GE2025 Samia: Nitawaboreshea usikivu wa TBC Taifa hapa Singida ili iweze kusikika vizuri

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hiyo nayo ni sera ya kunadi mbele za watu wenye akili timamu?
 
Ndio vitu anavyoweza kuongea. Ndio maana hawajataka kuwe na mgombea wa maana , angeleta changamoto. Hata hao wagombea wa kawaida, wanapangiwa ya kuongea. Maana wakiongea tu ya kwao kichwani, wanampiku kwa sera na maongezi ya maana. Ndio maana hata CCM B mwenzao Mpina wamempiga pini kwanza asiongee ongee, maana atamuacha Bi Mdashi kwa mbali sana. Watanzania tumeula wa chuya hapa..
 
kumbe na wewe umeliona hili yani hawa wapinzani wa mchongo wanaongea sera nyepesi ama ambazo hazina mashiko kabisa na wengine wanasifia kabisa ccm na kuipinga chadema.
 
Mgombea wa kuchaji wallah kazi ipo mwaka huu😂😂
 
Aisee hii dharau kubwa sana ni sawa na mtu Leo akuambie nitakununulia kibatari kwakuwa huna umeme.
 
Daah
 
Hii habari usingeileta mkuuu, yani ungeacha hivo hivo watu wa singida wamsemee weee wasahau ili wakija kutuambia tuwaite waongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…