Sami Khedira apiga Hat trick Juve ikiua 6-2

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Inatokea mara chache sana katika maisha ya mwanadamu, Kiungo mkabaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ujerumani, Sami Khedira leo ametupia magoli matatu ( hat trick ) wakati Juventus ikiua 6-2.

Ni hat trick ya kwanza kwa Sami Khedira katika career yake ya kusakata kabumbu.

Toka nifatilie mpira wa ushindani sijawahi kusikia Kiungo mkabaji akitupia goli tatu katika mechi moja. Sio mbaya kama wapenzi wa mpira tukampongeza kwa jambo ambalo amelifanya.

Habari za Khedira kupiga Hat trick hazijapewa uzito kwa kuwa yeye sio Messi wala sio Ronaldo ndio maana wazandiki wa soka wameuchuna tu.

Hongera sana Sami Khedira mmoja kati ya viungo bora wa kukaba kwa miaka 7 iliyopita.
 
Tunampa pongezi kama ilivyo familia ya wanasoka. Ila hilo neno wazandiki ondoa kabisa
 
Back
Top Bottom