Hamjambo Wore!
1. Kila kiongozi kama walivyo binadamu wengine Wana ubora na udhaifu wake.
2. Ni nadra Sana Kwa viongozi wengi wakubwa kukubali udhaifu mbele za watu.
3. Hata Wazazi nyumbani wengi wao hawakubali ukweli kuhusu udhaifu wao.
4. Hii ni Tofauti na Samia. Mara kadhaa nimemsikia akizungumza bila wasiwasi kuhusu udhaifu wake.
5. MTU mkubwa mwenye cheo kikubwa sio Jambo la kawaida kutaja sifa zake ambazo ni udhaifu. Mara nyingi hii huwa kiashiria cha Unyenyekevu na kutokupenda Majivuno.
6. Ni kweli Samia hapendi Majivuno. Atu tuseme hana majivuno. Na watu wasio na majivuno kikawaida hawapendi mashindano. Na watu wasiopenda mashindano hawapendi kugombana gombana.
7. Samia nilimsikia wakati Fulani akijielezea kuhusu CV yake. Aliongea ukweli wote. Aliitaja historia yake hasa ya elimu ambayo sio historia yenye nguvu na utukufu. Hakuwa kipanga, hakuwa na zile Akili ambazo wengi huzitamani.
8. Pamoja na historia hiyo ya elimu isiyo na utukufu lakini aliisema waziwazi na akikiri kwamba Hakusoma Sana.
Kwa Sisi wataalam wa saikolojia sio Jambo rahisi MTU kuzungumza mbele ya umma historia isiyo na utukufu.
9. Wengi hupenda kuelezea mambo mazuri, makubwa na yenye utukufu waliyoyafanya huko nyuma. Huku wakiacha kuelezea udhaifu wao. Lakini Samia kwa Hilo hayupo hivyo.
10. Samia angeweza kunyamaza tuu na kutoeleza lolote kuhusu ukweli wa elimu yake lakini hakuona kama akisema itamdhuru.
Zaidi ita inspire watu wengine wengi ambao walikuwa au Wana uwezo wa kawaida au wachini katika Elimu au mambo mengine.
11. Samia amekiri mara kadhaa nchi yetu ni Maskini. Huo ni ukweli ambao viongozi wenye majivuno hawaupendi.
12. Umaskini wa nchi haupo kwenye resources bali upo katika Hali halisi ya mifuko ya watu na akili za watu.
Ni kweli nchi yetu ni maskini kwa sababu inawatu maskini wa pesa na akili. Haimaanishi hawapo wachache wenye vipato au wenye akili kama Sisi watibeli.
13. Samia juzi nilimsikia akiongea kuhusu Ukweli kuwa yeye Hana uwezo wa kufuatilia na kusimamia mambo Hasan ya miundombinu ya ukandarasi na uhandisi kwa sababu yeye sio mtaalamu WA mambo hayo. Huku akikiri wazi kuwa mtangulizi wake yeye alikuwa Bora kwenye eneo hilo.
14. Kwa Sisi Watibeli tunaposikia Mtu akiongea Ukweli hasa unaomhusu yeye mwenyewe kwa upande wa udhaifu wake tunampa Credits kadhaa. Kwa sababu ni Jambo ambalo wenye viburi hawaliwezi.
15. Wengine huona aibu, wengine huhisi watadharaulika. Lakini ukweli unakawaida moja. Kukuumiza kwa muda lakini kukupa heshima baadaye.
16. Samia amekuwa akikiri kuwa yeye ni binadamu na wanadamu wanakosea. Hilo hata waliochini yake wanafaidika nalo. Ukikosea kwa Samia basi kusamehewa utasamehewa hii ni tofauti na wasiopenda Ukweli.
17. Tatizo la watu Aina ya Samia ni suala la maendeleo. Watu Aina ya Samia sio Wazuri kwenye maendeleo ya haraka kwa sababu ni watu wanaotoa nafasi zaidi ya mara nyingi pale MTU anapokosea.
18. Naweza kusema, kwa saikolojia hiyo inaniambia Samia ni wale watu ambao walikuwa wamepewa nafasi nyingi, waliopewa Neema nyingi licha ya kutokuwa na uwezo toshelevu. Hivyo naye haoni shida kutoa nafasi kwa wale ambao wanakosea au kutokuwa toshelevu. Kuwapa nafasi. Kuwapa nafasi ya pili.
19. Hii ni tofauti na Wale watu ambao wao walipita moja kwa moja. Ambao hufanya Jambo mara moja bila kutegemea second chance. Hawa wanakuwa kidogo harsh. Na wengi hawapendelei mfumo wa kutoa nafasi mara mbili.
20. Samia hapendi majibizano. Kama nilivyosema hapo juu. Watu wasioona kukiri udhaifu wao mbele za watu. Hawapendi mashindano.
