Samatta Vs Msuva Timu Ya Taifa!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Baada ya kumfuatilia Sana Samatta akiwa na Timu Ya Taifa nimeamua Kuandika Huu uzii na Kusema kuwa Simon MSUVA ni Bora Zaidiiii Kuliko Samatta Katika Timu ya Taifaa, Bado Samatta hajaonesha kiwango chochote timu Ya Taifa kama Afanyavyo Msuva, Samatta Amekuwa Akicheza kwa Tahadhari mnoooo kuliko mchezaji yoyote na amekuwa anapoteza mipira kirahisi sanaaa kwa kuhofia kuumiaa! nadhani Anajitahadhari kwa sababu Anaogopa Asije akaumia timu ya Taifa Na kushindwa kucheza ulaya! Hii inafanya ashindwe hata kujitumaa kama wachezaji wengine! Angalia Msuva Anavyocheza akiwa na Timu ya Taifa,angalia Striking force ya Msuva Na Wachezaji wengine Ni tofauti kabisa na Timu na Samatta! Yule Samatta Wa Genk sio huyu wa Timu Ya Taifa

Ni wakati sasa Wa Timu ya Taifa Kuacha Kumtegemea Samatta kama mchezaji wao anaeweza kunadiri matokeo muda wowote hapana! Ni wakati sasa Wa Timu Ya Taifa Kukomaa na Local Players Wetu pamoja na Msuvaa, ni wakati sasa wa Makocha kuanza kumfanyia Sub Samatta na Kuacha vijana wengine waoneshe Uwezo Wao!

Samatta anawadanganya hata Makocha na kusabisha makocha waogope hata kumfanyia Sub au kumuacha Kumuita Wakihofia Kusemwa na Majungu ya Watanzania ila Kiuhalisia Samatta Timu Ya Taifa Hana Msaada kama Akiwa Genk! Angalia Msuva Anavyo tafuta magoli na Ku creat chances nyingi sana tofauti sana Na Samatta

Kwangu Mimi Sijaona Kipya cha Samatta Akiwa Na Timu ya Taifa,Kwangu Mimi Msuva Ni Bora Kuliko Samatta katika Ngazi ya Timu ya Taifa,Msuva Ni wakati sasa Wakwenda Ulaya

Samatta Wa Genk sio Wa Taifa Stars
 
Uko sahihi. Anakenua kenua tu uwanjani. Siyo yule Samatta tunayemfahamu. All im all, Taifa Stars wamestahili kuadhibiwa kizembe kabisa kwa mwalimu kukosa plan b kama mwalimu mwenzake wa Libya.

Waliridhika kwa kuongoza kwa kagoli kamoja, sasa mambo yamewageukia kama yale yaliyowatokea Equatoria Guinea uwanja wa Taifa.
 
sasa aumie timu ya taifa.. atibiwe kwa NHIF haifiki hata agakhan nairobi
 
Mtu belgium yupo kwenye wafungaji bora timu ya taifa anapiga penati tu
Najua mpira una matokeo 3 hapa hatuongelei matokeo tunaongelea kiwango cha samata timu ya taifa
 
Nimekupata mkuu, kuna ukweli Fulani hapa. Personal nimeumia sana na haya matokep ya Leo.. Actually match mechi ilikuwa tunatusua ile..?
 
Mtu belgium yupo kwenye wafungaji bora timu ya taifa anapiga penati tu
we umesimamia kucha hapa ila siku akifanya vizuri utakuja tena kusifia ndo wabongo mlivyo baya la siku1 unasahau mazuri yote bila kujua kila kitu kina wakati wake
 
Huyo boya hana lolote bhana kwa taifa stars
we umesimamia kucha hapa ila siku akifanya vizuri utakuja tena kusifia ndo wabongo mlivyo baya la siku1 unasahau mazuri yote bila kujua kila kitu kina wakati wake
 
Msuva akienda ulaya naye atakuwa hana mchango timu ya taifa kwa hiyo usimshauri aende ulaya mkuu
 
Alikua bora ktk ufungaji ligi ya kongo drc na mazembe,mpaka kugombea mchezaji bora afrika
Amekua mfungaji bora ktk ligi ya ubelgiji mpaka kufikia kuibeba genk kuteaa ubingwa na kuipeleka Uefa
Amefanikiwa kuwa mtz wa kwanza kucheza Uefa na kuzifumania nyavu za mabingwa wa ulaya home and away-anfield-licha ya kukabwa na mabeki wazoefu akiwemo beki bora ulaya..!....vipi leo awe mbovu?
Tatizo halipo kwa samata jiulize samata anacheza na akina nani uwanjani?
Kiukweli wachezaji wetu ukiondoa labda msuva wana viwango duni mno!wengi uzoefu hawana,ball control,speed &accuracy vipo chini mno...hilo ndio tatizo..Sama goal wanamuimba pale genk acha kabisa!
 
Hapa kunawatu wanashindwa kuelewa hatumlaumu samatta kwakua tumefungwa, Hata tungesginda Ila bado tusingeridhishwa na kiwango anachoonesha samatta katika timu ya taifa. Wote tunajua kua huu sio uchezaji wa samatta Bali anajilinda asipate majeruhi. Hali hii inapelekea atoe msaada kidogo Sana katika timu.

Tutaendelea kumlaumu samatta Kama akiendelea kucheza namna hii Kama anaogopa majeruhi Basi ahakikishe hapotezi mipira ambayo wachezaji wenzake wanaangaika kuicover yeye anapoteza kirahisi anawashusha morali wachezaji wenzake na pia anapelekea kutokea makosa mengi mpaka kupoteza mchezo.

Ni muda sahihi Sasa kutomtegemea samatta katika timu ya taifa Bali tuwape nafasi wachezaji wengine waoneshe ushindani katika namba ya samatta anatuangusha Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…