Samia Suluhu baada ya kutembelea ziara Korea Kusini, wamarekani watoa uzushi

Huyu ngeti kaandika kwa kukurupuka

Ova

Nafikiri umefika wakati hata kiongozi wa nchi inabidi tumjue uelewa wake vizuri.
Je, ni mchumi ,au mwanqsheria ,au Mwanasayansi asiyekubali mambo bila fact na data za kutosha au shujaa wa kivita kama Kagame au Mwenye kipaji tu kama Paulo Makonda !!
Lakini inawezekana tunaongozwa na mtu aliyeshinikizwa tu kushika dola la watu mil.65 kutokana na nchi kuwa na watu wasiofuatilia mambo yanayohusu taifa lao na vizazi vijavyo zaidi ya kuimba ,"Ni ile ile ooh ni ile itajulikana " Mbele kwa mbele ".

Tutaangamiza taifa letu kiuchumi,kiutamaduni na kiusalama kwa sababu ya wanasiasa na watawala wanaowaza kujilimbikizia mali binafsi na familia zao kwa kushirikiana na wageni.

Hivi wangekua na nia njema wangeshindwa kuwaorganize wafanyabiashara wa ndani wakajenga mahoteli na viwanja vya ndege Kwenye mbuga za wanyama kama ilivyo kwa Wageni.

Hivi hawajui kuwa pale kilipojengwa kiwanja cha ndege cha Kia ndipo yalipo Madini ya Tanzanite na kilijengwa kimkakati na sio kama wanavyofikiri kuwa ni kwa ajili ya utalii. ingekua utalii si kingejengwa Arusha ?
Pale KIA ndipp penye madini hasa ya Tanzanite.
Sasa wamepewa Waarabu wajifanye kuwa wanafanya upanuzi wa Kiwanja.
Yetu macho , tumeamua kumpa mjukuu wa Sultani wa Oman urithi wetu .

Ndugai alisema ,2025 mtaamua wenyewe nchi ipigwe mnada au tuendelee kukopa kopa na kutembeza bakuli
 
nilikuwa natafuta hii koment, nimechoka na kuchoka kusoma kuwa korea kusini imewekewa vikwazo,

Hao ndio machawa wanaoishi kijanja janja na kuwakoromea watu wanazuoni mahiri na wataalamu wa sheria na siasa kama Tundu Lisu, Mwabukusi, Warioba, Butiku, Ndugai, Polepole n.k .

Na utakuta mleta mada amepigiwa na simu ya pongezi kwa uzalendo na kumtetea mama . Mwishowe anapata uteuzi .
 
Bollen Ngeti,

Sijuie kwanini huyu jamaa Huwa namfananisha na kampani ya kina Benard Membe,William malechela na Lazaro nyalandu!

Mwenye uelewa tafadhali!!
 
Nafikiri umefika wakati hata kiongozi wa nchi inabidi tumjue uelewa wake vizuri.
Je, ni mchumi ,au mwanqsheria ,au Mwanasayansi asiyekubali mambo bila fact na data za kutosha au shujaa wa kivita kama Kagame au Mwenye kipaji tu kama Paulo Makonda !!
Lakini inawezekana tunaongozwa na mtu aliyeshinikizwa tu kushika dola la watu mil.65 kutokana na nchi kuwa na watu wasiofuatilia mambo yanayohusu taifa lao na vizazi vijavyo zaidi ya kuimba ,"Ni ile ile ooh ni ile itajulikana " Mbele kwa mbele ".

Tutaangamiza taifa letu kiuchumi,kiutamaduni na kiusalama kwa sababu ya wanasiasa na watawala wanaowaza kujilimbikizia mali binafsi na familia zao kwa kushirikiana na wageni.

Hivi wangekua na nia njema wangeshindwa kuwaorganize wafanyabiashara wa ndani wakajenga mahoteli na viwanja vya ndege Kwenye mbuga za wanyama kama ilivyo kwa Wageni.

