Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ijayo itaendeleza jitihada za kuboresha huduma za afya mkoani Kilimanjaro, ikiwemo kuimarisha hospitali, kuongeza watumishi na kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana kwa wakati.
Samia amebainisha hayo leo Jumatano, Oktoba 1, 2025 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliofurika kwenye Viwanja vya Mashujaa Mjini Moshi ambapo amesema jitihada zilizochukuliwa katika awamu ya sita zimepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na kupanua huduma za matibabu ambazo awali hazikupatikana katika mkoa huo.
“Kwa kiasi kikubwa tumepunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na hizi jitihada zitaendelea ili twende vizuri. Zaidi, Hospitali yetu ya rufaa ina huduma za wagonjwa mahututi, inahuduma za watoto njiti, ina huduma za kusafisha figo, ambazo awali hazikuwepo ndani ya mkoa,” amesema Samia