Samia moja ya ubora wake ni kuongea ukweli kuhusu uwezo wake. Hapendi majivuno anakubali hali na sifa zake hata kama nyingine ni dhaifu

Angalia mfano mwingine nakupa.

Pale juu umezungumzia ukweli wa Samia anapokiri hawezi kufanya ufuatiliaji kama wa mtangulizi wake.

Ujue hii kauli yake itaisababishia serikali hasara ya mabilioni, kwasababu wezi sasa watakuwa na amani, watapiga sana pesa zetu walipa kodi kwenye miradi ya serikali.

Hiyo kauli inaendelea kutufanya tuwe taifa la "business as usual". Kwangu nalaani sana huu udhaifu, hasa pale kiongozi mwenye mamlaka anapokiri anao.
 

Ukweli wake Una positive na negative impacts

Negative upo kama ulivyoeleza.
Positive ni wananchi wataona umuhimu wa kuchagua kiongozi mwenye competent
Lakini vipi ukachagua mwenye competent lakini asiwe mkweli kuonyesha madhaifu yake katika maeneo mengine?

Mfumo unaotakiwa ni kuunda mfumo usiotegemea mtu mmoja(Rais) pekee
 
Sasa mkuu, kwa nafasi yake unadhani anaweza kudanganya watu wasijue? Lazima wajue tu ndio maana lazima mtu akihojiwa aseme ukweli dunia isimuumbue.

Hata kama angekuwa na good sense of humour au anajushusha, kila kitu kimekuwa denounced tarehe 29, hakuna tena anachoweza kuongea mtanzania akamuelewa, ameshindwa kukiri na kuomba radhi kwamba aliuwa watanzania, nguvu iliyotumika ni sahihi kwa mazingira, hicho ni kiburi kikubwa sana na majivuno kwamba hata niseme nini, nina backup ya jeshi na hakuna wa kunigusa.

Hakuna raisi au mtu anayeingia ikulu na ujuzi wa ikulu, kila mtu anaingia akiwa hajui anaenda kukutana na nini. Kusema kuna mambo hajui ni sawa, ila kujifunza kuishi mazingira mapya na kuyahimili ni kitu kingine, ndio maana tunasema ABILITY and COMPETENCE!!
 
"Mwenye competence lakini asiwe mkweli"

Afadhali huyu, kwasababu mwisho wa siku matendo ni bora zaidi ya maneno.

Kuliko kuwa na kiongozi anayekiri hawezi kutimiza majukumu yake, kwangu ni afadhali niwe na kiongozi anayeweza kutimiza majukumu yake, hata kama akiwa muongo.

Naamini hata akidanganya tutajua ukweli tu.
 

Viongozi wenye majivuno kusema wanajua Kia kitu hujawahi kuwaona au kuwasikia?

Ni kweli Samia anapwaya maeneo ya uchumi wa zile project kubwakubwa kutoenda kwa wakati.
 

JPM alikuwa na sifa unayoitaja hapo.

Unajua tabia za mtu ambaye anamajivuno anapotawala?
 
Viongozi wenye majivuno kusema wanajua Kia kitu hujawahi kuwaona au kuwasikia?

Ni kweli Samia anapwaya maeneo ya uchumi wa zile project kubwakubwa kutoenda kwa wakati.
Mkuu,
Anapwaya, usitake kumpaka mafuta wakati anapwaya kila mahali. Watu walidhani kwenye demokrasia na siasa safi angefanya vizuri, hasa alivyoingia tu, lakini ukweli ni kwamba hata kwenye demokrasia amefeli sana, hana political tolerance kama mtangulizi wake tu, hili lilikuwa eneo pekee angefanya vizuri historia ingemkumbuka sana, ila look at her now!

Huku kwenye uchumi na maendeleo, usimamizi wa rasilimali wala tusiongee, ukweli uanujua nae anaujua.
 
Nafasi aliyokalia Samia ni ngazi kubwa sana kwake. Polepole alijitahidi sana kumwambia lakini akaamua kumsikiliza mkwere(Samia aliwahi kukiri huyu ni "bosi" wake - kosa kubwa sana) ambaye naye alipwaya kwenye mambo mengi sana. Na mkwere anafahamu uwezo wa Samia ni wa kawaida sana hivyo kuboronga kwa Samia inamnufaisha mkwere kwa kuwa mapungufu ya Samia yamekuwa makubwa sana kuzidi ya kwake mkwere.

Samia angemsikiliza Polepole angejijengea heshima kubwa sana. Ataishia kukumbukwa kama kiongozi aliyebariki mauaji ya MAELFU ya raia zake. Hiyo itamtafuna maisha yake yote.

Wahenga walisema "Majuto ni mjukuu"
 
Asante kwa kuuma na kupuliza!!
 
.

15. Wengine huona aibu, wengine huhisi watadharaulika. Lakini ukweli unakawaida moja. Kukuumiza kwa muda lakini kukupa heshima baadaye.


Hakuna Raisi, ukiacha Nyerere, atakayekuja kukumbukwa na kuheshimika huko mbele kama Dr Samia Suluhu Hassan. Ni suala la muda tu.

Samahani, hivi meta mada huogopi kutukanwa na haters wa Samia?!!!
Maana wao hawataki kusikia neno lolote positive kwa Samia, ukilitoa basi ugomvi......tena haters wengine wanakasirika Hadi wanapiga ngumi Kuta za nyumba zao kwa hasira
 
Hiyo kauli inaendelea kutufanya tuwe taifa la "business as usual". Kwangu nalaani sana huu udhaifu, hasa pale kiongozi mwenye mamlaka anapokiri anao.
Niambie tofauti iliyopo kati ya uzito na ujazo, mfano ana uja[zo]-uzito unaelewa maana yake?
 
WaTz tuna kawaida ya kutreat kila jambo kwa ukawaida kawaida, na kuchanganya mambo na misingi ya mambo.

Hii ni nchi sio mahusiano, we can’t accept lame excuses na second chances.

Rais akiona hana uwezo haitoshi kujikubali kuwa sina uwezo, bali anapaswa kustep down kujiuzulu, si huna uwezo? unataka nini sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…