunua nyeusi au nyeupe kama hiyo.. sio mbaya lakini
Jana nilitaka kuandika kitu kama hiki nikasema ngoja kwanza lazma atajitokeza wa kuniwakilisha kimawazo! kama ningeandika jana ningekuja kupigwa mitama ya shingo hapa!
 
xSamatta.jpg.pagespeed.ic.rTpXCEDMup.jpg


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji.
Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.

Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo baada ya kunyimwa miezi kadhaa iliyopita.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.

Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa League japo amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha.
Wema sepetu fursa hii hujaiona?
 
Back
Top Bottom