Samia alitarajia Bashe amnange Bashiru pale Kondoa

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Hivi punde pale Kondoa Rais Samia akiwa njiani kuelekea Babati alimuita Waziri wa Kilimo ndugu Bashe na kwa msisitizo akamtaka aongelee kwa kina mambo matatu yahusuyo Sekta ya Kilimo ambayo ni Mbolea, Mbegu na Chakula.

Ajabu, kwa utulivu na umakini mkubwa ndugu Bashe amefanikiwa kuukwepa mtego aliotegewa wa ama kumzodoa Bashiru aliye-trend na issue ya kuwataka Wakulima waache u-zwazwa lau kumkosoa kwa kauli ile aliyoitoa kwenye Jukwaa la Wakulima siku chache zilizopita.

Heko Bashe.

NB: Bashiru siyo Ndugai!
 
Mbona mnaishi kwa mashaka sana kama digidigi porini[emoji16]?
Hivi punde pale Kondoa Rais Samia akiwa njiani kuelekea Babati alimuita Waziri wa Kilimo ndugu Bashe na kwa msisitizo akamtaka aongelee kwa kina mambo matatu yahusuyo Sekta ya Kilimo ambayo ni Mbolea, Mbegu na Chakula.

Ajabu, kwa utulivu na umakini mkubwa ndugu Bashe amefanikiwa kuukwepa mtego aliotegewa wa ama kumzodoa Bashiru aliye-trend na issue ya kuwataka Wakulima waache u-zwazwa lau kumkosoa kwa kauli ile aliyoitoa kwenye Jukwaa la Wakulima siku chache zilizopita.

Heko Bashe.

NB: Bashiru siyo Ndugai!
 
Katibu mkuu wa Sasa leo atatoa ufafanuzi kuhusu maneno ya Bashiru. Tuwe na subra.
 
Hivi punde pale Kondoa Rais Samia akiwa njiani kuelekea Babati alimuita Waziri wa Kilimo ndugu Bashe na kwa msisitizo akamtaka aongelee kwa kina mambo matatu yahusuyo Sekta ya Kilimo ambayo ni Mbolea, Mbegu na Chakula.

Ajabu, kwa utulivu na umakini mkubwa ndugu Bashe amefanikiwa kuukwepa mtego aliotegewa wa ama kumzodoa Bashiru aliye-trend na issue ya kuwataka Wakulima waache u-zwazwa lau kumkosoa kwa kauli ile aliyoitoa kwenye Jukwaa la Wakulima siku chache zilizopita.

Heko Bashe.

NB: Bashiru siyo Ndugai!
Bashe wa leo siyo yule wa bunge la bajeti. Sasa ameshagundua kuwa hana jipya na kuwa hata yeye anaweza kuwa nje ya jukwaa
 
Bashiru hapindishi?

Bashiru wa tume ya katiba mpya ya Warioba ni Sawa na Bashiru wa Magufuli?
Ni Bashiru wawili tofauti kabisa. Hata yule Bashiru wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na yule wa wakati ule kidole chake kinachovya kwenye buyu la asali pale Lumumba na baadaye Magogoni ni viumbe wawili tofauti kabisa.

Katika dunia hii tunayoishi sisi wana wa Adamu na iliyojaa songombingo za kila aina nimejifunza jambo moja kubwa katika maisha yangu. "Kamwe usimwamini binadamu yeyote kwa 100%." Binadamu anaweza kubadilika wakati na mahali popote na akafanya jambo hadi watu mkabaki midomo wazi kwa mshituko na mshangao. Na hasa ikiwa jambo hilo litafanywa na mtu aliyekuwa anapewa heshima kubwa na wale wanaomzunguka
 
Back
Top Bottom