Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri

Pascally siku hizi uzee unamuandama kiasi hata uwezo wa kufanya uchambuzi hana tena.
 
Nadhani umerejea kwenye lile umbo lako la asili, sio ambalo ulikuwa nalo hapo juzi Kati kumfueahisha mwendazake.
Be blessed ndugu Pascal Mayalla
 
Inategemewa kabisa kwamba baada ya Magufuli mitazamo kama hii, ya kuonekana awamu ya Magufuli ilikuwa si chochote wala si lolote, ingejitokeza. Utawala wa Magufuli ulikuwa nira nzito kwa watu wote wanaotaka serikali iwe "easy-going" katika utendaji wake, nikidesa msemo wa jarida la Economist.

Kama kuna ufisadi ulifanyika enzi ya Magufuli hauwezi kulinganishwa na awamu iliyopita. Na wala hakuna mwenye ndoto kwamba utawala wa Magufuli ulikuwa hauna kasoro kabisa.

Na wala hakuna utawala kamilifu, kama mtawala ni mwanadamu. Ila kitu kinachotanabaisha utawala wa Magufuli kama miongoni mwa tawala bora kabisa kuwahi kuwepo katika nchi yetu, ni utawala uliotuonyesha kwamba inawezekana, na kwamba kila kitu kiko ndani yetu, hatutaangalia nje kwa msaada.

Sasa, kuna watu kama the Economist wanaojaribu kukoleza doa utawala wa Magufuli, na kujaribu kubadlilisha mtazamo wa mama ili afuate nyendo potofu. Mama ni mwanadamu, na anaweza kupotoka, ila kuna nguvu kubwa nyuma yake ambayo haitakubali dhana potofu zipate nafasi. Ameonyesha dalili za kuanza vizuri, mfano hajakubali legacies za bosi wake (Magufuli), ikiwemo mtazamo wa bosi wake kuhusu uviko19, kuwa havina maana tena. Magufuli was no saint, lakini alikuwa anajua nini watanzania wanataka.

Na somo la Magufuli litumike kama somo kwa wanasiasa wote. Kama wanataka kuwa relevant katika siasa zao, mtanzania wa kawaida ndie mteja wao nambari one. Sisi watanzania wa kawaida tuna nguvu kubwa sana kuliko mnavyofikiria. Tunataka barabara safi, huduma za afya bora, na maisha bora kwa ujumla. Pia tunataka heshima yetu kama binadamu, tuna dignity. Hatutakubali kuona viongozi wetu wanatukuza kitu kingine chochote zaidi ya dignity ya utanzania na mtanzania.
 
Mkuu Pascal Mayalla

Kwanza, ahsante kwa kurejea na kuua tetesi. Wapo waliosema ulionekana na sufuria la majani ukiwa umedhoofu, wengine wakisema ulionekana na suti mpya ya bluu maeneo karibu na wizara ya elimu zamani na mkoba umeandikwa designated DC n.k. Usiwajali waosha vinywa muhimu umerudi

Kuhusu Rais Samia, tukiri kuwa anaishi na kufanya kazi katika damage iliyosababishwa na mwendazake.

Mfano sheria zote zilizowekwa haraka haraka zingine zikilenga watu na si nchi zipo na zitaendelea kuwa na nguvu na kuwa abused na watu wasio na mapenzi mema. Moja ni hii ya 'Money Laundering'

Sijui Rais Samia atafanya nini kuhusu hizi sheria za hovyo.

Pili, ''recycling' ya watu wale wale waliotufikisha hapa haitamsaidia. Lini watu hao walitubu kuacha unafiki?

Tatu, kuna mambo yatakayomkwaza Rais Samia na nasikitika kuona hajayashugulikia.

Rais alitakiwa asafishe safu ya wapiga debe na ili kujipa nafasi ya kutenda

Rais angeanza na Mwanasheria mkuu kwanza kwani kuna kitu nakiona hakipo sawa.

Chama cha Wanasheria TLS kilitoa muongozo wa katiba katika Mazingira ya dharura kama ya kifo.

