kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Wawekezaji lengo lao ni kupata wala sio kuja kutuletea maendeleo. Ni juu ya nchi yenyewe kuweka sheria na taratibu kuhakikisha uwekezaji wa wageni unanufaisha umma wa wananchi wala sio wawekezaji peke yao au wawekezaji na tabaka fulani tu nchini.
Vigogo wanaotaka kufaidika na uwekezaji wa kigeni ni rahisi kuwakubalia wawekezaji wenye nia ya kuikamua nchi tu bila kuacha maendeleo yoyote kwa wenyeji.
Kazi kubwa imefanyika awamu ya tano kuhakikisha uwekezaji wa kigeni una faida kwa mwekezaji na raia wenyeji. Hili la kutaka wawekezaji kuweza kupeleka mashauri nje ya nchi lazima lisikubaliwe.
Kama mwekezaji ana nia njema kuona wenyeji wanafaidika na uwekezaji kwa nini asiweze kuamini mfumo wa sheria wa nchi yetu? Kwani mfumo wa sheria wa tanzania lengo lake ni kutoa haki kwa wenyeji tu au kwa wote wanaoishi na kufanya shughuli zao tanzania?
Uzoefu ulishatuonyesha jinsi wageni wanavyoweza kuidhulumu nchi yetu kwa kutumia mifumo ya kishetia ya nje ya nchi yetu. Mifano ya karibu ni kesi za richmond na iptl. Kesi zinazungushwa na kuchukua miaka mingi bila kuisha huku nchi ikipoteza fedha nyingi na kutiwa hasara kubwa.
Kesi inazungushwa hadi inapotea mtu hajui mwanzo wala mwisho.
Watanzania tusirudishwe nyuma. Mwenye kutaka kuwekeza aje sio kila mwekezaji aje na masharti ya kutaka kubadili sheria zetu.