PostGE2025 Samia: Hatua za kuunda Tume ya Maridhiano zimeanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mbowe alikuwa anafanya ujasiriasiasa,ndio maana raia wengi wamemshtukia na yeye ameona ajiongeze kwa kukaa kimya ambayo nayo ni busara hasa ukiona janjajanja yako imeshtukiwa!.
Nia ya mtu hajifichi Mkuu!
Sawa.

Amandla...
 
Better strategist to what end? What results exactly? Umeona mara tu baada ya kupokwa keki, genge lake lote la viongozi na wake zao viti maalum lilikimbilia wapi
Keki ipi? Hilo unaloita genge lake walijitoa kwenye chama wakawaachia mkiendeshe mnavyotaka. Walifanya ambacho nafsi zao ziliwatuma kufanya. Sasa kazi kwenu maana hamna wa kumsingizia.
Wanasiasa aina ya Lipumba, Mbowe, Zitto ndio ndoto za CCM, wapo wapo tu kuonyesha nchi ina "demokrasia" huku wakiendelea kuchezea akili zetu.
Mpango wa CCM ni wa kutawala nchi kwa namna yeyote. Hilo ndio hamuelewi. Kwa kukurupuka kwenu kumewapa miaka mitano mingine wakati wakiwakaba pumzi. Tuna miezi michache tu baada ya wao kurudi madarakani na pumzi imekata. Wanajua hamna kitu mataifa ya nje watakacho wafanyia zaidi ya kuwanyooshea vidole.

Mbowe aliwaambia kuwa atakaa pembeni lakini hamuishi kumuandama. Badala ya kupanga mta survive vipi miaka mitano ya kutoshiriki siasa nyie mmebaki kuwaandama waliokuwa wanachama wenzenu. Inaelekea mnaogopa kupambana na CCM.

Mbowe, Chaumma n.k. sio maadui wenu. Kaeni nao muone mtafanikisha vipi adhma yenu ya kuitoa CCM madarakani. Hiyo ndio inatakiwa iwe focus na sio kingine. Mbowe alipambana alivyojua yeye sasa ni zamu yenu kutuonyesha kuwa njia yenu italeta mafanikio. Mpaka sasa hamna mlicho fan ikiwa. Mlisema uchaguzi haufanyiki lakini "umefanyika" na serikali ya CCM iko madarakani pamoja na bunge lake. Na itakuwa hivyo mpaka "uchaguzi" ujao.

Amandla...
 
Babu…. Better this way!

Kuliko kuwa na chama ambacho Watanganyika tunaweka matumaini yetu hapo kumbe baadhi ya viongozi nyuma ya pazia wanashirikiana na CCM kutokufikia matakwa ya wananchi yenye mlengo wa kiukombozi.

Kila Chama kifutike ili siku tukianza tuanze upya, We seriously care less about CDM ya Mbowe. In a way hamuamini tukiwaambia kuna watu wanaipenda nchi kuliko vyama.

We have been played huh! No ninyi na Mbowe wenu ndio mmetuchezea kwa Miaka Mingi. Take this way: Kuna watu sababu ya uzalendo or being Naive wamepoteza maisha, wamepoteza mali au wameumizwa kwa kupigania maslahi ya nchi kumbe ninyi na mbowe wenu mnajua mnachofanya ikiwemo kuuza mipango na mikakati, Kuvujisha taarifa za vikao na hata whereabouts kwa watu walionekana ni threat, Kirahisi rahisi hivyo unataka watu kama hawa waone unachokiona “CDM ya mbowe ilikuwa na faida blah blah”?

Mr. Strategy, Strategy ilikuwa ni ipi sasa? Kuendelea kuisindikiza CCM hadi lini? Ushirika wa wachawi….

Sisi watanganyika tutafurahi CDM ikifutwa kuliko iwepo iolewe na CCM, Tunamsaliti namba moja wa wananchi ambaye ni CCM, na viwasaliti vya wananchi vikafu? Viaisiti na vichauma hatujitaji CDM kama msaliti!!!!! Mlichukue hili mliweke kwenye notibuku zenu.
 
Haya uliyonayo kwa FAM ni zaidi ya mahaba.
Kama uchaguzi tu wa chama umekuacha na majeraha namna hii, hivi kweli yale mauaji ya kuanzia 29 Oct. yanaweza kupona kwa Watanzania!!???
 