Hivi hawajui kuwa pale kilipojengwa kiwanja cha ndege cha Kia ndipo yalipo Madini ya Tanzanite na kilijengwa kimkakati na sio kama wanavyofikiri kuwa ni kwa ajili ya utalii. ingekua utalii si kingejengwa Arusha ?
Pale KIA ndipp penye madini hasa ya Tanzanite.
Sasa wamepewa Waarabu wajifanye kuwa wanafanya upanuzi wa Kiwanja.
Yetu macho , tumeamua kumpa mjukuu wa Sultani wa Oman urithi wetu .

Ndugai alisema ,2025 mtaamua wenyewe nchi ipigwe mnada au tuendelee kukopa kopa na kutembeza bakuli
Kwa nini ujenge kiwanja cha KIA juu ya deposits za Tanzanite?
 
Marekani inailalia Korea ya Kaskazini na kuiona Korea ya Kusini kama “nunda”?

Hapo umechanganya madesa!
Na Mimi nikasugua macho yangu nikadhani na usingizi ndiyo sababu naona Kinyume nyume...Kha!
 
Mwandishi ni mmoja wa wasomi wajinga waliojaa hapa nchini.
Kuna mtu nilisoma nae high school,mpaka anafika form 5 alikuwa anajua USA ipo bara la Ulaya,ukijaribu kumuelimisha anakuwa mtata.
 
Ni hawa hawa Korea Kusini walikubali kutufungia mitambo hiyo tena kwa "Siri Kubwa" Marekani isijue maana ingeleta mushkeli wa kidiplomasia kati yetu na wao. Wakijifanya wakulima wa mboga -mboga mchana lakini kumbe ni mainjinia walifuzu, Wakorea walifunga mitambo.
Kwa nini unaweka siri za jeshi letu hadharani hivi? Hicho kibali umekipata wapi? Uzuri umetuwekea na namba yako ya simu hapo tutajua namna ya kufanya!
 
Marekani inailalia Korea ya Kaskazini na kuiona Korea ya Kusini kama “nunda”?

Hapo umechanganya madesa!
Hata mimi nimeshangaa! Tangu lini Marekani akawa rafiki wa Korea Kaskazini na kuisulubu Korea Kusini?
 
Mimi nikisikia tu Marekani wanalalamika hata kama sijasoma mkataba najua fika lazima itakuwa na tija Kwa nchi kwakua wao huwa hawapendi nchi ipate kitu chenye tija

Huku ndiyo kuishiwa uelewa.

Pesa ya USA ya MCC ilipeleka umeme vijijini kwa 80%, ilijenga barabara toka Tunduma mpaka Sumbawanga. Na pia miradi minhine mingi mbalimbali. Kwako hivyo vyote havikuwa na tija kwa Tanzania? Kweli wengi humu wanachojua ni kuandika, kusoma na kuhesabu tu!!!
 
Na Bollen Ngetti
0683 226539
B-pepe bollenngeti@gmail.com

SIKU tatu kabla Rais Samia Suluhu Hassan hajaelekea Korea Kusini kuhenyea kwa ajili ya nchi yake niliandika huko kwa Max (X) kwamba, "Rais Samia unaenda Korea Kusini lakini jiandaye na matusi, kejeli , dhihaka na hata uzushi kutoka Marekani".

KWELI, Rais Samia Suluhu Hassan amefika Korea na kufanikisha dili la mkopo wa Shilingi 6.57 Trilioni wa sharti nafuu ikiwamo riba ya 0.01% kwa muda wa miongo 4 inayoanzia 2026. Fedha ambayo itaelekezwa katika miradi ya kimkakati inayolipa kama sekta ya usafirishaji na uchukuzi!

