Sambusa za Mlenda

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
8,082
Reaction score
17,838
Mzuqa,

Nilipokua field Nyarugusu nikimalizia thesis yangu katika Masters in Geology mida ya jioni nilikuwa najichanganya kitaa kula sambusa za mlenda.

Hizi Sambusa zinahitaji utaalam wa hali ya juu kuzila. Kwani unapomega inabidi uangalie juu kama kuku anavyokunywa maji na kuuvuta mkono ulioshikilia kipande kingine kikubwa cha sambusa juu hili uzi wa mlenda nao uvutike. Baada ya hapo unatoa mkasi mfukoni nakuukata ule uzi.
 
Tumejua una Masters ya Geology mkuu. Hongera. Haukuwa na haja ya kutueleza ulienda Nyarugusu kufanya nini.
 
Naona unaongelea ugali kwa mlenda, chakula chetu wasukuma ha ha ha umesahau chips za michembe mh
 
Ntajaribu kuzipika, waweza elezea zinakuwa zimekatwa katwa au nzima nzima?
Michembe ni viazi vitamu vilivyo katwakatwa halafu vikaanikwa juani na kukauka .kuvipika unavikaanga na mafuta baadae unaweka maji na kuvifunika viivye.
 
Michembe ni viazi vitamu vilivyo katwakatwa halafu vikaanikwa juani na kukauka .kuvipika unavikaanga na mafuta baadae unaweka maji na kuvifunika viivye.

Naaha sikumaanisha michembe, nilimaanisha sambusa za mlenda alizoongelea mtoa mada.

Hayo matobolwa nayajua sana ndo yamenikuza hayo na mahama kule kwetu Tabora.
 
Naaha sikumaanisha michembe, nilimaanisha sambusa za mlenda alizoongelea mtoa mada.

Hayo matobolwa nayajua sana ndo yamenikuza hayo na mahama kule kwetu Tabora.
Kwaku fukilia mtoa mada alimaanisha ugali na mlenda kwa sababu ukila ugali na mlenda lazima tonge liende juu kidogo halafu mlendemko unaukata kwa mkono, karibu tule mlenda na ugali wa udaga.
 
Kwaku fukilia mtoa mada alimaanisha ugali na mlenda kwa sababu ukila ugali na mlenda lazima tonge liende juu kidogo halafu mlendemko unaukata kwa mkono, karibu tule mlenda na ugali wa udaga.

Asantee, uko wapi nije kuonja maana Nna njaa kweli.
 
Nzuri zaidi kama utatumia mlenda wima au mlenda bata na ntwiri.

Mmhhh huo siujui, naujua mlenda wa kinyanyamwezi na mlenda wa kawaida wa kuchanganya majani ya maboga na bamia.

Ila mapishi ni ubunifu,naweza kupika sambusa za matembele....

Serena Hotel wanapika cabbage rolls Yaani cabbage imepikwa kisha inazungushwa kwenye ngano kama chapati za kufungia maandazi kisha inakaangwa. Vitamu hivyoo, huwa napenda kuagiza hivo, kababu na chicken drums wananiletea na sosi ya kuchovyea nashushia na glass ya wine siku imeisha.
 
Mlenda bata au mlenda wima ndio ndio mlenda halisi wa kinyamwezi ambao badala ya kutumia bamia kwenye msusa unatumia mlenda bata au wima, Pia hutumika kwenye nswaru.
 
Mlenda bata au mlenda wima ndio ndio mlenda halisi wa kinyamwezi ambao badala ya kutumia bamia kwenye msusa unatumia mlenda bata au wima, Pia hutumika kwenye nswaru.

Asante sana, mwezi wa 12 nna safari ya Bariadi, ila ntapitia nyumbani Tabora nichukue huo mlenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…