Inatokea mara chache sana katika maisha ya mwanadamu, Kiungo mkabaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ujerumani, Sami Khedira leo ametupia magoli matatu ( hat trick ) wakati Juventus ikiua 6-2.
Ni hat trick ya kwanza kwa Sami Khedira katika career yake ya kusakata kabumbu.
Toka nifatilie mpira wa ushindani sijawahi kusikia Kiungo mkabaji akitupia goli tatu katika mechi moja. Sio mbaya kama wapenzi wa mpira tukampongeza kwa jambo ambalo amelifanya.
Habari za Khedira kupiga Hat trick hazijapewa uzito kwa kuwa yeye sio Messi wala sio Ronaldo ndio maana wazandiki wa soka wameuchuna tu.
Hongera sana Sami Khedira mmoja kati ya viungo bora wa kukaba kwa miaka 7 iliyopita.