Mara baada tu ya Rais kufanikisha jambo letu HIMA Marekani kupitia sauti yake, Voice of America, VoA ikaandika uzushi, dhihaka na matusi kwamba, "Tanzania imesaini mkopo wa fedha na Korea Kusini kwa sharti la kugawa sehemu yake ya bahari na madini". Ujinga uliovuka mawingu!

Hivi, katika hali tu ya kawaida Rais Samia ni mwendawazimu, mjinga, asiye na akili wala uzalendo kiasi gani hadi atoe sadaka ya sehemu ya bahari na madini yetu kwa gharama ya mkopo ambao bado tutailipa? Kwa nini isingekuwa mbadilishano wa hayo matrilioni na kipande cha bahari na madini ili lojiki iwepo? Yani unaenda kwa Mangi unamwambia akukopeshe mchele wa kilo 50 kwa ajili ya shughuli ya binti yako utamlipa mwisho wa mwezi na hapo hapo unamwambia njoo nyumbani nikupe fremu bure pamoja na kwamba mchele wako nitakulipa mwisho wa mwezi! VoA na Joseph Biden mmetukosea sana kwa ujinga huu. We can be stupid but not fool to that extent!

Watanzania tuelewe mambo mawili hapa kama si moja kubwa! Na atakayeelewa awaeleweshe wengine 10 wasio na smart phones. Kwanza kuna vita kubwa ya kiuchumi duniani. Kila Taifa linatumia kila aina ya mbinu halali na haramu kujiweka sawa kiuchumi maana uchumi ndio kila kitu.

Na moja ya mbinu ya mataifa makubwa ni pamoja na kudhoofisha nchi zingine kiuchumi, kiteknolojia na ikibidi hata kisiasa na kijeshi. Marekani kupitia shirika lake la kijasusi ilitumia kila mbinu chafu kuwatenganisha ndugu wa tumbo moja KOREA ikazaliwa Korea Kusini na Korea Kaskazini huku USA ikilalia Korea Kaskazini na kumuona Korea Kusini kama "nunda" na adui. Korea Kusini imewekewa vikwazo chungu nzima na Marekani hasa katika eneo la ubunifu wa teknolojia ya zana za kivita bila mafanikio.

Wananchi wa Korea Kusini waliamua kushikamana na kujenga uzalendo kwa nchi yao wa kupigiwa mfano baada ya kuona, "hatuna ndugu wala mjomba, lazima tujikomboe wenyewe" na pakwanza walipoanzia na kupambana na kushinda saratani ya rushwa na ufisadi na kumtambua kila Mkorea Kusini alipo ndani na nje ya nchi yao na anafanya nini kwa maslahi ya Korea Kusini!

Nimkumbushe Mtanzania jambo ambalo limewahi kutokea lakini haikuandikwa popote na kokote rasmi! Miaka michache tu zilizopita Jeshi letu la Ulinzi limewahi kuwa na haja ya Rada kwa ajili ya Ulinzi wa anga ambayo ingefungwa Morogoro. Maombi yalienda kwa nchi nyingi ikiwemo USA ya Joseph Biden aka Joe Biden bila mafanikio.

Ni hawa hawa Korea Kusini walikubali kutufungia mitambo hiyo tena kwa "Siri Kubwa" Marekani isijue maana ingeleta mushkeli wa kidiplomasia kati yetu na wao. Wakijifanya wakulima wa mboga -mboga mchana lakini kumbe ni mainjinia walifuzu, Wakorea walifunga mitambo.

Hata hivyo USA ilipogundua ilileta shida lakini kwa ukomavu wetu wa kidiplomasia Tanzania ya Jakaya Kikwete iliwaambia USA, "sisi tuna shida ya Rada, kama hamtami hawa watufungie basi mtupe yenu". USA ilikubali lile sharti na Korea Kusini ikafungasha virago maana na wao hawakuona sababu ya magomvi yao kutuathiri. Tuna historia ndefu na Korea Kusini kuliko USA kama nitakavyoeleza kupitia gazeti moja ya gazeti la wiki!

