Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

Hongera Samata Naona Ulichoka Kupewa Lift Na Thomas Buffel Na Leon Bailey.
 
Ni uamuzi wake, ni pesa zake.
Lakini mimi binafsi sijavutiwa na uamuzi huo, kwa sababu sio vizuri sana kwa kijana mdogo aliyepata mafanikio makubwa ya kipesa kwa muda mfupi kisha kukimbilia kutumia pesa zake kwenye Vitu vya gharama kubwa sana kama kununua gari ya kutembelea ya kifahali. Gari ya milioni 136 la nini kwa kijana ambaye ndio kwanza anamiliki gari katika maisha yake huko Ulaya?

Wenye Hekima watanielewa vizuri.
Naaam..... Ndio maana tunapinga ununuzi wa Dear Bomba wakati ya msingi tunaombaomba. Labda samatta kashayatimiza.

Kila la heri Samatta. Vuta na wengine upatapo fursa.
 
Unashangaa Samata ona huyu mtu wa kwanza kununua Ferrari Tanzania
1475516805490.jpg
 
130M unanunua gari wkt ukiipasua robo unapata gari latest nzuri, hivi kajenga kwao? Hapo usikute anaishi ktk studio apartment, akili za vijana wa leo.
Sio vijana tu mkuu. Kuna taifa linaongozwa na mtu mzima wa kileo tena mpyampya kaamua kununua ndege wakati anaombaomba madawati na hospitali hazina chanjo.
 
xSamatta.jpg.pagespeed.ic.rTpXCEDMup.jpg


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji.
Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.

Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo baada ya kunyimwa miezi kadhaa iliyopita.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.

Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa League japo amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha.
Kwani kuna tatizo kwa samata kununua gari aipendayo?
 
Kwanza asante kwa:-
1. Kutilia mashaka UANAUME Wangu. (Japokua nimeshindwa kuelewa unawezaje kujua jinsia za members wa humu ndani)
2. Kutuita wapumbavu na huyo "mp.umbavu mwenzangu" (nadhani ulimlenga nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania).

Pili;-
Unaweza ukawa unamaanisha nini labda unavyosema mtu kapata hela na THE FIRST THING Kununua ni gari ya 130M ? Unataka kutuambia hata saa ya mkononi, kijiko, glasi, sturi, kiwanja, nyumba n.k hana ?

Hata ikiwa hivyo vyote hana, U nani wewe hata umpangie nini aanze kununua nini afuate ?

Unajua hata angenunulia bia hela zake zote yuko sahihi maana hela ni mali yake na anapata kwa njia halali!

Sijui huko mtaani kwenu unaishije na majirani kwa hili gubu, mtu asinunue bodaboda, smartphone, kitenge, suruali mpya, mafuta ya kupakaa etc halafu ukajua utaongea wiki nzima na hizo critics zako.

Nitoe RAI tu kwa MBWANA ALLI SAMATTA POPPAT, kaka saizi nunua BOMBARDIER kabisa umnyooshe huyu.

LoveYou
Nimependa hiyo bombadia. Maana mkuu kanunua 2 watu wanamsakaaaamaa.... na yeye kuonyesha yuko sahihi, anaongeza zingine kubwa 2. Hayo ndo mambo ya hela. Tumia utakavyo. Tatizo ni kwa hela za umma
 
Hajapata kamdada kamoja ka bongo movie kakumsaidia kula maisha?
 
Back
Top Bottom