Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kujengwa kwa reli ya kisasa yenye urefu wa takribani kilomita 1,000 itakayoanzia Mtwara hadi Mbamba Bay, mkoani Ruvuma.
Akihutubia mkutano wa kampeni leo Septemba 22, 2025 mjini Songea, Samia amesema reli hiyo itakuwa chachu ya kukuza uchumi kwa kurahisisha usafirishaji wa madini ya Liganga na Mchuchuma pamoja na mazao mbalimbali ya kilimo kutoka kusini mwa Tanzania.