tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Akiwa Igunga Mkoani Tabora kwenye muendelezo wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM, Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga Kituo kikuu cha Mabasi Igunga pamoja na soko kuu la Igunga ikiwa atachaguliwa kuongoza tena Tanzania kwa kipindi kingine cha 2025/26.
Soma pia: Rc Shinyanga: Tumepokea shilingi bilioni 588 kila kona barabara zinajengwa chini ya Rais Samia
"Nakubaliana nanyi kwamba Igunga hii ya sasa ya maendeleo inahitaji stendi yenye hadhi yake ili kukidhi mahitaji ya mabasi makubwa kutoka mikoani kwahiyo moja ya jambo tutakalolifanya mkitupa ridhaa ni ujenzi wa stendi."
Amesema Samia. Aidha amesema dhamira ya kujengwa kwa kituo hicho cha mabasi pamoja na soko la Igunga ni kufungua na kutanua wigo wa biashara kwenye Wilaya hiyo, suala ambalo litakwenda sambamba na ujenzi wa barabara za viwango vya lami katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.
Dkt. Samia amesema miongoni mwa barabara zitakazojengwa ni pamoja na barabara ya Igunga- Mbutu- Igurubi, Choma- Simbo pamoja na barabara ya Igunga- Mwanzugi.

Chanzo: Lemutuz TV