GE2025 Samia: Kila Mtanzania atakuwa na shughuli ya kumuingizia kipato

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Bi mkubwa anaendelea kutupangilia. Mimi nipo siti ya mbele kupata hizo fursa za kupata vipato
====================
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya chama hicho ikipata tena ridhaa ya kuongoza dola itaifanya Tanzania kuwa taifa linalojitegemea katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya uchumi.

Akinadi sera zake hii leo Septemba 18, 2025 katika kampeni za chama hicho kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Samia ameeleza kuwa serikali yake itaandaa mpango maalumu wa kuwawezesha Watanzania wote kuwa na shughuli zinazowaingizia kipato huku akieleza kuwa hiyo ni njia mojawapo itakayosaidia kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi.

Rais Samia amefafanua kuwa mpango huo mbali na kukuza uchumi wa taifa utasaidia pia kuinua hali za maisha kwa Watanzania wote huku akiahidi pia kuimarisha ustawi wa jamii, kulinda amani, usalama na utulivu pamoja na kudumisha demokrasia na utawala bora.
 
Wakati anaongea hivyo alikuwa hajapiga kweli glasi ya altar wine! Maana hilo ni jambo lisilo wezekana kabisa.
Kama mpaka muda huu ameshindwa kuwaajiri walimu waliotapakaa kote nchini, atatumia njia gani kuhakikisha kila mtu ana shughuli ya kumuingizia kipato!

Hizi ni porojo/Hekaya za Abunuwasi bila shaka.
 
itaandaa mpango maalumu wa kuwawezesha Watanzania wote kuwa na shughuli zinazowaingizia kipato huku akieleza kuwa hiyo ni njia mojawapo itakayosaidia kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi
Alieleza pia nini kilikwamisha mpango huo kukwama kwa miaka minne iliyopita'?
 
Nipeni mtonyo na mie
Maana huku kijijini kwetu
Misaada mingi tunatoa kila wakati
Nitapata ya kusevia vitukuu wangu

Habari nzuri

Kazi iendeleeee
 
Ni sawa na Sista kufuatilia wacheza pornographia sijui anatafuta nini huko wakati masista hawaruhusiwi kubanduliwa
 
Bi mkubwa anaendelea kutupangilia. Mimi nipo siti ya mbele kupata hizo fursa za kupata vipato
====================
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya chama hicho ikipata tena ridhaa ya kuongoza dola itaifanya Tanzania kuwa taifa linalojitegemea katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya uchumi.

Akinadi sera zake hii leo Septemba 18, 2025 katika kampeni za chama hicho kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Samia ameeleza kuwa serikali yake itaandaa mpango maalumu wa kuwawezesha Watanzania wote kuwa na shughuli zinazowaingizia kipato huku akieleza kuwa hiyo ni njia mojawapo itakayosaidia kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi.

Rais Samia amefafanua kuwa mpango huo mbali na kukuza uchumi wa taifa utasaidia pia kuinua hali za maisha kwa Watanzania wote huku akiahidi pia kuimarisha ustawi wa jamii, kulinda amani, usalama na utulivu pamoja na kudumisha demokrasia na utawala bora.

No wonder anmeifungia JF ili info zisiwafikie Watanzania. Hata Lukas ameshindwa kufagilia huu uongo.
 
Back
Top Bottom