Ma ccm hayatakiwi kuendekezwa kwa siasa za Mbowe za mapendano, inatakiwa siasa za Lissu...ukiweka ugoko na yeye anaweka ugoko, nyeusi ni nyeusi full stop!.
Kwasasa hapa Tz hakuna mwanasiasa samuya anamuhara kama Lissu ndio maana akaona bora amuweke ndani kusudi asipate ushindani wa maana kwenye uchaguzi fake!.
Na hata hayo maridhiano ya kitapeli wanayoyataka ccm, mlengwa mkuu hapo ni chadema ikubali kushiriki ili kuyahalalisha kwa umma na duniani kwamba Tz sasa ni wamoja baada ya kujipaka kinyesi oct 29...chadema wakiyagomea hayo maridhiano (naombea iwe hivyo) moja kwa moja yatakuwa yamefeli kabla hata hayajaanza kufanyika kupitia vyama vingine vya kitapeli!!.
 
Cdm ya Lisu inaendeshwa kitaasisi na sio mtu. Unaongelea cdm ya Mbowe kama tajiri, lakini cdm chini ya Mbowe ilikuwa inaenda kudumaa maana tayari alitaka kujiona bila hela zake chama kinakufa. Cdm ya Lisu hata iwe nia shilingi 10m huo ndio uhalisia, kuliko kuwa na 100m za kificho toka kwa mafisadi.

Hao akina Lisu walimkimbia Magufuli na sio Samia, na bado wangeweza kurudi kwani hawakufukuzwa. Unataka kuonyesha ni Mbowe ndio aliwarudisha, kwani yeye ndio aliawaagiza wakimbie? Hao waliofungwa kwa uonevu ilikuwa ni haki yao kuachiwa, na hata wasingeachiwa vifungo vya hukumu zao za uonevu vingekuwa vimesha, maana hawakuwa wamefungwa maisha.

Unauliza sasa hivi cdm iko wapi wakati chama kimezuiwa kufanya shughuli za kisiasa! Ilitakiwa kisiwe kimezuiwa kisha uje na hizi porojo zako. Hakuna aliyetengwa acha upotoshaji wa kijinga, ukiona mtu anasema ametemgwa ujue ni team Mbowe wanataka wabembelezwe baada ya boss wao kupigwa chini. Na kwa kukusaidia tu, Mbowe hakutaka uchaguzi uwe wazi vile, bali alizidiwa nguvu na team Lisu kwani hao hawakuwa tayari kwa matokeo ya kihuni. Na iwapo team Lisu wasingekaza Mbowe leo hii bado angekuwa mwenyekiti.
 
Mpango wa ccm kutawala kwa aina yoyote tayari umeshakutana na pigo la kwanza Mo29. Ni juu ya cdm kukaza kamba hakuna na maridhiano ya kitapeli tena. Ni bora cdm isiwepo kuliko kuwepo huku ikiburuzwa kwa siasa za kilaghai na ccm.

Na kwa kukusaidi tu, kwa sasa cdm ndio imezidi kuimarika baada ya kugomea uchaguzi wa kihuni. Na kwa msisitizo huku kujitoa muhanga kwa cdm ndio kutaleta mabadiliko mengi ambayo chama kitakachofaidika ni cdm zaidi kuliko vyama vingine vyote. No pain no gain, kwenye uchaguzi huu cdm wamecheza heko. Ule upuuzi wa cdm ya Mbowe umehamia Chauma, na matokeo ya kuburuzwa yamewaathiri moja kwa moja. Tuko tayari cdm isishiriki hata miaka 10 hadi reforms za kweli na katiba ipatikane, kisha tuingie uwanjani ndio mtafurahia show.
 
Hamuwezi kuandika historia upya ili isometric mnavyotaka nyie. Hakuna kiongozi wa Chadema ( Mwenyekiti, Makamu Wake na Katibu Mkuu) ambae amesimama hadharani kukana mchango wa Mbowe kwa Chadema. Hakuna.
Hakuna mfuatiliaji makini wa siasa za nchi yetu ambae anaweza kusema kuwa Mbowe haku sacrifice sana kwa sababu ya chama chake na nchi yake.
Mbowe alipoingia kwenye Uenyekiti, Chadema haikuwa hii Chadema ambayo leo mnajifanya kuipenda.

Mbowe amekaa mahabusu mara nyingi tuu, ametumikia kifungo, amenyang'anywa mali zake, amegharamia chama chake kwa mwili na mali.