21. Ndio maana tangu 2021 Alipoingia amejibu mashambulizi ya mitandaoni mara chache Sana.
Ni tofauti Sana na watu Aina ya JPM, kina Donald Trump ambao hawa wanamajivuno, majigambo na wanapenda ligi.
22. Kwa watu aina ya Samia nchi kuwa tulivu, salama na haki na utu kuzingatiwa ni Jambo la uhakika kwa kiasi kikubwa isipokuwa kama kuna shinikizo la vyombo vya Dola.
23. Samia mnaweza kuwa na ugomvi lakini akajikaza akatokea kwenye shughuli zako.
24. Kuhusu anastahili kuongoza au hastahili?
Kikatiba ya nchi anastahili.
Kuhusu kupitishwa kiholela kiujanjaunjanja mwaka Jana hiyo hastahili.
Kuhusu Uwezo anastahili kwa sababu nchi inaongozwa kwa Sheria na hakuna kipimo cha uwezo wa watu kuongoza.
25. Je anastahili kuheshimiwa?
Inategemea.
Kama atatenda mambo Mema na Mazuri heshima yake ni haki yake.
Kama hafanyi hivyo hastahili kuheshimika.
26. Anastahili kuheshimiwa kama Mama na mwanamke mtu mzima kama havunji heshima ya Umama na uanamke.
Anastahili kuheshimika Kama Rais na Amiri jeshi mkuu kama anafuata misingi ya nafasi hiyo.
27. Heshima moja ikivunjwa haivunji heshima zote. Inavunja heshima iliyovunjwa.
Mfano;
Ikiwa Rais au Waziri amejivunjia heshima yake katika mambo ya uongozi basi heshima itakayovunjika ni Ile inayohusu uongozi wake na sio heshima zingine kama heshima ya Ubaba/umama, ukaka/udada, na heshima zingine za kibinadamu.
28. Raia au mtu yeyote anapokosea na kujivunjia heshima yake katika eneo Fulani haimaanishi heshima zake zote zimevunjika. Hivyo utaacha kumheshimu kama kiongozi lakini heshima yake kama Mwanamke/mwanaume, Baba/Mama, itabaki palepale.
29. Mkeo/mumeo anapokuvunjia heshima ya ndoa labda kwa ku-cheat. Heshima iliyovunjika ni ya ndoa. Lakini bado lazima umheshimu kama Mama/baba wa watoto wako. Au mtoto wa mtu.
30. Mtu anapofanya uhalifu labda ameiba. Atavunja heshima ya uaminifu. Lakini sio kwamba mti huyo ni mbaya maeneo yote. Kama ilivyo mtu alivyomwema katika eneo Fulani haimaanishi ni mwema katika maeneo yote.
31. Hivyo hivyo Watibeli Tulivyo.
Naenda Zangu!
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Nasisitiza na narudia hapa Samia ndio Rais wangu Bora zaidi kuwaho tokea.
Hakuna namba ambayo hajaipita Wala kuacha alama kubwa sekta zote hapa Tanzania
Pili kuhusu aina ya watu,binafsi napendelea viongozi dizaini ya Samia badala ya hao kina Magu,Lisu ,huyo ropo ropo wa USA na wengine wa hivyo.
Hao wanaweza Wana chance kubwa ya Kuharibu kuliko kujenga ndio maana Leo hii umesikia CAG alisema bwawa la Nyerere limeleta hasara a Zaidi ya Trilioni 1 Kwa sababu za ukurupukaji wa kina Magufuli.
Magu hajasababisha hasara hiyo tuu hata pale jangwani kweymafuriko yeye Kwa ego yake alilazisha ujenzi wa karakana ya mabasi ya mwendokasi,Bado makesi kibao ya Nchi kushitakiwa,Mara samaki mara nini.
Maviongozi mapenda sifa Huwa ni ya hovyo.
Magu ndio alileta machawazakaharibu mfumo wa utumishi wa Umma na kujenga watu tegemezi,aliharibu biashara nk nk.
Much know hawafagi hata kidogo,Samia anafanikiwa ni Kwa sababu ametoa nafasi Kwa watu kuonesha vipawa vyao.
Udhaifu wake unaoneka ni kwa sababu hatuna mfumo unafanya kazi bila kutegemea mtu wa mwisho.
Yaani mtu(mjinga) anaona ni sahihi PM au Rais kuzunguka kutatua kesi za ndio na migogoro ya Ardhi il haoni kwamba Kwa nini Ngazi zote Kuna viongozi lakini hiyo migogoro ipo.
Watu wajinga hapo ndio wanatafsiri Kiongozi shupavu na watu Hawa wanajua utaratibu huo kwamba ulianziahwa na Magu lakini nawakumbusha tuu utaratibu huo ulianzishwa na Lowasa akiwa PM.