Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kitakachoingia kambini kujiandaa kwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji kutoka klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi, wakiongozwa na kocha Hemed Suleiman. Miongoni mwa wachezaji walioteuliwa ni pamoja na;
Katika safu ya ushambuliaji, wachezaji kama Simon Msuva (Al-Talaba SC, Iraq), Selemani Mwalimu (Wydad Casablanca, Morocco), na Kelvin John (Aalborg BK, Denmark) wanatarajiwa kuongeza nguvu kwenye kikosi.
Pia, Kiungo wa Simba SC, Yusuph Kagoma ameitwa Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco.
Hata hivyo, Taifa Stars itamkosa nahodha wake Mbwana Samatta katika mchezo huo muhimu dhidi ya Morocco kutokana na majeraha. Kukosekana kwake ni pigo kwa timu, lakini benchi la ufundi lina matumaini ya kufanya vizuri licha ya changamoto hiyo.
Kwanini kipa hajaitwa Diara yani hata Aziz ki ameonekana hana nafasi timu ya taifa? Naomba nafasi niwe Rais wa TFF ili niwaokoe ndugu zangu watanzania, laiti kama ningekua Rais wa TFF nisingekubali mchezaji kama Mukwala, Nouma, Aucho na Pacome wasiwepo
Hivi Ali Salim na Abutwalib Msheri Nani amecheza mechi nyingi za mashindano msimu huu?
Kwanini wasiitwe kipa toka timu zingine wanaofanya vizuri tofauti na Yanga na Simba?