Kwa mantiki hiyo sikushangaa hata kidogo kwa Marekani kupitia TBC yao ya umma kutoa uzushi wa kijinga wenye lengo la kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wake kupitia mawakala wao ndani ya nchi kusambaza ujinga huo kuelekea Uchaguzi wa S/M kisha Uchaguzi Mkuu 2025 kwamba "Samia anauza nchi yetu" ili tu Samia achukiwe na chama chake! Huu ni uzushi wa kipumbavu usiovumilika na ninaamini USA itaomba radhi.

Tanzania ni nchi huru na sera yetu siku zote ni kutokufungamana na upande wowote katika vita za kiulimwengu. Hatuchaguliwi adui wala rafiki. Tunachoangalia ni maslahi mapana kwa nchi yetu na watu wake. Leo Iran imewekewa kila aina ya vikwazo vya kiuchumi lakini sisi ni marafiki na Iran na tunafanya nao biashara chungu mzima ikiwemo gesi asilia.

RAIS Samia wewe piga kazi! Hizo ni kelele tu za chura! Wewe hata chama Cha Hamas kikikubali kutujengea Zahanati kila kila Kijiji wewe nenda kasaini mikataba. Tungesikia kelele zao leo tungekuwa na Hospitali ya Palestina pale Sinza? Uongo ukiachwa kusikika sana hufikia hatua ya kuaminika kuwa ni kweli. Ukemewe mapema na kila mzalendo wa nchi YETU!
04/6/2024
Time: 11:23
Dar es salaam

Pia soma: VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Hili andiko lote ni takataka kabisa kwa sababu mwandishi inaonekana ni mtu ama asiyejua chochote na ni mropokaji au mtu mnafiki na mwongo anayemini kuwa ana uelewa wa kuwadanganya watu wote.

Fikiria mtu ambaye ama haijui kabisa nchi ya Korea Kusini au anayeamua kusema uwongo dhidi ya Korea Kusini. Yaani kwa Ulimwengu huu wa leo, ukiona mtu haijui Korea Kusini wala Kaskazini, haijui Marekani, unadhani uduni wa uelewa wa mtu huyu ni wa kiwango gani??

Fikiria mtu mwongo aliyekosa uelewa kama huyu Bollen Ngetti anayeweza kuubadilisha urafiki na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya South Korea na USA, na kuugeuza kuwa eti ni uadui, anastahili kuwekwa kwenye kundi gani?

Huyu Bollen Ngetti ameandika uwongo huu kwa sababu ni mbumbumbu sana au kwa sababu ni mtu mwongo, mnafiki?

Korea Kusini ni rafiki mkubwa wa USA, ni nchi iliyopokea misaada mingi kutoka USA kuifikisha kiuchumi hapo ilipo. Ni nchi ambayo ilipewa privileges nyingi kwa soko la USA ili iinuke. Ni nchi ambayo, USA imepeleka FDI kubwa sana. Ni nchi ambayo hata jeshi lake lilijengwa sana na USA, na mpaka sasa wanashirikishana sana kwenye taarifa za kiulinzi na usalama na kufanya drills za kijeshi kwa pamoja, karibia kila mwaka. Halafu mtu, sijui kama ni kwa kudhamiria au kukosa uelewa, anasema kuwa ni nchi maadui!!

Bollen Ngetti apuuzwe kwa andiko hili la uwongo, uzushi na lililokosa weledi.
 
Kwani RUTO MAREKANI walimpa nini?
Hii pesa USangeitoa ingetangazwa dunia nzima.
 
Marekani ni Nchi ya kipumbavu,wao Misaada Yao ni ya ujinga ujinga na hawawezi kukupa hela yote Kwa pamoja.
Kama Marekani ni nchi ya kipumbavu kama unavyoropoka hapa huyo Sa100 alikwendaga kutafuta nn huko??
Na akitoka Korea anarudi tena huko Marekani muambie basi asiende kwa wapumbavu!.
Pale chawa anapokosa kumbukumbu!
 