TLS walieleza kukoma kwa baraza la mawaziri na viapo visivyohamishika kutoka kiongozi kwenda mwingine.

Nashangaa kinachoendelea ni tofauti kabisa na kujiuliza hivi akina Rugemeleza Nshala na wenzake hawakusoma katiba vizuri au Mwanasheria mkuu hakusoma vizuri. Kuna tatizo mahali na sijui kama Mheshimiwa ameliona!

TLS tunaomba mtusaidie ufafanunuzi kwani tumechanganyikiwa.

Moja ya makosa ya Mwendazake ni kitendo cha kutoheshimu katiba na kutaka yeye awe katiba na kila kitu
Zama hizo zimepita , swali je Rais Samia atarithi makando kando ?

JokaKuu
 

Mkuu zimmerman, hitimisho lako linaakisi matumaini ya Watanzania wengi na si ya hao wachache, na hasa wanasiasa wachumia tumbo. Hawa madai yao muda wote ni demokrasia yenye Uhuru usio na mipaka na Haki pasipo kuwajibika.

Hayati Magufuli katika mengi mazuri aliyoyafanya, na kwa kauli za Rais na Makamu wake, kwa sasa, yamegusa maslahi mapana ya kitaifa, km:
√ Uwajibikaji wa viongozi wa umma kwa wananchi; na
√ Kusimamia kwa weledi rasmali za nchi, ikiwa ni pamoja na makusanyo ya kodi na matumizi yake, kwa maendeleo ya nchi.

Hayo ndio mambo mawili makuu yanayomtofautisha Hayati Magufuli na watangulizi wake, hata Marais wengi barani Afrika. Matokeo yake, tumeshuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa, yenye kuchochea kukua kwa uchumi, kwa fedha za ndani. Tumethibitishiwa kuwaTanzania ni tajiri hatuhitaji kutembeza bakuli la ombaomba.
 
Mkuu Pascal Mayalla

Kuhusu Rais Samia, tukiri kuwa anaishi na kufanya kazi katika damage iliyosababishwa na mwendazake.

JokaKuu

Nafikiri ulitizame kivingine. Kwamba rais SSH anaishi na kufanya kazi katika positive image iliyosababishwa na mwendazake.

Wakati Kikwete anaingia madarani alisema anafurahi kuingia madarakani akirithi nchi yenye uchumi imara. Sasa rais Samia, japo hajasema, anaingia madarakani huku akiwa amerithi nchi yenye uhuru kamili, ikiwemo wa kiuchumi.

Leo hii hakuna mtanzania anayefikiri kwamba maendeleo ya nchi yake yanategemea kudra au msaada nje ya nchi yake.

Na nimemsikia Mpango akimwagiza Mwigulu kuongeza wigo wa kukusanya kodi hadi wastani wa trillion 2 kwa mwezi. Si mwanzo mbaya!
 
We Pascal Mayalla unajua wazi kuwa wenye akili ya kujiongeza walikuwa hawamkubali marehemu.
Marehemu aliwapenda wajinga wajinga... Unakumbuka lile swali lako kuhusu ukuu wa mihimili mitatu ya dola? Kama ulipewa majibu na ukaridhika naomba uwalaumu The Economist
 
Ndugu Mwengeso,

Nafurahi kuona kwamba kuna watanzania wengi wenye mtazamo kama wetu, kama wewe.

Kwa bahati mbaya baadhi ya watanzania wenzetu hawajatembea nchi za wenzetu, au kuinteract na watu wa nchi za magaharibi kupata ladha ya nini wanasema, kuwaza au kufanya kuhusu nchi zetu. Kama wangefanikiwa, bila shaka wangekuwa upande wa Magufuli.

Mfano, wazungu wengi wanafikiria kwamba waafrika ni watu wenye IQ ndogo sana, na hatuwezi kuendelea sisi wenyewe hivyo tunahitaji either kusaidiwa au kutawaliwa. Wamerank IQ za ethniticities kwamba wa kwanza ni Semitics na Asians (wayahudi na jamii ya wachina wakiwemo wahindi na wachina), wa pili ni Caucasians ( wazungu), na wa mwisho ni Africans.

