Samia hana hela hizo acheni kutufanya wajinga!

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Mara ooh Samia katoa bilioni kadhaa kwa ajili ya jambo fulani ama ooh Samia kakubali mkoa fulani upewe pesa zile-mimi Jitombashisho nasema tuondoleeni huo upuuzi wenu Samia hana hizo pesa.

Pesa ya Watanzania ya kodi ajabu mnammlikisha mtu kana kwamba zake huo ni uzwazwa na upunguani tena mkome mara moja!

Alaah!
 
Kama ulimsikiliza vizuri Waziri wa Fedha Mama ni mmoja wa mabilionia wakubwa Tanzania.
 
Uzuri huu ujinga alianzishaga Magu na wapambe wake.Acha waenzi legacy ya Shujaa.
 
Hata kama nilivutiwa na JPM lakini huo upuuzi niliupinga waziwazi na hata sasa naupinga kwa nguvu zote.

Eti Samia huyu huyu aliyekuwa analalamikia posho za wabunge ni ndogo leo ajabu kawa bilionea 😂?!
 
Mara ooh Samia katoa bilioni kadhaa kwa ajili ya jambo fulani ama ooh Samia kakubali mkoa fulani upewe pesa zile-mimi Jitombashisho nasema tuondoleeni huo upuuzi wenu Samia hana hizo pesa.

Pesa ya Watanzania ya kodi ajabu mnammlikisha mtu kana kwamba zake huo ni uzwazwa na upunguani tena mkome mara moja!

Alaah!
Mkuuu hii id yako ina maana gani??
 
Hata kama nilivutiwa na JPM lakini huo upuuzi niliupinga waziwazi na hata sasa naupinga kwa nguvu zote.

Eti Samia huyu huyu aliyekuwa analalamikia posho za wabunge ni ndogo leo ajabu kawa bilionea 😂?!
Ndio wanaendeleza legacy ya Shujaa wa Africa hivyo.
 
Rais ndiyo mbeba maono Mkuu wa nchi. Ndiyo maana great leaders wanakumbukwa kwa maono yao Makuu. Rais kutoa fedha kufanya Mapinduzi makubwa ya kisekta ni maono na maelekezo yake ktk allocation ya financial resources siyo kwamba anatoa mfukoni.

Ila bila maono yake watu wangechezea fedha ndombolo ya solo na mchapalo ktk semina. Simple iko hivyo😀😀😀.
 
Back
Top Bottom