Samia AFCON City kuoamba Jiji la Arusha

Samia AFCON City kuoamba Jiji la Arusha

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Arusha

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi ametembelea eneo utakapojengwa Mji wa “Samia AFCON City” kwenye eneo linalozunguka Uwanja Mpya wa Michezo unaojengwa eneo la Mirongoine jijini Arusha.

Waziri Ndejembi amefanya ziara hiyo Oktoba 03, 2024 kukagua eneo ambalo mji huo umepangwa kujengwa na kusisitiza kusimamia matumizi ya fedha za umma kwa kuangalia thamani ya fedha za serikali.

Katika kutekeleza mradi huo, Waziri Ndejembi amesema Serikali inalipa kiasi cha Sh. Milioni 35 kwa ekari moja na amesisitiza kujadiliana na wadau wa eneo hilo na kusimamia matumizi sahihi ya fedha ili yaendane na thamani ya fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Mimi wakati nakuja, kiukweli nilijua kuna nyumba tayari, tunaenda kuziondoa. Lakini nafika site nakuta vitu vipo tofauti na ndipo nawekea mkazo hapo kusimamia fedha za Serikali kwa kuangalia value for money” amesema Waziri Ndejembi.

Naye Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Arusha Bw. Geophrey Mwasonjo amesema wanasimamia utekelezaji wa mradi huo ili kuendana na kasi ya ukuaji wa jiji la Arusha ikizingatiwa mkoa huo umepata heshima ya inayoandaa mashindano ya Afcon 2027.

Soma Pia: Mhandisi Sanga akagua eneo la Samia Arusha AFCON City

Kwa upande wake mmoja wa wamiliki wa maeneo utakapojengwa mji wa Samia AFCON City, Bw. Paul Lyimo amesema yupo tayari kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga mji huo kwa kutoa ekari 84 ambazo atalipwa fidia na Serikali.

I think ifike hatua tumuache samia apumzike,,mnavyomtaja kila sehemu imefikia hatua sasa watu wanakerwa nae zaidi kuliko kumkubali Kama inavyodhaniwa
 
I think ifike hatua tumuache samia apumzike,,mnavyomtaja kila sehemu imefikia hatua sasa watu wanakerwa nae zaidi kuliko kumkubali Kama inavyodhaniwa
Inakuuma nini?
 
Wakati Jengo la LAPF tower pale Dodoma kwa sasa hv PSSF tower lipo kwenye makablasha kabla ofisi za LAPF hazijaama kutoka mtaa wa Mtendeni walitaka jengo likikamilika liitwe Jakaya Mrisho Pension Tower. Nikawaambia wanachama wanaochangia kwenye mfuko wenu watajuaje ilo jengo limejengwa kwa pesa zao? Naje si ni bora jengo likaitwa jina la mfuko ili kuwavutia wanaajiriwa wapya kuvutiwa na mfuko hyo kuchagua kujiunga kuwa wanachama? Nikawa nimeeleweka sasa hv ukiliona lile jengo pale Dodoma unasema yes pesa za michango ya wanachama ilitumika vzr.
 
Back
Top Bottom