Samia Suluhu ni Rais Haramu, Serikali ya Hofu, na Teuzi za Kujinusuru

Umepoteza muda wako na ukapoteza wa kwangu pia. Kweli tz watu wana uhuru mpana wa kutoa maoni yao.

Wapo watu ambao walitaka Samia atende kinyume cha Katiba ya 1977 ili waje na hoja ya amevunja katiba, na wako watu ambao waliotaka Samia afuate maelekezo yao badala ya Katiba au airekebishe Katiba kwa maelekezo yao tu. Baada ya haya yote kushindikana ndipo wakaenda kuchoma mali za watanzania wenzao kwa kisingizio cha kudai haki.

Kila nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo hata kama kuna mtu anaona Katiba ni mbaya kwake. Lazima mtu huyo avumilie tu hadi hapo katiba itakaposema vinginevyo. Hata Kama ukipeleka kesi yako Umoja wa mataifa au ICC kuhusu Samia au Serikali watapanda ndege kwenda huko wakiwa na katiba na sheria za nchini kwenye mabegi yao. Chaguzi zetu zinaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu hata Kama Katiba na sheria zetu ni mbaya sana. watanzania Tumepatana wenyewe malipo ya dinali moja kila mwezi tutalipana dinali moja kila mwezi hadi hapo tutakapokaa kitako tena wenyewe na kukubaliana ujira tofauti kwa kazi ileile. Shida yetu tuna malofa ambao anajifanya wanatujua sana sisi watanzania na kutaka kutusemea na kutuamulia bila sisi wenyewe kuwatuma. Wanatoka hadharani na kusema watanzania wanataka katiba mpya badala ya kusema mimi na mke wangu tunataka katiba mpya. Ukimuuliza hao watanzania ni akina nani, wako wangapi, wanaume au wanawake na mlikutana wapi wakakwambia hayo wanakunja ngumi. Huo ni ulofa na ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…