Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Tuanzie hapa..
Striker kazi ni nani?
Kazi yake striker ya msingi ni ipi?
Kazi ya ziada ya striker ni ipi? (iwapo team ikiwa imeshinda au kufungwa)

Kuna aina ngapi za ma striker..
Ukiyajua haya basi utajiona mjinga sana.

Kajifunze
 
Mkuu issue ya Samatta binafsi namtakia kila la kheri tu, kuhusu mapungufu anayotajwa nayo naamini kama yapo atayafanyia kazi.

Bongo tumeharibiwa na wahenga, eti aliyeko juu mngoje chini.
kweli mkuu yeye sio MUNGU kuwa hana mapungufu
Sababu huwezi kupata natural striker aliekamilika kila kitu kwa karne hii.

Atakuwa top finisher lakini hana spidi.
Atakuwa top finisher lakini hawezi ku defense.!

Mengine kama pumzi si yanarekebishika?

Sasa eti striker anavizia golini..! Hii ni kauli ya expert wa soka kweli?
 
kweli mkuu yeye sio MUNGU kuwa hana mapungufu
Sababu huwezi kupata natural striker aliekamilika kila kitu kwa karne hii.

Atakuwa top finisher lakini hana spidi.
Atakuwa top finisher lakini hawezi ku defense.!

Mengine kama pumzi si yanarekebishika?

Sasa eti striker anavizia golini..! Hii ni kauli ya expert wa soka kweli?

True, ligi yenyewe ni ngumu. Na tumemwona mechi moja tu.

With time ata-integrate na wenzake, chemistry ikikaa sawa tutamwona Samatta tunayemwitaji.

Moja ya vitu namkubali jamaa ni humbleness, hii inamsaidia kufit na wenzake kwa haraka na kujifunza.

Kuna off watapata ya wiki 2, ni muda kiasi wa yeye kuendelea kupata ABCs za ligi na kuelewana na wenzake.
 
True, ligi yenyewe ni ngumu. Na tumemwona mechi moja tu.

With time ata-integrate na wenzake, chemistry ikikaa sawa tutamwona Samatta tunayemwitaji.

Moja ya vitu namkubali jamaa ni humbleness, hii inamsaidia kufit na wenzake kwa haraka na kujifunza.

Kuna off watapata ya wiki 2, ni muda kiasi wa yeye kuendelea kupata ABCs za ligi na kuelewana na wenzake.
Mleta Mada nadhani umeiskia hii 👆👆
 
Najua nitashambuliwa kwasababu waTz hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakina kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia [emoji1][emoji1]. Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahis kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..
Mmh! Wachawi mmeanza.

Unayajua majukumu ya namba 9? Pamoja na mengine yote, lakini lililo kubwa ni kufunga (au kumalizia kufunga mipira ya mwisho).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili bhana, unaacha kumwambia ajirekebishe wapi ili azidi kuwa vizuri unatuambia eti hato maliza misimu miwili EPL as if wewe ni Mungu unaijua kesho yake,
Na kwenye kandanda hakuna bahati hata siku moja, bahati inachukua asilimia ndogo sana kwenye mafanikio ya mtu, kilicho mfikisha pale ni kipaji na juhudi sio kubahatisha,
Msipende kujifanya mnawajua sana binadamu kumshinda Mungu mwenyewe,
Si ajabu haya anayasemea akiwa kwenye kilinge cha sangoma ili kumlegeza mtoto wa watu. Maana si kwa ramli hii.

Kwa nini aanze na negativity badala ya mazuri yake then amshauri nini cha kufanya!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kujua ukweli au uongo wa hi thread muangalie jamaa akiwa national team

ARUSHA KWETU
 
Uchambuzi uchwala huo.. hivi unamjua giroud wewe?? Giroud ana ufundi gani au anakaba?? Uliza ni msimu wa ngapi yupo EPL..

Kuna aina mbili au tatu za namba 9... kuna ile aina ya Firmino , aina ya Aguero na aina ya Samatta..wanaojua mpira wamenielewa..

BTW kocha kaona aina ya uchezaji wake tangu Genk na bado kamsajiri sasa wewe ni nani toka Tz useme hawezi fit Aston villa??
 
