Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake ya awamu ya sita kwa kushirikiana na ile ya awamu ya tano zimefanikiwa kutekeleza kwa vitendo maono na fikra za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika kujenga taifa imara, linalojitegemea na linalowajali watu wake.
Dkt. Samia alitoa kauli hiyo leo, Jumatano Oktoba 14, 2025, wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 26 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — kiongozi na muasisi wa nchi aliyejenga misingi ya taifa katika itikadi na falsafa za kujiletea maendeleo, kupambana na umaskini, ujinga na maradhi.
“Tunapomzungumzia Baba wa Taifa hatuwezi kumtenganisha na misingi ya kiitikadi na kifalsafa aliyojenga kupitia dhana mbalimbali. Alisisitiza kuwa maendeleo yenye maana lazima yawalenge watu. Ndiyo maana dira na mipango yetu yote ya maendeleo pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi inajielekeza kujenga taifa linalojitegemea, lenye uchumi jumuishi na ustawi wa watu,” alisema Dkt. Samia.
Akiwa Butiama, mkoani Mara, mnamo Oktoba 10, 2025, alipozaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa, Dkt. Samia alisema serikali yake imefanikiwa kutimiza maono ya Mwalimu Nyerere kwa vitendo kupitia miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo ujenzi na ukamilishaji wa mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, unaozalisha zaidi ya megawati 2,000 za umeme na kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa umeme nchini.
Aidha, ametaja miradi mingine inayotekelezwa kuwa ni uhamisho wa makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, ambapo mihimili yote ya serikali sasa imehamia mkoani humo; ujenzi wa mradi wa maji wa Same–Mwanga–Korogwe, bwawa la Mkomazi (Korogwe) lililofikia asilimia 50 ya utekelezaji, na bwawa la Kidunda, ambalo litakapokamilika litasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Morogoro na maeneo jirani.
“Baba wa Taifa alituachia misingi mizuri ya kifalsafa, kisera na kisiasa. Kazi yetu kama viongozi ni kutafsiri misingi hiyo katika mazingira ya sasa. Dira, mipango na ilani ya uchaguzi ya CCM zinatafsiri fikra hizo kwa vitendo — kujenga taifa.