GE2025 Samia: Reli ya SGR na kuupanua uwanja wa ndege wa Mara, kutaleta mageuzi ya kiuchumi

GE2025 Samia: Reli ya SGR na kuupanua uwanja wa ndege wa Mara, kutaleta mageuzi ya kiuchumi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ikiwa atapewa nafasi ya kuunda serikali kupitia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, atauendeleza na kuupanua uwanja wa ndege wa Mara ili kuufanya kuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa na hivyo kukuza uchumi na biashara ndani ya Mkoa huo.

Dkt. Samia pia amesema kukamilika kwa reli ya Kisasa ya SGR kutoka Bandari ya Tanga- Moshi- Arusha mpaka Musoma kutaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi Mkoani humo, akiwaomba Watanzania kukipa kura Chama Cha Mapinduzi ili waweze kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo.
 
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza nchi Oktoba 29, 2025 baada ya uchaguzi mkuu kumalizika atauendeleza na kuupanua uwanja wa ndege wa Mara ili kuufanya kuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa ili kukuza uchumi na biashara ndani ya Mkoa huo.

1760081459431.png
Dkt.Samia Amesema hayo jana Alhamisi Oktoba 09, 2025, wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa Musoma Mjini Mkoani Mara kwenye muendelezo wa Kampeni zake Mkoani humo, akieleza pia ahadi yake ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kama ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 ilivyoelekeza pamoja na ufufuaji wa bandari za Mkoa huo.

Amesema kukamilika kwa reli ya Kisasa ya SGR kutoka Bandari ya Tanga- Moshi- Arusha mpaka Musoma kutaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi Mkoani humo, akiwaomba Watanzania kukipa kura Chama Cha Mapinduzi ili waweze kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha,pia amewatahadharisha wananchi wa Mkoa wa Mara kuhusu baadhi ya watu wanaopita kwao na kuwarubuni kutokukichagua Chama Cha Mapinduzi, akiwaita kama watu walionuna na wanaotaka kukikomoa Chama hicho, akisisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM hakiwezi kukomolewa na badala yake amewahimiza wananchi kukichagua kwa kishindo ili kuwaletea maendeleo kwa miaka mitano ijayo
 
Back
Top Bottom