GE2025 Samia: Tutaendeleza mchakato wa Katiba Mpya kama ilivyo katika ilani yetu ya CCM

GE2025 Samia: Tutaendeleza mchakato wa Katiba Mpya kama ilivyo katika ilani yetu ya CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza kwamba katika kutambua umuhimu wa mshikamano kwa Watanzania wote, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena, atahakikisha Serikali yake inaendeleza mchakato wa kupata Katiba mpya kama ilivyoainishwa katika Ilani ya uchaguzi ya chama chake ya mwaka 2025-2030.

Akiwa katika kampeni zake wilayani Butiama mkoani Mara leo, Oktoba 10, 2025, Dkt. Samia pia amesisitiza kwamba suala la Katiba mpya ni hitaji la makundi mbalimbali ya watu kwa nyakati tofauti, na ameongeza kuwa, licha ya mchakato huo kutokamilika katika awamu ya nne, yeye atahakikisha unaendelezwa katika kipindi chake cha uongozi.
 
Back
Top Bottom