Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Nadhani nilikosea kujaji analysis hii, nadhani mleta uzi yupo sahihi.

Nimeangalia juzi akianzia bench ikanipa wasiwasi na asivyo kuwa mtu wa kutafuta mpira, nahisi anaweza sugua banch zaidi
Kukiri kukosea ni uungwana, si watu watz wengi wana hulka hiyo, binafsi napendezwa sana na mtu aliye huru kutoa mawazo yake lakini ambaye yuko tayari kukubali pale uhalisia unapo bainisha tofauti na fikra zake.
 
Ooooh mleta mada ana wivu, mara ooh ni Yanga, mara sijui nini ...

Kuukubali ukweli ni moja ya kukufanya ujitambue kisha kubadilika ili upige hatua moja kwenda mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo tukiambiwa ukweli tunakuwa mbogo..Samatta alikuwa utopolo pale Villa,,na hakuna kocha angeanza msimu mpya kwa kumtegemea yeye,so kuuzwa ilikuwa lazima tu
 
Huyu Samatta soon atapelekwa Uturuki kumalizia mpira wake baada ya timu yake kuwa imeshuka daraja.

Hana mpira wa kucheza EPL yule, ni kweli alibahatisha tu kwani hata spidi ya EPL hawezi.
Duhh watu na maono yenu
 
Huyu Samatta soon atapelekwa Uturuki kumalizia mpira wake baada ya timu yake kuwa imeshuka daraja.

Hana mpira wa kucheza EPL yule, ni kweli alibahatisha tu kwani hata spidi ya EPL hawezi.
Wee jamaa ni nuksii duh
 
Najua nitashambuliwa kwasababu watanzania hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie, inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia Samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakuna kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia [emoji1][emoji1]. Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahisi kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..
We jamaa utakuwa Mganga wa Jadi
 
Huyu Samatta soon atapelekwa Uturuki kumalizia mpira wake baada ya timu yake kuwa imeshuka daraja.

Hana mpira wa kucheza EPL yule, ni kweli alibahatisha tu kwani hata spidi ya EPL hawezi.
Uliona mbali
 
Binafsi kucheza ulaya tu ni hatua kubwa. Habari ya lig gan acheze na ip asicheze ni mipango ya Mungu.
Kumewahi kuwa wachezaji mahiri sana na walioshindwa kuwika EPL
Majina Kama Deco, Shevi, hawakuwah kufany vizuri EPL pamoja na uwezo wao walikotoka.
Mbwana kaonesha njia, kumponda hakutuongezei wala hakutupunguzii. Wengine hata Yanga au Simba tu tumeshindwa kufika.
#Haina Kufeli
 
Back
Top Bottom