Mama hajioendekezi kwa mtu na sisi pia sera yetu kimataifa inafahamika vyema kabisa. Hatuna budi mtu wala kufungamana na mtu yeyote yule waka kupewa adui wa kumchukia na kutokushirikiana naye.

Sera inasema hivyo lakini mbona wewe kada unaonekana unaupande unaoukubali zaidi
 
Huku ndiyo kuishiwa uelewa.

Pesa ya USA ya MCC ilipeleka umeme vijijini kwa 80%, ilijenga barabara toka Tunduma mpaka Sumbawanga. Na pia miradi minhine mingi mbalimbali. Kwako hivyo vyote havikuwa na tija kwa Tanzania? Kweli wengi humu wanachojua ni kuandika, kusoma na kuhesabu tu!!!
Unajua wao walichukua ngapi kupitia energy and mineral sector? We mwenzetu hata kujua kiasi hiki Cha Kusoma, kuhesabu na kuandika hujafikia pengine unajua tu kuuanisha rangi na picha za vitu😂😂😂
 
Na Bollen Ngetti
0683 226539
B-pepe bollenngeti@gmail.com

SIKU tatu kabla Rais Samia Suluhu Hassan hajaelekea Korea Kusini kuhenyea kwa ajili ya nchi yake niliandika huko kwa Max (X) kwamba, "Rais Samia unaenda Korea Kusini lakini jiandaye na matusi, kejeli , dhihaka na hata uzushi kutoka Marekani".

KWELI, Rais Samia Suluhu Hassan amefika Korea na kufanikisha dili la mkopo wa Shilingi 6.57 Trilioni wa sharti nafuu ikiwamo riba ya 0.01% kwa muda wa miongo 4 inayoanzia 2026. Fedha ambayo itaelekezwa katika miradi ya kimkakati inayolipa kama sekta ya usafirishaji na uchukuzi!

Mara baada tu ya Rais kufanikisha jambo letu HIMA Marekani kupitia sauti yake, Voice of America, VoA ikaandika uzushi, dhihaka na matusi kwamba, "Tanzania imesaini mkopo wa fedha na Korea Kusini kwa sharti la kugawa sehemu yake ya bahari na madini". Ujinga uliovuka mawingu!

Hivi, katika hali tu ya kawaida Rais Samia ni mwendawazimu, mjinga, asiye na akili wala uzalendo kiasi gani hadi atoe sadaka ya sehemu ya bahari na madini yetu kwa gharama ya mkopo ambao bado tutailipa? Kwa nini isingekuwa mbadilishano wa hayo matrilioni na kipande cha bahari na madini ili lojiki iwepo? Yani unaenda kwa Mangi unamwambia akukopeshe mchele wa kilo 50 kwa ajili ya shughuli ya binti yako utamlipa mwisho wa mwezi na hapo hapo unamwambia njoo nyumbani nikupe fremu bure pamoja na kwamba mchele wako nitakulipa mwisho wa mwezi! VoA na Joseph Biden mmetukosea sana kwa ujinga huu. We can be stupid but not fool to that extent!

Watanzania tuelewe mambo mawili hapa kama si moja kubwa! Na atakayeelewa awaeleweshe wengine 10 wasio na smart phones. Kwanza kuna vita kubwa ya kiuchumi duniani. Kila Taifa linatumia kila aina ya mbinu halali na haramu kujiweka sawa kiuchumi maana uchumi ndio kila kitu.

