GE2025 Samia: Hakuna Chama kitakachoweza kwa sasa hivi kulinda na kuinua Utu wa Mtanzania kama siyo CCM

GE2025 Samia: Hakuna Chama kitakachoweza kwa sasa hivi kulinda na kuinua Utu wa Mtanzania kama siyo CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema hakuna chama chochote cha siasa nchini kinachoweza kulinda na kuinua utu wa Mtanzania kama CCM.

Akihutubia wananchi wa Mchinga mkoani Lindi katika mkutano wa kampeni leo, Septemba 25, 2025, Dkt. Samia amesisitiza kuwa kaulimbiu ya chama chake “Kazi na Utu Tunasonga Mbele” inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msingi na fursa za kiuchumi.

“Inawezekana hapa na pale katika safari yetu ya miaka minne mitano tukawa tumekosea, lakini ninataka niwaambie hakuna chama kitakachoweza kwa sasa hivi kulinda na kuinua utu wa Mtanzania kama siyo Chama Cha Mapinduzi. Ndiyo maana tumekuja na hii kaulimbiu ya Kazi na Utu Tunasonga Mbele,” amesema Dkt. Samia.

Amebainisha kuwa dhamira ya CCM ni kuwapa wananchi huduma bora za kijamii na kuongeza kipato kupitia shughuli zao za kiuchumi.

Akijibu hoja za vyama vya upinzani, Dkt. Samia amesema sera nyingi zinazotolewa na wapinzani tayari zinatekelezwa na CCM.

“Wengine wanapitia tu Ilani yetu wanadokoadokoa wanasema, ‘tutatoa elimu bure’, kwani CCM hatutoi? Tunatoa kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita. Mwingine anakwambieni nitaleta maji, alikuwa wapi asiyalete siku zote? CCM si tumeshaleta maji, kwahiyo mengine yote ni ya kuigiza tu,” amesema.

CCM hii ya wanamtandao haina tofauti na bokoharam, imeteka na kuua watu wengi sana kuliko hata makaburu walivyofanya Afrika Kusini.
 
Huyu mama bwana kumsemanga vibaya sometimes ni kumvunjia adabu, basi tu amekataa kustaafu...
 
CCM hii ya wanamtandao haina tofauti na bokoharam, imeteka na kuua watu wengi sana kuliko hata makaburu walivyofanya Afrika Kusini.
Huwa naamini jamii forum ni sehemu ya takwimu sahihi na hapa si facebook!
MKUU;
mkuu tusaidie kujua makaburu wa afrika kusini waliua watu wangapi (kwa idadi) na ccm imeua watu wangapi(kwa idadi) na ili hoja yako iwe na uzito tusaidie na hao wana ccm waliokuwa wanaua ili tukichukie kabisa hk chama.
 
Kama hadi sasa hujui hilo basi wewe ni mmoja wa hao watekaji.
 
Amebainisha kuwa dhamira ya CCM ni kuwapa wananchi huduma bora za kijamii na kuongeza kipato kupitia shughuli zao za kiuchumi.
Maneno matamu sana haya. Na nayaunga Mkono. Hata hivyo, ningependa kujua utaratibu upi utatumika kuhakikisha haya maneno matamu yanatekelezeka?

Natanguliza Shukrani kwa majibu ya kina.
 
Utu ni nini ?

Labda tuanzia hapo kwanza; Huenda tuna definition tofauti, huwezi ukasema unalinda UTU wakati watu wanakosa basic needs let alot some other needs....
 
Utu ni nini ?

Labda tuanzia hapo kwanza; Huenda tuna definition tofauti, huwezi ukasema unalinda UTU wakati watu wanakosa basic needs let alot some other needs....
Utu ni kukosa maji ya uhakika
Huduma za afya za uhakika, ufukara uliopitiliza, kuuliwa ukimhoji kiongozi

Huku tulifanya mapambio
 
Huwa naamini jamii forum ni sehemu ya takwimu sahihi na hapa si facebook!
MKUU;
mkuu tusaidie kujua makaburu wa afrika kusini waliua watu wangapi (kwa idadi) na ccm imeua watu wangapi(kwa idadi) na ili hoja yako iwe na uzito tusaidie na hao wana ccm waliokuwa wanaua ili tukichukie kabisa hk chama.

..Wakoloni wa Kiingereza walikuwa na utu kuliko serikali za CCM.

..Hakuna mwana Tanu aliyeuwawa kwasababu ya kudai uhuru wa Tanganyika.

..Mwalimu Nyerere alishtakiwa kwa kesi moja ya uchochezi, viongozi wa upinzani wameandamwa na makesi kibao zikiwepo za ugaidi, na uhaini.

..Hakuna mgombea wa Tanu aliyeenguliwa katika chaguzi zilizosimamiwa na Wakoloni wa Kiingereza. Ccm imeengua maelfu ya wagombea wa upinzani ktk chaguzi zote za vyama vingi.
 
Sasaiv nan anadai nini?
Kama ni katiba na sheria za uchaguzi, hao wamekuwa wabunge na madiwan kupitia sheria hz hz!

SEMA UPINZANI UCHWARA UMEKOSA MWANAMKAKATI WA KISIASA, kila mtu anajifanya mwanaujuaji.

hata hvo mbnu mnazozitumia kuuhadaa umma ni null and failed hypothesis.
 
..wapinzani wengi wamekuwa wakitangazwa baada ya wananchi kutishia amani, na kufanya vurugu, ili mshindi halali atangazwe.

..wafuasi kadhaa wa vyama vya upinzani, wameumizwa, au kuuwawa, ktk vurugu za kushinikiza wapinzani walioshinda watangazwe.

..kwa hiyo, wanaodai Reforms wanataka kuwepo na mazingira bora, salama, na ya haki sawa, kwa wadau wote wa uchaguzi.

..hoja ya Reforms haipingwi kwa kuwaita majina mabaya wote wanaoiunga mkono. Yaani kinachopaswa kupingwa ni hoja, na sio watoa hoja.

..Swali langu kwako ni hili: Reforms zinazopendekezwa zina ubaya gani kiasi kwamba ni vigumu kuzitekeleza?
 
JokaKuu
hakuna anayekataa mabadiliko, wote tunahitaji mabadiliko tena mabadiliko bora yatakayotumika miaka mingi ijayo...
-kituko hapa ni pale ambapo chadema na upinzani wanaibeba hi ajenda na kuigeuza kuwa mtaji wa kisiasa..
-ni wakati gani unahitaji hayo mabadiliko na ni nn kilichopo mbele?
nakumbuka miaka ya 2013 mchakato huu wa katiba ulifanyika..ni nani aliusitisha? nani aliuzilia?
au tufanye forecast kwmb upinzani ulipoona ajenda hyo inapata majibu walijiona wanaenda kuisha au kukosa ajenda?
unajua kuandaa katiba si kuandika gazeti la mwanahalisi, ni ishu ya mchakato!

tatzo upinzani mmekosa ajenda, mnataka mbembelezwe kama last born..taifa hatuendi hvo!
mtapata uungwaji mkono kama mtaacha kuwaaminisha watz ujinga wa kuwa katb n swala la watz wachache(upnzan)
 
0CE2A59E-F767-4EF5-ABC4-7D573F1CC5B7.jpeg
 
Back
Top Bottom