Mbowe ameandamana hata alipokuwa peke yake na binti yake. Wakati huo mashujaa wenu wamejifungia ndani au kwa masista. Na aliandamana kupinga mauaji. Mpambanaji Hilda Newton alijificha asionekane. Lissu alipokamatwa Mbeya, Mbowe alienda mara moja kuwa nae. Lissu akatuahidi kuwa kesi hiyo ataisimamia mwenyewe na atawashitaki binafsi waliompiga. Imefikia wapi?

Mbowe alikataa kupokea ruzuku kwa sababu alipinga matokeo ya uchaguzi na alihakikisha chama chake kinaendelea na shughuli zake.

Mbowe alipigania maisha ya Lissu. Mbowe alisimamia kesi ya Mdude mpaka akashinda. Watu wangapi wametoka jela kwa sababu ya mpango wa maridhiano ya Mbowe?

Heche amekiri wazi kuwa Mbowe ndie aliyemuingiza na kumlea katika siasa za upinzani. Na wako wengi kama yeye. Lissu amelea wangapi?
Unasema Mbowe amekuwa anavujisha siri za mikutano wakati ni Lissu ndie aliyempa swahiba wake Msigwa taarifa za mikutano wakati akishindana na Mbowe!
Kweli shukrani ya punda mateke. Lakini kuna uwezekano kuwa mnatumiwa na CCM kuhakikisha kuwa Mbowe anamalizika kisiasa. Sitashangaa kusikia kuwa mpo kwenye payroll.

Amandla....
 
Hatua za uundaji katiba mpya zipo hatua ipi?
Ushoga tz Upo au haupo..??Wanafanya mpaka sherehe na sare wanashona ma media zinasapot Enhe chadema ndio karuhusu mkuu..??Kwanza hakuna pahala chadema imesema tutaruhusu ushoga
 
Maridhiano ya kwanza ni kukiri na kuutaka radhi umma kwamba chini ya uongozi wake watu waliauwa , waliouwawa wako wapi ? Kama wapo watu wapewe wapendwa wao,

Naona ngumu kumeza 😂😂
 
Hatua !!?! Sawa. Tunasubiri
 

Mauwaji hayakufanywa kidini , kwani wafanyaji hawana dini. Wangalikuwa na dini wasingaliyafanya waliyoyafanya
 
Naunga mkono kulirudisha taifa na nchi katika Umoja...

Lakini ni lazima tuzingatie utaratibu wa kupata hicho tunachokitaka...

Tunachotakiwa kuunda sio TUME YA MARIDHIANO.

Chombo kinachotakiwa kuundwa ni tume ya kimahakama inayoitwa kwa jina halisi la TUME YA UKWELI NA MARIDHIANO (TRUTH & RECONCILIATION COMMISSION)...

Na kama yuko serious kweli, aachane mara Moja na kile alichofanya, kuunda Tume ya Jaji Chande. Huo ni uchafu na ni upuuzi 100%...

TRUTH AND RECONCILIATION COMMISSION hii ndiyo itakayotafuta ukweli wa kilichotokea, kujua na kuwatambua waliohusika na mauaji, kuwatambua walioathirika na matukio hayo ya mauaji, kupendekeza hatua za kuchukua na namna ya kwenda mbele...

Katiba mpya na mengine ni moja ya Suluhu au majibu ya matatizo ya nchi na taifa letu....

Lakini hatuwezi kurukia kuanzia kufanya suluhu kabla ya kuujua ukweli wa sababu zilizotufikisha hapa mpaka serikali inaua raia wake inayojidai kuwaongoza zaidi ya 10,000...!
 
Nchi nayo inavituko hii, badala ya kurekebisha mambo ya tume ya uchaguzi yaliyopeleka watu kususia uchaguzi na hatimaye kuuwawa unaenda tume uridhie nini. Tume yenyewe itajikuta ni waccm watupu wanakutana na kutoa taarifa ya kuridhiana. Labda kama tume ni kwa ajili ya kuwadanganya wafadhili.
 
Nchi nayo inavituko hii, badala ya kurekebisha mambo ya tume ya uchaguzi yaliyopelekea watu kususia uchaguzi na hatimaye kuuwawa unaunda tume uridhie nini. Tume yenyewe itajikuta ni watu wa ccm watupu wanakutana na kutoa taarifa ya kuridhiana. Labda kama tume ni kwa ajili ya kuwadanganya wafadhili
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…