Na moja ya mbinu ya mataifa makubwa ni pamoja na kudhoofisha nchi zingine kiuchumi, kiteknolojia na ikibidi hata kisiasa na kijeshi. Marekani kupitia shirika lake la kijasusi ilitumia kila mbinu chafu kuwatenganisha ndugu wa tumbo moja KOREA ikazaliwa Korea Kusini na Korea Kaskazini huku USA ikilalia Korea Kaskazini na kumuona Korea Kusini kama "nunda" na adui. Korea Kusini imewekewa vikwazo chungu nzima na Marekani hasa katika eneo la ubunifu wa teknolojia ya zana za kivita bila mafanikio.

Wananchi wa Korea Kusini waliamua kushikamana na kujenga uzalendo kwa nchi yao wa kupigiwa mfano baada ya kuona, "hatuna ndugu wala mjomba, lazima tujikomboe wenyewe" na pakwanza walipoanzia na kupambana na kushinda saratani ya rushwa na ufisadi na kumtambua kila Mkorea Kusini alipo ndani na nje ya nchi yao na anafanya nini kwa maslahi ya Korea Kusini!

Nimkumbushe Mtanzania jambo ambalo limewahi kutokea lakini haikuandikwa popote na kokote rasmi! Miaka michache tu zilizopita Jeshi letu la Ulinzi limewahi kuwa na haja ya Rada kwa ajili ya Ulinzi wa anga ambayo ingefungwa Morogoro. Maombi yalienda kwa nchi nyingi ikiwemo USA ya Joseph Biden aka Joe Biden bila mafanikio.

Ni hawa hawa Korea Kusini walikubali kutufungia mitambo hiyo tena kwa "Siri Kubwa" Marekani isijue maana ingeleta mushkeli wa kidiplomasia kati yetu na wao. Wakijifanya wakulima wa mboga -mboga mchana lakini kumbe ni mainjinia walifuzu, Wakorea walifunga mitambo.

Hata hivyo USA ilipogundua ilileta shida lakini kwa ukomavu wetu wa kidiplomasia Tanzania ya Jakaya Kikwete iliwaambia USA, "sisi tuna shida ya Rada, kama hamtami hawa watufungie basi mtupe yenu". USA ilikubali lile sharti na Korea Kusini ikafungasha virago maana na wao hawakuona sababu ya magomvi yao kutuathiri. Tuna historia ndefu na Korea Kusini kuliko USA kama nitakavyoeleza kupitia gazeti moja ya gazeti la wiki!

Kwa mantiki hiyo sikushangaa hata kidogo kwa Marekani kupitia TBC yao ya umma kutoa uzushi wa kijinga wenye lengo la kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wake kupitia mawakala wao ndani ya nchi kusambaza ujinga huo kuelekea Uchaguzi wa S/M kisha Uchaguzi Mkuu 2025 kwamba "Samia anauza nchi yetu" ili tu Samia achukiwe na chama chake! Huu ni uzushi wa kipumbavu usiovumilika na ninaamini USA itaomba radhi.

Tanzania ni nchi huru na sera yetu siku zote ni kutokufungamana na upande wowote katika vita za kiulimwengu. Hatuchaguliwi adui wala rafiki. Tunachoangalia ni maslahi mapana kwa nchi yetu na watu wake. Leo Iran imewekewa kila aina ya vikwazo vya kiuchumi lakini sisi ni marafiki na Iran na tunafanya nao biashara chungu mzima ikiwemo gesi asilia.

RAIS Samia wewe piga kazi! Hizo ni kelele tu za chura! Wewe hata chama Cha Hamas kikikubali kutujengea Zahanati kila kila Kijiji wewe nenda kasaini mikataba. Tungesikia kelele zao leo tungekuwa na Hospitali ya Palestina pale Sinza? Uongo ukiachwa kusikika sana hufikia hatua ya kuaminika kuwa ni kweli. Ukemewe mapema na kila mzalendo wa nchi YETU!
04/6/2024
Time: 11:23
Dar es salaam

Pia soma: VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Acha uzwazwa, walio toa taarifa ya mikataba hiyo ni wakorea wenyewe, na iko wazi, acha porojo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom