upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Rais Samia Suluhu Hassan amesema
kuwa moja ya matamanio yake makubwa ni kuufanya Mkoa wa Tanga kurejea kwenye hadhi yake ya zamani kama mkoa wa viwanda.
Akizungumza leo Ijumaa, Februari 28, 2025, katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, alipohitimisha ziara yake ya siku sita, Rais Samia amesema kuwa tayari Serikali imeanza kupanua viwanda vilivyopo na kujenga vipya ili kuongeza ajira kwa wananchi.
Soma: Rais Samia ahahidi miradi mikubwa ya maji, barabara na bandari mkoani Tanga
Kauli hiyo ni majibu kwa ombi la Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, aliyependekeza Serikali iufufue uchumi wa mkoa huo kupitia viwanda.
"Nataka Tanga iwe ya viwanda tena ili vijana waachane na kupoteza muda vijiweni wakinywa kahawa na kupiga majungu," amesema.
Ameahidi kulegeza masharti ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi na kuimarisha uchumi wa mkoa huo.