Pre GE2025 Samia Teachers Mobile Clinic inayoratibiwa na CWT inatarajiwa kusikiliza changamoto mbalimbali za walimu Geita

Pre GE2025 Samia Teachers Mobile Clinic inayoratibiwa na CWT inatarajiwa kusikiliza changamoto mbalimbali za walimu Geita

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto za walimu nchini (Samia Teachers Mobile Clinic) inayoratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kushirikiana na serikali inatarajia kuwasili mkoani Geita Februari 25, 2025 na kumalizika tarehe 26 Februari ambapo lengo ni kusikiliza changamoto mbalimbali za walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za CWT mkoa wa Geita Katibu wa CWT mkoani humo Pauline Tinda amesema changamoto ambazo zinatazamiwa kushughulikiwa ni pamoja na walimu ambao wana matatizo ya kimuundo, mishahara isiyolipwa kwa ajira mpya, mapunjo ya mishahara kwa muda mrefu pamoja na walimu ambao wamekuwa na shida ya vyeo kwa kutopandishwa madaraja na vyeo vya mseleleko.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameongeza kuwa tayari wameshatenga vituo vitatu ambapo kituo cha kwanza ni Wilaya ya Bukombe ambacho kitatoa huduma kwa walimu wa Bukombe pamoja na Mbogwe, Chato na siku ya tarehe 26 kituo kikuu kitakuwa kwenye shule ya wasichana ya sekondari ya Nyankumbu iliyopo Manispaa ya Geita ambapo watatoa huduma kwa Walimu wa Wilaya ya Nyang’hwale Halmashauri ya Wilaya Geita pamoja na Manispaa ya Geita.

Pia ziara hiyo inaendeshwa kupitia timu ya Maafisa kwa kuhusisha Maafisa kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Wizara ya fedha na Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Walimu.

Ziara ya Samia Teachers Mobile Clinic inayoendelea kutoa huduma kwa walimu ni hatua muhimu katika kuboresha sekta ya elimu nchini. Hii inawawezesha walimu kujikita zaidi katika kazi yao ya ufundishaji, kwa kuwa huduma zao zitaboreshwa na kupunguza mzigo wa matatizo yanayoweza kuathiri utendaji wao.

 
Back
Top Bottom