kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Umepoteza muda wako na ukapoteza wa kwangu pia. Kweli tz watu wana uhuru mpana wa kutoa maoni yao.View attachment 3528131
Hakuna namna ya kuficha ukweli huu kwa mapambo ya maneno: udhaifu wa Rais wa sasa unatokana moja kwa moja na ukweli kwamba hana uhalali wa kisiasa wala wa kimaadili. Huyu si Rais wa ridhaa ya wananchi, bali ni Rais wa nguvu, vitisho, na damu ya raia. Msingi wa madaraka yake haukujengwa kwa kura huru na ya haki, bali kwa matumizi ya jeshi, polisi, na vyombo vya dola vilivyogeuzwa silaha dhidi ya wananchi waliodai haki yao ya kidemokrasia.
Rais anayepatikana kwa njia hiyo hawezi kamwe kuwa kiongozi jasiri. Hawezi kujiamini. Hawezi kuheshimu wananchi. Na hawezi kuongoza kwa maono. Ndiyo maana kila hatua anayochukua ina harufu ya hofu na kujinusuru, si uongozi. Teuzi za kuwateua viongozi wastaafu kama washauri wake si ishara ya hekima; ni ishara ya panic, ni dalili ya Rais anayejua kuwa amekataliwa na wananchi.
Tatizo si hao washauri. Tatizo ni Rais ambaye anafahamu kuwa yuko madarakani kinyume cha ridhaa ya umma. Rais halali hutegemea kura; Rais haramu hutegemea bunduki. Rais halali hutegemea taasisi; Rais haramu hutegemea watu wachache anaowajua. Rais halali husikiliza wananchi; Rais haramu huwatisha wananchi. Hii ndiyo sababu Rais huyu hawezi kusimama peke yake anajificha nyuma ya majina ya zamani ili kuhalalisha uongozi ambao kimsingi hauna uhalali.
Leo hii kuna civil disobedience kubwa nchini wananchi hawamtii Rais kimaadili, hawamwamini, na hawajioni sehemu ya serikali yake. Hata pale ambapo hakuna maandamano ya wazi, kuna kutotii kwa kimya kimya, kuna kukataa kiroho na kisaikolojia, kuna kuvunjika kwa mkataba wa kijamii kati ya dola na raia. Serikali inayopendwa haiogopi wananchi; serikali inayochukiwa huishi kwa hofu ya wananchi. Ndiyo serikali hii.
Katika mazingira haya, Rais analazimika kujikusanyia “ngao za kisiasa” kwa kuwateua watu wa zamani anaodhani watampa uhalali wa bandia. Lakini uhalali haupatikani kwa teuzi. Haupatikani kwa vyeo. Haupatikani kwa mikutano ya siri. Uhalali hutoka kwa wananchi na wananchi tayari wamesema HAPANA.
Teuzi hizi zinafichua ukweli mchungu: Rais anajua kuwa hana mizizi kwa wananchi, hana imani hata na mfumo wake mwenyewe, na hana ujasiri wa kukabiliana na hasira halali ya umma. Huyu ni Rais anayeongoza kwa kuahirisha kuanguka, si kwa kuongoza taifa. Kila uteuzi ni jaribio la kununua muda, si kutatua tatizo.
Historia haidanganyiki. Serikali zilizojengwa juu ya mabavu, damu, na wizi wa kura huanguka si kwa sababu ya upinzani pekee, bali kwa sababu hazina uhalali wa kuishi. Teuzi za washauri wastaafu hazitabadilisha ukweli huo. Haziwezi kuzima hasira ya wananchi. Haziwezi kufuta damu iliyomwagika. Na haziwezi kuhalalisha uongozi haramu.
Kwa kifupi, Rais huyu si dhaifu kwa sababu anawateua washauri; anawateua washauri kwa sababu ni dhaifu. Dhaifu kwa sababu hana kura. Dhaifu kwa sababu hana ridhaa. Dhaifu kwa sababu anaogopa wananchi. Na kiongozi anayewaogopa wananchi wake tayari ameshindwa haijalishi ana madaraka kiasi gani.
Wapo watu ambao walitaka Samia atende kinyume cha Katiba ya 1977 ili waje na hoja ya amevunja katiba, na wako watu ambao waliotaka Samia afuate maelekezo yao badala ya Katiba au airekebishe Katiba kwa maelekezo yao tu. Baada ya haya yote kushindikana ndipo wakaenda kuchoma mali za watanzania wenzao kwa kisingizio cha kudai haki.
Kila nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo hata kama kuna mtu anaona Katiba ni mbaya kwake. Lazima mtu huyo avumilie tu hadi hapo katiba itakaposema vinginevyo. Hata Kama ukipeleka kesi yako Umoja wa mataifa au ICC kuhusu Samia au Serikali watapanda ndege kwenda huko wakiwa na katiba na sheria za nchini kwenye mabegi yao. Chaguzi zetu zinaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu hata Kama Katiba na sheria zetu ni mbaya sana. watanzania Tumepatana wenyewe malipo ya dinali moja kila mwezi tutalipana dinali moja kila mwezi hadi hapo tutakapokaa kitako tena wenyewe na kukubaliana ujira tofauti kwa kazi ileile. Shida yetu tuna malofa ambao anajifanya wanatujua sana sisi watanzania na kutaka kutusemea na kutuamulia bila sisi wenyewe kuwatuma. Wanatoka hadharani na kusema watanzania wanataka katiba mpya badala ya kusema mimi na mke wangu tunataka katiba mpya. Ukimuuliza hao watanzania ni akina nani, wako wangapi, wanaume au wanawake na mlikutana wapi wakakwambia hayo wanakunja ngumi. Huo ni ulofa na ujinga.