Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Bendera yetu halisi.
Ndugu zangu.
Maamuzi ya Rais Samia kufuta sherehe za uhuru wa Tanzania ni sahihi kwa wakati huu tunapoelekea kupata katiba mpya na bora.
Tanzania haikupata uhuru wake Desemba 9, 1961. Bali nchi ya Tanganyika ndiyo inayosherehekea Uhuru wake siku hiyo. Nyerere na wenzake hawakupigania uhuru wa 9 Desemba kwa Tanzania bali kwa Tanganyika na Watanganyika.
Tumpongeze bi Samia kwa kuamua kuuishi ukweli. Ameona ni upuuzi kusheherekea uhuru wa Tanganyika chini ya kivuli cha Tanzania. Tanzania ni zao la muungano ambapo Zanzibar baada ya Mapinduzi ya 12 January 1964 ikaungana na Tanganyika ili kuzaa Tanzania mnamo tarehe 26 April 1964 kiasi cha miezi mitatu mbele baada ya Mapinduzi.
RAI
Sisi Watanganyika, tusheherekee siku ya Uhuru wetu bila kificho. Tuvae Tshirts zenye bendera yetu na tarehe ya uhuru, tubebe skafu zenye kuipamba Tanganyika na siku yake ya uhuru. Tusheherekee kutoka mioyoni mwetu huku tukiendesha mijadala ya wazi na mitandaoni kuhusu uhuru na manufaa ya muungano.
Siku ya Tanzania ni 26 April na siyo 9 Desemba.
Happy Independency Day for Tanganyika 1961