GE2025 Samia: Tunaahidi na kutekeleza tofauti na vyama vingine

GE2025 Samia: Tunaahidi na kutekeleza tofauti na vyama vingine

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema tofauti na vyama vingine vya siasa, CCM ndicho chama pekee chenye rekodi ya kutekeleza ahadi zake na kueleza wazi namna ya utekelezaji wake.

Akihutubia maelfu ya wananchi mjini Songea leo Jumatatu, Septemba 22, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya VETA, Dkt. Samia amesema vyama vingi vimekuwa vikiahidi mambo yaliyoandikwa tayari kwenye Ilani ya CCM, lakini tofauti kubwa ipo kwenye namna ya utekelezaji.

“Nimekuwa nikiwasikiliza ndugu zangu wanaozunguka kama mimi na yale wanayoyasema kwenye sera zao. Kila nikisikiliza ni yale yale yaliyomo kwenye Ilani ya CCM, lakini sisi tukiandika tunajua tutatekeleza kwa njia gani, fedha itatoka wapi na namna ya kukamilisha tunayoyasema. Suala sio tu kusema, suala kubwa ni namna ya kufanya. CCM tunasimama kwa ujasiri kuomba kura kwa sababu tumefanya mmeona, na tunaamini tutafanya na mtaona,” amesema Dkt. Samia.

Katika hotuba hiyo, ameeleza pia mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta za afya, maji, elimu na umeme, akisema serikali ya awamu ya sita imevuka malengo ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, huku miradi mingine mingi ikiendelea kutekelezwa nchi nzima.​

Aidha, Dkt. Samia ametumia nafasi hiyo kuwaombea marehemu watatu na mjeruhi mmoja waliopata ajali wakati wa shughuli za uchimbaji madini mkoani Ruvuma, akiwafariji familia zao na jamii kwa ujumla.​
 
Out of curiosity...zile ahadi za flyover 7 Dsm zilikua ni ahadi za kwenye ilani ya 2020 au chombeza za slow slow?
 
Aisee awamu hii Tanganyika tumepatwa.

Nadhani kama nchi, haijawahi kutokea tangu tupate uhuru kuwa na wagombea wa aina hii. Ukienda kuwasikiliza na wale wenzake wengine aliowanunulia magari kwa kutumia kodi zetu, na kwenyewe ni vichekesho tu.
 
Yani too low !
Watu mnawateka.
Watu mnawauwa.
Watu mnawaibia kura.
Watu mnawafyeka kabla.
Watu mnawapa kesi.
No fairness
Sasa hiyo nafasi ya kutekeleza hizo ahadi wanapata wapi?
Yani mpaka kero kumsikiliza.
 
Wanaahidi na kutekeleza machache kwa kodi za wananchi hakuna chama kilishashika dola zaidi yao
 
Back
Top Bottom