Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, leo Oktoba 22,2024, amesema basi hilo limepata ajali majira ya alfajiri, wakati likitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Machame, Wilaya ya Hai kwenye shughuli za maziko ya mwanakwaya mwenzao.
Kwa mujibu wa DC Mgeni, basi hilo liliacha njia na kugonga kalavati dogo la Kirinjiko.
"Ni kweli watu watano wamepoteza maisha, wakiwamo wanawake watatu na wanaume wawili. Wote hawa ni wana kwaya KKKT waliokuwa wakitokea Dar es Salaam kuelekea Machame,"amesema.
Basi hilo lilikuwa likiongozana na mabasi mengine manne, na dereva wake alisinzia na ghafla alishtuka ameligonga kalavati hilo.