Samatta cheza mpira acha kuchonga

Samatta cheza mpira acha kuchonga

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Samatta ni mchezaji mkubwa aliepitia changamoto nyingi hadi kufika pale alipo. Sidhani kama anapaswa kuhangaika na maoni ya mashabiki wake kwenye mitandao.
Hakuna kocha au mchezaji mkubwa makini duniani ambaye atakisikiliza comments za mashabiki mitandaoni na kufanya maamuzi kuhusu mchezaji. Kumbuka kuwa Mbwana analipwa pesa nyingi za club, hivyo sidhani kuwa benchi la ufundi linaweza kumuadhibu samatta eti kwa sababu tu ya maoni ya mashabiki mitandaoni.

Wako wachezaji wanaokumbana na maneno na vitendo vichafu VYA mashabiki lakini wanabaki kuwa focused. Leo hii hapa Tanzania kila mwanahabari na chombo cha habari anawabeza mashabiki wa Mbwana wanaotoa maoni yao binafsi kuhusu Mbwana. Hivi ni vitu vya kawaida sana hapa Ulaya. Kama samatta ataanza kushughulika na maoni ya mashabiki huru mitandao atakosea sana na kuna siku mashabiki nao watamtupa mkono.

Cheza mpira kocha wako atakuona achana na mashabiki wanasema nn kuhusu we we.

Vyombo vya habari tuache kukuza mambo m adogo sana kama haya yaonekane kama jambo kubwa la kitaifa.
 
Sawa mkuu sisi wanahabari na wananchi wa kawaida tumekielewa hatutacomment tena kweny page yake wala ya timu yake
Shabiki ni shabiki tu tofauti na angesema TFF, Waziri au Mkuu wa nchi iweje kila chombo cha habari inchini kinatangaza malalamiko ya Samatta kuhusu comments za mashabiki? Mbona haya ni ya kawaida kwa wachezaji wote wakubwa duniani? Fungua accountants za wachezaji wakubwa na club kubwa duniani utakutana na comments chanya na hasi za mashabiki dhidi ya watu wao. Yupo mtangazaji mmoja alisema redioni kuwa watanzania ni washamba watamharibia Samatta asipangwe kwenye mechi. Uliona wapi kocha mwenye akili akiacha kumpanga mchezaji anayeweza kumpatia matokeo kwasababu tu ya comments za mashabiki wasiojulikana. Tuache ulimbukeni wa aina hii, badala yake tumwambie kijana wetu aongeze Juhudi ndani na nje ya uwanja kumshawishi kocha na wachezaji wenzake.
 
Namnukuu Edo Kumwembe..

"Mashabiki waache kutukana. Lakini
wanaachaje? Kila mtu kashika simu
yake mahali alipo. Mwingine yupo
kwetu Tunduru, mwingine yupo
Kibondo Kigoma, mwingine yupo
Manzese, mwingine yupo Ngara. Ni
ngumu kuzuia. Ndio maana Edward
Lowassa alituhimiza kwa kusema
‘Elimu Elimu Elimu’".
 
Samata sio kwamba ananyimwa Pasi bado hajazoea mfumo wabongo muwe waelewa ulimbukeni wa mitandao
 
R.I.P meja kunta


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Acha kuwatetea hao wasiojitambua, hata ningekuwa mimi Samatta ningelalamika aiseeee!!!

Comments watu wanaandika mpaka matusi, unaonekana kabisa umetoka jamii ya watu wasiojitambua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Messi alikuwa anabezwa kwao kwa kushindwa kwake kuisaidia timu yake ya taifa la Argentina. Wanamtuhumu kucheza chini ya kiwango kuliko anavyochea akiwa Barca, mbona hatujasikia mapovu ya kujitetea. Shabiki ni mtu wa aina yake aiseii, anachojali yeye ni mabao tyuu sio porojo nyingine. Akaze tu msuli kuwaridhisha maboss wake waliomsajili kwa miaka 4 wampe namba uwanjani.

Shabiki ni mtu anaeweza kukatiza katikati ya uwanja wakati mechi ikiendelea na mbele ya polisi wenye bunduki, mbwa na farasi sembuse kuandika tu kwenye mitandao!! aache ligi na mashabiki wake, akumbuke kuwa wengine ni wale aliowakosea hapa na pale kama binadamu.
 
Back
Top Bottom