GE2025 Samia: Tujitokeze kwa wingi Oktoba 29 tuwazibe midomo

GE2025 Samia: Tujitokeze kwa wingi Oktoba 29 tuwazibe midomo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kukichagua CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiahidi kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kusogeza huduma za kijamii karibu yao zaidi na kustawisha uchumi kama shabaha ya kukuza utu wa Mtanzania kwa miaka mitano ijayo.

"Watu wengi sana wanajitokeza kwenye mikutano, mnaweza mkafikiria Chama cha Mapinduzi kimeshashinda mkalala usingizi. Niwaombe sana hatuko peke yetu, uchaguzi huu unasimamiwa na watu wengi na jinsi tunavyojaa kwenye mikutano yetu hivyo hivyo tukajae kwenye masanduku ya kura na hivyo ndivyo tutakavyoweza kuwaziba midomo wale ambao wana midomo kwa Tanzania," amesema Samia.

Samia amebainisha hayo leo Jumanne, Septemba 30, 2025 wilayani Korogwe, akiwa njiani kuelekea mkoani Kilimanjaro kwenye Wilaya za Same na Mwanga, akiwashukuru wananchi wa Mkoa huo na hususan Korogwe kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ya kampeni aliyoifanya tangu Jana Jumatatu kwenye Wilaya za Pangani na Handeni na Tanga Mjini.

Pia Soma: GE2025 - Samia: CCM tunataka ushindi wa heshima tuwazibe midomo wale wengine
 
Huyu hana uwezo wa kuwaziba midomo watu kwa njia ya kura, ndiyo maana ameamua kuwaziba watu midomo kwa njia za kishetai za kuwateka na kuwaua watu. Ametuvunja sana mioyo, na kutuaibisha kwa kiwango cha ajabu, sisi sote tuliowahi kumwunga mkono.

Laana ya Mungu, tunaomba iwe juu ya mtu huyu na kizazi chake, kutokana na mauaji na dhuluma alizozifanya.
 
Back
Top Bottom