Sasa mimi huchukia sana ninapoona baadhi ya watanzania na waafrika wenzetu kwa ujumla wanavyoonyesha live kwamba kweli race yetu pengine ni kweli ya mwisho kwenye IQ. Kwa mfano, ninapoona baadhi ya watanzania wenzetu wanavyopotezwa na narratives za wazungu kiasi cha kubeba kila kitu kinachoandikwa au kusimuliwa na vyombo vya habari vya wazungu kuhusu nchi zetu, au kufikia levels za kununuliwa na wazungu ili kufifisha juhudi za nchi yetu kujikwamua, huwa najiwazia kwamba nchi zetu zina watu wenye IQ ndogo.

Lakini pia natiwa moyo na watu kama wewe kwamba, hapana, nchi zetu bado zina watu ambao Mungu anaweza kuwatumia kuleta uamsho. After all binadamu wote ni sawa, na Mungu wetu ni mmoja, dunia yetu ni moja na Mungu hana upendeleo.
 
Kutoa data za corrona zinasaidia nini mataifa yanayotoa data corrona mbona ndo imepamba moto? Lockdown,vaccine,mask mbona hazijawaokoa?
Rais afuate msimamo uleule siyo kutaka kuwafurahisha mabeberu.
 
Here we go 🕺
 
Sheria nyingi zimetungwa kwa kukidhi haja za mtu na si za nchi. Sheria zimetungwa kulenga watu na si tatizo

Unakumbuka sheria ya viongozi wa mihimili kutoshtakiwa ilianzaje!

Hakukuwa na uhuru bali woga! watu walijificha na kuhofu kila uchao. Huo ndio uhuru?

Uhuru upi wa uchumi wakati deni la Taifa limefikia mahali pabaya hata kutia shaka ya kukopesheka!
 
Tunawaza tofauti. Mimi nawaza maslahi ya nchi kwa ujumla wake. Yaani, ni kitu gani au sera gani ineleta impact ya kiuchumi kwa watanzania kwa ujumla wao, wewe unawaza mtu.

Sheria ya mihimili kutoshtakiwa haina shida. Tatizo lako unawaza mtu binafsi badala ya mhimili. Haina shida mhimili wa uraisi kutoshtakiwa. Urais ni alama ya utaifa, kushtaki urais ni kujishtaki kama taifa. Rais, kama mtu, akiwa mbovu kuna solutions zake. Ya kwanza ni kuwa voted out of the office. Ya pili ni kumaliza muhula na kusepa zake.

Mwinyi na Kikwete urais wao haukuwaridhisha watu wengi. Lakini walimaliza ngwe zao na wamebaki historia na funzo ya nini rais hapaswi kufanya. Trump amemaliza urais wake na akawa voted out. Wamejaribu kumimpeach lakini bila shaka kile kilikuwa kiinimacho. La kuzingatia ni kwamba tukifahamu maslahi ya nchi ni yepi, tutaweza kutofautisha kati ya mtu na kile anachokisimamia au kukihubiri.
 
Unaandika utafikiri unapiga umbeya viunga vya Lumumba.

Learn to highlight your key points
Paskali hapa anafeli sana na kwavile anajua ukitaka kumficha mwafrika weka kwenye maandishi basi nae anatembea humohumo
 
Paskali hapa anafeli sana na kwavile anajua ukitaka kumficha mwafrika weka kwenye maandishi basi nae anatembea humohumo
Mwafrika msifie, mpe chakula ukimaliza mpe pombe. Umemaliza, unaweza kumfur**** kabisa.
 
Kuhusu corona, wasitupangie.
Utapangiwa utake usitake. Hatuishi mbinguni, ugonjwa huu ni hatari. Ukikupata ndio utaujua au kuusahau moja kwa moja. Tatizo wewe hutaki kukubali ukweli. Ukimwi ukiupata ni wewe tu lakini huyu corona anakumaliza wewe au mimi na familia zetu. Tuendelee kuchukua tahadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…