Acha ghiriba kijana,hivi washambiaji wote huwa wanahangaika kwenda kukaba sijui kitengeneza mashambulizi?mfano Van Nestroy alikuwaje??Berbetov he?Van Persie?
 
Mbwana Ally Samatta asili yake kubwa ni fundi wa mpira hasa!!!Tangu yupo Simba alikuwa na uwezo wa kutoka na mpira katikati ya Uwanja akipiga vyenga mpaka kufanikiwa kufunga...

Rejea mchezo wa Simba na Tp Mazembe mchezo pekee uliomfanya Tajiri wa Tp Mazembe Moise Katumbi kujinadi atamchukua Samatta kwa bei yeyote baada ya kuona kijana akivuruga vibaya kiungo pamoja na Beki ya Mazembe yeye pekee yake(One man Army!!)

Samatta Tp Mazembe alikuwa mfalme sio kwa kufunga tu bali kwa uwezo wake wa kuweza kuichambua beki ya timu Pinzani!! Tresor Mputu ufalme wake uliisha baada ya Samatta kufika pale!!

Tatizo watu wameanza kumfuatilia Samatta akiwa Genk ambapo alibadilishiwa majukumu ya kiuchezaji na walimtengeneza kwenye kufunga tu kama mshambuliaji wa kati..

Imani yangu Samatta anacheza kwa maelekezo ya Kocha wake tofauti na hapo usimchukulie poa kwenye kutembea na kijiji...asingefanikiwa kwa ufungaji pekee huyu jamaa ana vitu vingi labda ashindwe kwenda sawa na mfumo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fox in the Box nacho ni kipaji

Unamjua Michael Owen.... ?

Sio kwamba napenda kuangalia watu wa aina hii ya mpira lakini kama utatupia nyavuni na timu kuundwa according to your strength utafanikiwa tu
 
Mtunga uzi

Yaelekea hufatilii soka kabisa,

Unamshangaa samatta?

Mbona Kuna washambuliaji walipita hata changa hawajui, lkn walitoboa vibaya mnoo kwa staili yao ya kuibia, na one touch goal km ulivyosema

Mfano mzuri kwa Africa ni Didier Drogba, huyu jamaa alikua hajui hata kupiga chenga akibaki na beki mmoja tuh, lkn mpira ya vichwa, kuibia na mengine ndo ilimpaisha

Ukijifunza ushabiki, jifunze kupitia history sio kukurupuka tuh

Samatta kwa upande mwengine ni mgeni kweny ligi, pia kwa taifa analotoka ni pekee kufika hapo na hakuna mwengine nyuma yake kwa ck hizi za Karibuni, (Labda mm[emoji12][emoji12]) so wakati huu wa mwanzo atapagawa sanaaa, lkn akizoea utakuwa moto wa kuotea mbali kwani jamaa juhudi na bahati anayo kisoka

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fox in the Box nacho ni kipaji

Unamjua Michael Owen.... ?

Sio kwamba napenda kuangalia watu wa aina hii ya mpira lakini kama utatupia nyavuni na timu kuundwa according to your strength utafanikiwa tu
Tunao Watanzania wa namna hi, katika mitaa yote hapa Tz, inakaduriwa hawapungui 11% ya watz wote Wana tabia hii. Husna, kijicho, uchawi, ushirikina na kutowapendelea wenzao mafanikio. Wewe ni mwanga
[emoji12][emoji12][emoji12]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtunga uzi

Mfano mzuri kwa Africa ni Didier Drogba, huyu jamaa alikua hajui hata kupiga chenga akibaki na beki mmoja tuh, lkn mpira ya vichwa, kuibia na mengine ndo ilimpaisha

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu acha kushusha CV za watu...
Ingawa sikatai kwamba finisher kazi yake ni kutupia nyavuni no matter what, ila Drogba nguvu zilimbeba na he had some talent na umbo lake was a perfect target man ambaye angeweza ku-hold the ball; ingawa alipata mafanikio ukubwani.., aina ya watu unaowasema ni kina Allan Shearer na Michael Owen..

 
Back
Top Bottom